Vitu vinatukwamisha Taifa kusonga mbele, bali yakipungua mambo haya Tanzania ingekuwa tupo mbali mno

Vitu vinatukwamisha Taifa kusonga mbele, bali yakipungua mambo haya Tanzania ingekuwa tupo mbali mno

2.kutumia kiswahili shuleni
4.uchawa

Naunga mkono hoja

Kuna mamtu hayampendi chura kiziwi ila yanaendekeza uchawa ili yapate teuzi
 
Ukishaingiza matusi jua tayari umeshindwa kujadili kimantiki...

Ulipaswa ueleze ni kivipi Simba na Yanga zimekua kikwazo kwa maendeleo ya nchi...

Mpira ni moja kati ya sekta inayokuza uchumi kwa kasi sana...

Sasa badala tujifunze kufanya uwekezaji wa mpira wenye maslahi kiuchumi, mnatamani tuiuwe sekta hii..
Kama kuna sehemu nimetukana, naomba niwie radhi!

Lakini unaposema unaendeleza sekta, anayodumaza nguvu kazi ya Nchi, ina kuwa a grace in disguise.

Taifa letu bado linajitafuta, humani resource inahitajikq sana ku push up maendeleo, na sio watu kushinda vijiweni kujadili mpira.

Au nyie mnavaa miwani myeusi hamuoni yanayoendelea kwa watu hasa vijana??
 
Kuna watu wanabisha, sijui wao wanaishi wapi? wanakuja kulinganisha England na TZ.

Simba na Yanga ni Cancer dhidi ya maendeleo ya Nchi.
Taifa ambalo aaubuhi badala ya kusikiliza ya Dunia ni uchambuzi wa michezo😁😁
 
We unadhani kwanini chaguzi za Marekani huo mwezi wa nane mpaka wa kumi na moja tu; campaign ya uraisi inagharimu zaidi ya millioni 100 mpaka 200.

Unadhani kazi ya kupata attention ni nyepesi kama mnavyodhurura ndugu communication ni discipline inahitaji wataalamu wa mipango.

Huna mbinu za kukusanya attention unataka kulaumu washabiki wa mpira. Hii culture issue Tanzania; yaani mtu akishindwa kitu lazima atafute external factors za kulaumu.
Ivi unawezaje kufanya comparison ya Marekani na Tanzania!?

Nimeshindwa kuelewa dhumuni lako kabisa,
 
Taifa ambalo aaubuhi badala ya kusikiliza ya Dunia ni uchambuzi wa michezo😁😁
Yan mpaka huwa najiuliza, idara yatu ya Ujasusi katika auchumi imeamua kupotezea au ndio wameamua liwalo na liwe, acha liende mbele kwa mbele
 
Andiko lako, excludes role of the Gvt to the people

Andiko lako liko too theoretical kwa nchi za dunia ya tatu hasa Tanzania.

Kama maelezo yako yote hayajasema kazi ya gvt kwa watu wake basi kuna sehemu utakuwa aidha umepitiwa au umeamua tu kwa makusudi kutokusema.

Nimeonesha concern yangu kuhusu utekelezaji wa bajeti na vi paumbele vyetu, wewe unazungumzia theory of adoption to external environment, wakati huo huo stakeholder wa hiyo adoption ni watu wasiokuwa na uelewa au uwezeshwaji wa ku adopt in term of
1. Capital.
2. Health.
3. Education
4. Agriculture
5. Infrustucture.

Infact, maelezo yako yame base kwa nchi zilizoendelea zaidi ya miaka hata 200 iliyopita.

Inchi zinazo endelea zinahitaji watu wanaoweza kuhoji na kutoa mawazo endelevu ya yale yanayo tendeka ndani ya nchi
Kazi ya serikali ni kuweka mazingira ya kukuza biashara, kuwekeweza kwenye public and merit goods.

Mengine ni wewe sasa kuusoma mchezo unahitaji elimu ya aina gani to maximise your chances of employability in the future.

Shida moja ya elimu ya Tanzania ni kutokuwa na ofisi ya ‘career advice’ kuanzia form four kwenda juu ili wanafunzi waende picha halisi ya combo wanazotaka fanya A level, halikadhalika wanafunzi wa A’level kupewa picha halisi ya job market ya hizo shahada wanazotaka kufanya na employability chances.

We unakurupuka tu na shahada lako umechagua mwenyewe una kazi unataka kuilaumu serikali how come.

Unatakiwa ujipange.

Wafanya biashara sawa wanaweza lalamikia mambo kama kodi etc ambayo yana fanya mazingira yao kuwa challenging.

Iła wewe una mbinu za ushawishi tatizo Simba na Yanga; huo sasa utoto.
 
Taifa letu bado linajitafuta, humani resource inahitajikq sana ku push up maendeleo, na sio watu kushinda vijiweni kujadili mpira.
Mkuu ni wapi hapo watu wanashinda siku nzima wanajadili mpira na hawafanyi shughuli zingine...

Kijana wa bodaboda, muuza genge, muuza duka, mkulima akijadili Simba na Yanga uchumi wake unaathirika vipi?

Ninachokiona hapa ni wewe kutamani kila mtu afikiri unavyofikiri wewe.
 
Au nyie mnavaa miwani myeusi hamuoni yanayoendelea kwa watu hasa vijana??
Mimi sioni shida...

Kwasababu Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, watu hawajapenda michezo kwa kulazimishwa, wameshawishiwa..

Ukitaka wajadili siasa kila siku, washawishi.
 
Kazi ya serikali ni kuweka mazingira ya kukuza biashara, kuwekeweza kwenye public and merit goods.

Mengine ni wewe sasa kuusoma mchezo unahitaji elimu ya aina gani to maximise your chances of employability in the future.

Shida moja ya elimu ya Tanzania ni kutokuwa na ofisi ya ‘career advice’ kuanzia form four kwenda juu ili wanafunzi waende picha halisi ya combo wanazotaka fanya A level, halikadhalika wanafunzi wa A’level kupewa picha halisi ya job market ya hizo shahada wanazotaka kufanya na employability chances.

We unakurupuka tu na shahada lako umechagua mwenyewe una kazi unataka kuilaumu serikali how come.

Unatakiwa ujipange.

Wafanya biashara sawa wanaweza lalamikia mambo kama kodi etc ambayo yana fanya mazingira yao kuwa challenging.

Iła wewe una mbinu za ushawishi tatizo Simba na Yanga; huo sasa utoto.
Mayor, hapa umeelewaka vizuri, Hakuna namna unaweza kunexclude roles of gvt kwa watu wake.

Na umekiri kuwa bado kama nchi hatufanyi vizuri kwenye kutengeneza mazingira kwa maeneo niliyotaja kwenye moja ya post zangu hapo juu.

Simba na Yanga, ni tatizo katika uhalisia huu; watu hawafanyi kazi za kujiingizia kipato badala yake wanaishia kujadili mpira wa simba na yanga. au mpira kwa ujumla.

Na hili, kwa Dar ni almost kila sehemu, radio hasa FM radio takribani zoote mapeema asu buhi ni mpira.

Impact yake nini!?
1. Watu wanakuwa na mawazo ya mpira tu, hivyo kushindwa kubuni njia anuai za kujipatia kipato ( Psychological problem)

2. Watu kukosa moral ya kufanya kazi hasa timu yao inaapofanya vibaya ( Stress)

3. Kushindwa kujadili kuelewa sera, hatua na mchango wa wancanchi katika maendeleo ya taifa ( collective responsibility in dvl).

4. Nchi kukosa dira sahihi ya maendeleo, kwakuwa hakuna msukumo wa wanachi katika kutimiza malengo kusudiwa.
 
nakuunga mkono kwenye simba na yanga maana nimewahi kuwaambia wanangu kuwa hii simba na yanga ina wabrain wash wasahau kuhusu nchi yao walinipinga vibaya sana wengine kidogo tuzichape
Lakini hili la Simba na Yanga linatumika pale Kiongozi anapokuwa "dhaifu" na wengine wameongezea "wasanii"
 
Mayor, hapa umeelewaka vizuri, Hakuna namna unaweza kunexclude roles of gvt kwa watu wake.

Na umekiri kuwa bado kama nchi hatufanyi vizuri kwenye kutengeneza mazingira kwa maeneo niliyotaja kwenye moja ya post zangu hapo juu.

Simba na Yanga, ni tatizo katika uhalisia huu; watu hawafanyi kazi za kujiingizia kipato badala yake wanaishia kujadili mpira wa simba na yanga. au mpira kwa ujumla.

Na hili, kwa Dar ni almost kila sehemu, radio hasa FM radio takribani zoote mapeema asu buhi ni mpira.

Impact yake nini!?
1. Watu wanakuwa na mawazo ya mpira tu, hivyo kushindwa kubuni njia anuai za kujipatia kipato ( Psychological problem)

2. Watu kukosa moral ya kufanya kazi hasa timu yao inaapofanya vibaya ( Stress)

3. Kushindwa kujadili kuelewa sera, hatua na mchango wa wancanchi katika maendeleo ya taifa ( collective responsibility in dvl).

4. Nchi kukosa dira sahihi ya maendeleo, kwakuwa hakuna msukumo wa wanachi katika kutimiza malengo kusudiwa.
Good Morning
 
Watu wanajadili simba na yanga asubuhi hadi jioni, hawana agenda ya maendeleo au muelekeo wa taifa lao.

Unategemea nini nchi kama hiyo! wananchi hawana mawazo mbadala ya maendeleo!
Swali ni Moja nani aliekuambia anataka maendeleo unayoyaongelea kati ya hao wanaojadili simba na yanga
 
Swali ni Moja nani aliekuambia anataka maendeleo unayoyaongelea kati ya hao wanaojadili simba na yanga
Hufahamu maana ya collective responsibilty!?

Wao wakiugua matibabu watayapata wapi!? na huko watakapoyapata public health facilities zimepatikanaje?

Maswali ni mengi ambayo utaishia kujibu kirahisi tu kuwa, " wao wamekuambia wanataka matibabu kwenye public health facilitie"

Ndio mana makusanyo ya kodi ni kidogo, kwakuwa sekta za uzalishaji ni chache, watu hawafanyi kazi, hali inayopelekea umaskini uliyo kithiri
 
Sasa tatizo la mashabiki wa simba na yanga hapo lipo wapi maana naona kama umechanganyikiwa
 
Wewe ni rema?

Hapa nakataa, maana kuna mataifa kama Misri na England wanapenda mpira kuliko sisi na wako vizuri kiuchumi...

Tusitumie akili ndogo kujadili failure zetu, tutaendelea kuanguka...

Simba na Yanga imezuia vipi nchi kusonga mbele?
Uingereza hawazungumzii Man U, Liverpool, Newcastle, Aston Villa tangu asubuhi mpaka jioni.
Nimeishi huko.
 
1. YANGA NA SIMBA - Ni burudani iliyogeuka kuwa sumu, inapewa umakini mkubwa sana kuzidi mambo ya kitaifa, ndio maana ligi ikisimama huwa ni ngumu kuzima skendo nzito,

2. Kutumia kiswahili shuleni - Kama taifa tumeshaambulia aibu kibao kuanzia kwa Mawaziri, Marais, wakalimani, n.k. wenye PHD zao, wanapata ugumu Kuelewa, kujieleza, kuchangia mawazo, n.k. English ni lugha ya kimataifa ni lazima watoto wafundishwa kuanzia shule ya msingi tena ikibidi waletwe wakenya maana english medium kibao waalim wa kiingereza lugha inawapa shida wanajua kufundishia ubaoni pekee, Hali hii imefanya watanzania wengi kuogopa kutoka nje ya nchi, Wakenya na wahindi wanapiga pesa ndefu kwenye biashara za kimataifa kwa maloghafi za Tanzania, n.k.

3. Ulafi- mfano mdogo tu Tanzania ni nchi yenye pato dogo kitaifa, wananchi wanajikamua kulipa kodi lets say imefika bilioni 1, serikali inanunua magari matatu vx michuma ya kisasa, Bajeti hio inaweza kununua Hilux 20 mpya imara ila ukitoa hayo mawazo wanakimbilia Kujitetea kwamba "Mnataka tutembelee baiskeli ?" Barabara zetu sehemu nyingi ni moja inatumika na magari yote, ajabu ni kwamba kiongozi anataka attention kwa kusimamisha magari yote lisaa zima ili aonekane, ni ubinafsi !!

4. Uchawa

Soma Pia: Ningekuwa Rais ningefanya mambo haya muhimu zaidi
Uachage masiraha wakati wa kujadili hatma ya taifa letu.
 
Huelewi unachojadili, kaa kimya!
Jinga kweli wewe mambo ya ushabiki wa mpira na mambo ya maendeleo yanaingilianaje hujielewi mbona ni vitu viwili tofauti tafuta hela jinga kabisa wewe maisha Yako magumu unaanza kuingilia hobby za watu ambao wanaishi maisha yao
 
kufeli mmefeli wenyewe msisingizie simba na yanga, Tanzania mpira ndio unakuwa hivi mmeshaona nchi za wengine huko wanavyofatilia timu zao kindakindaki na maendeleo yapo mbali tu..!

Ni ufitini,ujinga na uzandiki kufikiri Kiswahili kinaturudisha nyuma!,kenya wanakitumia Kiswahili na wanapiga pesa kupitia Kiswahili hichohicho!. nchi ngapi hapa africa wanaongea English lkn tuponao kwenye ombwe moja la uchumi!.. china wanatumia lugha yao lkn wanachuana maendeleo na nchi nyengine kubwakubwa na nchi nyingi za asia miaka ya 60's tulikuwa tunalingana nao uchumi lkn leo wapo mbali mno na wanatumia lugha zao!.

shida inaanzia ubongoni maana hata kuainisha tu mambo yanayotusumbua umeshindwa!,hata uongee English kushinda hata wa British wenyewe kama hauna uwajibikaji,u serious,mipango,dira ya nchi,usimamizi mzuri utakwama tu!..
michezo haijanza tz nchi nyengine wanamichezo na timu kubwakubwa zenye wafuatiliaji wanaojitoa kabisa na maendeleo wanayo.. mkuu kaa chini ufikiri vyema hizo sio sababu tuacheni uvivu na imani za kijinga ndio maana watu wanapigwa pesa na wakina nabii huko.
 
Back
Top Bottom