Vitu kumi vya kufanya kama hujaajiriwa

Vitu kumi vya kufanya kama hujaajiriwa

Verdy CB

Senior Member
Joined
Mar 19, 2013
Posts
149
Reaction score
66
Ajira zimekua ngumu kupatikana siku hizi bila kujali unamjua nani au nini ukijuacho.
Hivi vitu kumi vitakusaidia kukuongezea ubunifu na kukuweka katika hali nzuri katika soko hili la kutafuta ajira.

1. Andaa Ratiba.
Wengi huwa wana tabia ya kujiendekeza mara baada ya kukosa ajira. Ila pale utakapoandaa ratiba yako itakusaidia kuwa makini zaidi. wahi kuamka, jipange, pata muda wa kutafakari. Huwez jua unaweza pata hata bonge la wazo la biashara.

2.Tafuta ajira ya muda (Tempo)
Hii itasadia katika kutengeneza daraja kati yako na ajira mpya ya kuduma. Itakusaidia pia kuongeza ujuzi na uwezo wa kifedha mpaka pale utakapopata ajira ya kudumu.

3. Fanya kazi mtandaoni.
Kama wewe ni graphics designer, mchoraji, msanii, mwandishi au mwalimu. Upo katika nafasi nzuri ya kupata ajira mtandaon katika mitandao halali kama Freelancer, Guru na Elance. Hata ukianza kwa $5-$500 kwa mwezi si haba.

4. Jipange.
Angalia nini unachohitaji na usichohitaji ndani mwako na utafute namna ya kukitumia au kukitoa mbali ya uwepo wako kwa mpagilio mzuri.

5. Piga mazoezi.

6. Ongeza ujuzi wako.
kupata stadi mbalimbali hakuhitaji ulipie. unaweza ukajifunza zaidi kuhusu interviews na vitu mbalimbali kupitia elimu ya mtaa. Hii itakusaidia katika kutafuta kwako ajira.

7. Jitolee (volunteer)
Ukiwa unajitolea katika makampuni au taasisi mbalimbali unaongeza exposure yako katika tasnia hii.

8. Jitoe na jipende.
Hata kama huna hela unaweza ukatembea kidogo au kujisogeza kando ya bahari. Beach nyingi na tulivu unaweza pata hata ambazo hazina kiingilio. Hii itakusaidia kurelax na kupata muda kuuchangamsha ubongo n mwii.

9. Angalia kipi unachoweza kuuza.
Sisemi uuze vyote vilivyopo ndani. Ila angalia na umuhimu wa hicho kitu na thamani yake. kwa walio majuu mitandao kama Amazon na ebay itawarahisishia kazi yao. Ila hata kwa bongo siku hizi kuna mitandao kama hii pia.

10. Soma kozi yoyote.
Jaribu kupiga kozi mbalimbali kupitia taasisi zinazojulikana ili kupata cheti na kuipa mwanga mpya resume yako. Hii inaweza kuwa na gharama kubwa kama hivyo unaweza kusoma mtandaon kupitia taasisi zinazotoa elimu ya bure. Jaribu kuchek hapa 25 Killer Sites For Free Online Education

Natumaini vidokezo hivi vinaweza kukusaidia.

kwa msaada wa mtandao 24tz
 
Unaweza pia ukaenda magereza ya kilimo ukajifunza kilimo cha kisasa ..
Ova.
 
kabisaa, tatizo watu wanasubiria za maofisini za kuvaa tie.

Verdy, me nmejaribu kukonect na hivi vyuo lkn nmeona kuna kaugumu fulani kujiunga nao... au kwa vle na2mia cmu? msaada plz...
 
Verdy, me nmejaribu kukonect na hivi vyuo lkn nmeona kuna kaugumu fulani kujiunga nao... au kwa vle na2mia cmu? msaada plz...

Ugumu gan mheshimiwa?? au jaribu kwa kutumia pc then niambie ilivyokuwa. Nione nitakavyoweza kusaidia
 
Thus why naipenda jf, kila cku najifunza vitu vipya. ubarikiwe mkuu kwa modality yako.
 
kama ajira hakuna nenda hata driving school upate leseni ya daladala au maroli kisha jichanganye

hii point,kuna jamaa ni graduate anaendesha tank la mafuta kwenda rwanda kwa mwezi mileage plus mshahara anafunga zaidi ya m.na akirudi nyumbani kuna nukia i mean kuku,mkaa,mafuta ya kula ,mbuzi matunad ,mchale etc,asali ya tbr,etc,etc...waliiogpa kujichanganya mpaka sasa wanasota na mshikaji anawatoa nauli waendele kutembea na bakhasha ya khakhi
 
ukitaka ushuhuda nitakutajia watu wengi sana ambao wameanzia kwenye malori hivi siku hizi wanapewa hadi mikataba waache waendelee kusota
 
mkuu umeongea la maana sana kwani itawasaidia vijana wengi wanaojitambua na kufanya kile kinachowezekana pasipo kukaa kusubiri ajira za kuvaa tai na skuna

hata kwenye ikilimo siku hizi kinalipa sana ni bora mtu akatambua ana nini cha uwezo wake wa kukifanyia kazi akajitoa kwa hiilo ndipo ataona mafanikio yake hapo mbeleni sio kukaa na kusubiria ajira kwani ngumu kupatikana labda kwa sala
 
Verdy CB umetoa mada nzuri sana. Mimi binafsi niliacha kazi ya kuajiriwa na kuanzisha project ya ku design logos. Na sasa napiga kazi kuanzia Bongo hadi Kenya. Nimepata clients UK hadi Palestine, Sweden, India nk. Nilipoanza sikutafuta ushauri kwa mtu ( maana wakati mwingine tunakatishana tamaa) bali, nilimtanguliza Mwenyezimungu kisha nikafanya kazi kwa bidii na uaminifu. Na sasa mafanikio ninayaona.
Pls pitia blog yangu:
http://logoriddims.blogspot.com
 
Last edited by a moderator:
Verdy CB umetoa mada nzuri sana. Mimi binafsi niliacha kazi ya kuajiriwa na kuanzisha project ya ku design logos. Na sasa napiga kazi kuanzia Bongo hadi Kenya. Nimepata clients UK hadi Palestine, Sweden, India nk. Nilipoanza sikutafuta ushauri kwa mtu ( maana wakati mwingine tunakatishana tamaa) bali, nilimtanguliza Mwenyezimungu kisha nikafanya kazi kwa bidii na uaminifu. Na sasa mafanikio ninayaona.
Pls pitia blog yangu:
LOGO DESIGNER

kazi nzuri rafiki, nmeipitia blog yako logos zako ziko poa. Tunahitaji vijana wengi kama nyinyi ili Tanzania yetu ikue. Inakua poa sana pale mtu napoweza kupata malipo muda wowote na sio kusubiri mshahara mwisho wa mwezi wenye makato kibao. Bila kubadilika tutazidi kulalamikia serikali. Wakati CHANGES NI SISI
 
Asante sana. Ubarikiwe.
 
Kwa swala la vyuo nimejarbu kujiunga mkuu but inasumbua natumia simu...
 
Back
Top Bottom