Vitu vizuri havihitaji Watu wanaopenda utulivu wa bwerere. Kama hupendi changamoto basi vitu vizuri sio halali yako

Vitu vizuri havihitaji Watu wanaopenda utulivu wa bwerere. Kama hupendi changamoto basi vitu vizuri sio halali yako

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Moja ya dalili kuwa maisha yako yatakuwa ya chini ni kupenda bwerere. Kupenda utulivu wa bwerere.

Hakunaga vizuri kwenye bwerere. Yaani kamserereko.
Bwerere haitakuimarisha. Bwérere itakufanya uwe na akili mgando. Kupenda vitu visivyokupa changamoto.

Hata hivyo kwenye maisha. Vitu Bwerere havikufanyi ujivunie na upewe heshima.
Úkiwa wale Watu wasiopenda hekaheka, ving'ang'anizi na hustlers Basi usimlaumi yeyote.

Ukiona kazi unayofanya inakupa utulivu ujue kazi hiyo haina pesa. Haitakufikisha popote.
Unataka raha? Unataka utulivu? Alafu muda huohuo unataka vitu vizuri. Kuna vitu huvielewi.

Vitu vizuri havikupi utulivu. Lazima uhangaike, uhenyeke haswa ili ukomae.

Unataka familia yako íwe imara alafu muda huohuo hautaki mke au mume mzuri. Unaumwa kweli.
Ukiona familia ipo imara ujue Baba na Mama ni wazuri.

Uzuri kimwili, kiakili, kihisia na kiroho.

Na mtu akishakuwa mzuri lazima msumbuane pale mambo yakiwa hayapo sawa.

Elewa jambo moja vitu vizuri huwakataa Watu wasiostahili. Vitu vizuri hubagua. Vitu vizuri hudharau. Vitu vizuri huwa na maamuzi magumu kulinda uzuri na heshima yao.

Vitu vizuri havitaki kumilikiwa na Watu waoga. Watu wasio jasiri. Watu wasiojiamini.

Mtu asiyejiamini na mwoga ni rahisi kukata tamaa. Mtu asiyejiamini hawezi kuwa mwanafunzi mzuri kwaajili ya kujifunza mambo mapya. Akili yake huwa imepooza. Yeye kila kitu huona ni kigumu. Na vitu vizuri karibu vyote ni vigumu kuvipata.

Kuanzia uhai. Wamama wanapojifungua wanaweza kukwambia moto unaowawakia. Kupata mtoto ni jambo zuri lakini lazima upigane kufa kupona. Ukileta mchezo ni aidha Mama afe au mtoto au wote wawili.
Kulea mtoto awe mtoto mzuri haina tofauti kubwa na kuzaa. Lazima wazazi wapambane kufa na kupona. Lazima wa-fight na sio kutaka utulivu au kuhitaji mtu mwingine afanye badala yao.

Ni lazima watoto wetu wafundishwe kuwa, vitu vizuri huja kwa gharama ya kujitoa, jasho na damu, haviji bwerere, havitampa utulivu mtu yeyote mzembe. Lazima kupambana.

Unahitaji maisha mazuri basi kubali kabisa kuwa utulivu sio sehemu yako kwa muda unaohangaika kuyatafuta hayo maisha mazuri.

Ushindi mnono huhitaji pambano kali takatifu.

Vitu vizuri huwaponyoka wale wasioweza kuvilinda. Elewa ulinzi na usalama sio Bwerere waulize Wanausalama wàtakuambia. Muda wote lazima uwe macho.

Ñawatakia Sabato Njema.
Acha nipumzike sasa.

Robért Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom