Wakuu mtanisamehe nimechelewa kuja kwa wakati.
Vitu vya muhimu kuanza navyo ni kama;engine oil Total 1&5 litre petrol na diesel,engine oil General/Petrogen 1&5 litre nazo petrol na diesel,engine oil Oryx 1, 4&5lita, hydraulic Lubex 1&½litre, hydraulic ya general lita1 na ½ pia uchanganye na hydraulic za kawaida hizi ni za nje kama Rapide, Black Bulls etc pia hizo oil hapo juu unaweza kuchanganya na za nje ambazo bei zake ni rahisi kidogo kutokana na siyo kila mteja anaweza kutumia oil ya gharama {ukifika kwa wauzaji watakuelekeza zaidi ipi ni ipi}, brake fluid ujazo wa ½litre na ¼lita ziwe dot3 na hii kuipata imekuwa changamoto coz sirikali imeipiga marufuku inataka gari zitumie dot4 but mafundi wanayakataa wanasema yanakata rubber za brake japo nimeshafanya uchunguzi dot4 na 3 hayana tofauti yoyote, radiator coolant kuna za kibongo na za nje weka zote.
Pia, kuna oil za dumu {engine oil} 20 litre za bei rahisi hizi zinapimwa kwenye kopo za lita moja moja wanazinunua sana bodaboda na daladala.
Grease; General ndiyo hasa imezoeleka mikoani,kuna vitu kama motor flush, oil treatment, diesel&petrol treatment, gasket maker kubwa na ndogo, Epoxy quick, Araldite super glue ni vitu kila siku mafundi wanavitumia.
Oil filters; Toyota,OSK,Nissan na Teson No1 hizi ni kwa ajili ya gari zote ndogo ,oil filter same na hapo juu No2 hizi ni za gari kama MarkII na gari nyinginezo, uzuri hizi zinaingia kwenye gari zote anayefanya service akatoa ya Toyota anaweza akaweka ya Teson au OSK ikapiga mzigo fresh na zote zinafanana tofauti ni ubora hata bei kununua na kuuza zinatofautiana, changanya na za Hiace, Coaster bus Mitsubishi Canter maana ni gari zipo kila sehemu hizi unaweka chache chache tu.
Brake pads; hizi chukua za Kichina ukichukua packing ya Toyota zitakusumbua siku hizi wanaofunga original kwenye gari zao ni wachache hizo utaziweka ukishakuwa mzoefu au kwa order maalum,pads chukua gari ulizoorodhesha hapo juu uwezo ukiwepo chukua za gari zote.
Brake shoes, chukua za gari kama nilivyo-mention hapo chini [emoji1484]
Chassis parts; chukua stabilizer link mf:IST hizi hizi zinafunga kwenye gari 4 yaani Vitz na Raum new na Platz, RAV4, Corolla&Carina Spacio New {hizi za Spacio New zinafunga gari zaidi ya 5 inlc OPA,Corolla ya Police, Noah Voxy, Premio New na Allion}, MarkII etc.
CV Joint;TO4 Corolla&Carina,TO9Corona&RAV4 old model,TO35 IST,Vitz&Funcargo,TO54 Corolla new,Spacio new, OPA.
Fuel pump za ndani ya tank,hizi chukua packing ya Toyota,Denso na za Kichina{also hizo za Toyota ni mchina kazitoa copy ila zinakuwa bora kidogo usije ukaagiza pump kwa dealer wa Toyota ukafikiri utaweza kumuuzia mtu huko}wachache sana wanazinunua 100 kwa mmoja,pia spark plugs Denso na NGK hizi weka za sindano {Iridium} na za kawaida hizi za kawaida kuna fake na original changanya zote.
Tie rod end; hasa za Corolla, Carina na za Hiace hizo za Corolla zinaingiliana na Noah old model. hizi ukichukua za IST utapiga nazo picha ngumu sana hazifi unless una mtaji mkubwa wakuweka hela chini.
Rack end;{Corolla&Noah}, Carina, Hiace.
Ball joints; Carina, Corolla, Corona,IST&Vitz,Noah juu na chini, Hiace juu na chini, RAV4 old, MarkII GX90, 100,110.
Bearings; za miguu (Hub) IST, Corolla, RAV4, Noah old, ukiweza ongeza na mashine ya ku-press bush na bearing,compressor ya kujaza upepo na kusafishia air cleaner filters, car accessories kama carpet za chini, dushboard polish, air freshener, wiper blades, bulbs mchanganyiko, fire extinguisher 1Kg na triangle {hizi ni kwa gari ndogo}.
Ukiwa na uwezo ongeza battery Ns40/N40 na N50,hapa kwenye betr hata kama una uwezo sishauri sana kwa sasa subiri kama miezi sita au zaidi baada ya kufungua duka ndo uweke utakapokuwa umezoeleka,ila weka battery terminal kwa kuanzia.
Vitu ni vingi sana hapa nimejaribu kuandika vichache ila nashauri mtafute fundi aliye mitaa unakotaka kufungua biashara yako mfanye rafiki yako akuelekeze kwa ukaribu hapo mtaani/mjini ninini hasa kinachotoka kwa speed/kipi hakitoki kwa speed ili ktk manunuzi yako uzingatie kuchukua wingi au uchache wa kitu husika.
NB: Nasisitiza kuwa karibu na mafundi kutokana na wao kila siku wanacheza na vitu hivi na wanajua zaidi vitu wanavyovitumia mara kwa mara pia inawezekana nilivyoshauri hapa huko vikawa siyo dili sana wao ndo watakaokupa dira nzuri kuliko mimi,pia utajitahidi kujua bei wanazouza wenzako walio jirani na wewe ili umjue adui unayepambana naye anasimama vipi,hili litafanikiwa kwa kumkamata kijana muuzaji yeyote wa duka hapo mtaani unampa hela ya soda akupe bei ya vitu hivi au atakavyokushauri fundi wako ili siku ukishusha mzigo ujue jinsi ya ku-balance bei iwe chini kidogo ya wenzako ili ujenge jina.
Mungu akuongoze ndugu.