Vitu vya kuepuka kufanya ukiwa unaendesha gari ya Automatic

Vitu vya kuepuka kufanya ukiwa unaendesha gari ya Automatic

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2018
Posts
358
Reaction score
675
1. Kushuka kwenye mteremko gari ikiwa neutral, hii inasababisha kuzuia oil kusambaa na kusababisha msuguano kukosa kilainishi hicho na kupelekea kusagika kwa baadhi ya sehemu.

2. Kukanyaga mafuta kabla ya kubadilisha gear. Hii ni hasa kwa vijana unawasha gari na kuanza kupiga resi, kitendo hicho husababisha msuguano mkali na unaweza kuharibu sehemu za engine.

3. Kubadilisha gear wakati gari bado inatembea, hakikisha unakamata brake kwanza ndipo ubadilishe gear.

4. Kuweka neutral kweye taa nyekundu kwenye taa za barabarani, watu wengi hufanya hivyo ili kusave mafuta lakini kiasi unachosave ni kidogo sana kulinganisha na gharama ya tatizo unaloweza tengeneza, tumia brake ili gari liendelee kuwa kwenye drive mode, madhara hutokea unapoweka na kutoa neutral.

5. Kuweka parking kabla gari halijasimama kabisa. Hakikisha gari limesimama kabisa ndipo unaweka parking.

6. Kuendesha gari kwa speed ya juu kabla ya engine kupata joto, hasa kipindi cha baridi hakikisha engine imepata joto ili kuwezesha oil kusambaa kwenye sehemu zote.

7. Kuacha mafuta yakiwa machache katika tank, tank la mafuta linatakiwa kuwa full au kuwa nusu lakini sio chini kabisa. kuwa full kunasaidia engine na sehemu nyingine kuwa cool.

Imetolewa na Kimomwe Motors (T) Ltd, waagizaji wa magari. 0746267740

1573828512347.png
 
Nina maswali mawili:
1.Neutral gear inatakiwa kutumika wakati gani?
2.Madhara ya kuacha gari ikatembea na Petroli chini ya nusu tank au ikiwa tayari taa ya mafuta imewaka, tukiacha hilo ulilosema kuwa inasababisha engine kutokupoa vizuri? Ninauliza hivyo kwakuwa nimeshashuhudia Taxi au Daladala nyingi zikifanya hivyo vitu na sikuona madhara kwa hayo magari yao.
 
Kwenye neutral gear hapo pana mashaka sana, leta technical details za tatizo la kutumia neutral gear kwenye taa nyekundu, kwani wataalamu wanashauri kuweka neutral ili kupunguza friction ya gearbox, na itapunguza heat hivyo itadumu kwa muda mrefu, kuliko kusimama muda mrefu ukiwa kwenye drive mode afu umezuia kwa brakes tu.

Kimsingi namba 1 mpaka 4 nina mashaka nazo, elezea in details asee
 
Naunga mkono

Ila kuna wabishi kudadeki hata nusu saa hatoi mguu kwenye brake, kasimamia breki muda wote kwenye foleni. Na wanaofanya hivi ni madereva wa serikali, STL, SU unakuta V8 muda wote taa za breki zinawaka tu, nabaki najiuliza huyu hachoki kuweka kati huo mguu
 
Ila kuna wabishi kudadeki hata nusu saa hatoi mguu kwenye brake,kasimamia breki muda wote kwenye foleni. Na wanaofanya hivi ni madereva wa serikali, STL, SUunakuta V8 muda wote taa za breki zinawaka tu, nabaki najiuliza huyu hachoki kuweka kati huo mguu
Kuna gear sijawahi zitumia toka nijue kuendesha gari, Neutral, 2 na L. Mimi ni mguu kwenye break hata masaa matatu fresh tu.
 
Back
Top Bottom