Vitu vya kuzingatia wakati wa kuanzisha biashara ya spea za magari madogo

Mkuu hapo kwenye chasis parts kama vile tie rod end,rack end,Ball joints,cv joints,stablizer link unashauri kuchukua new(za kichina) au original(used)?
Nashauri uchukue vipya vya Kichina maana sokoni nako sasa ivi zimeingia akili mpya,siyo rahisi kumuuzia kijana msomi kitu mfano CV joint ikiwa na magris grease ishara wazi kwamba ilitumika ilikotoka akakubali kukupa pesa yake ila ikiwa kwenye boksi ni rahisi sana kumshawishi.

Used uza kwa order maalum tu pale mteja atakapohitaji,vitu used usivipe sana kipaumbele maana ni ngumu kusema ni vizima 100%.
 
Naomba kufahamu mitaa ambayo wanauza spare za magari kariakoo kwa bei ya jumla ahsante hapa namaanisha spare zote kuanzia accessories, battery's, spare parts, lubricants and tyres ahsante sana kama nitapata ushirikiano mzuri

Naomba kufahamu mitaa ambayo wanauza spare za magari kariakoo kwa bei ya jumla ahsante hapa namaanisha spare zote kuanzia accessories, battery's, spare parts, lubricants and tyres ahsante sana kama nitapata ushirikiano mzuri

Spare parts&Lubricants;Kariakoo anzia mitaa ya Msimbazi na Swahili,mtaa wa Mafia maduka pia yapo na mtaa wa Nyamwezi,ila mtaa wa Msimbazi ukiwa unatokea traffic lights za Morogoro road ukiwa unaelekea Gerezani kule maduka ni ya retail usiingie watakuumiza.

Car accessories;mtaa wa Lumumba ndo mahali pake hutokosa kitu,Lumumba yote kuanzia pale CRDB Vijana branch kuelekea barabara ya Uhuru {Arnaoutoglou} mule kote kumejaa maduka ya urembo wa magari.

Batteries & Tires/tubes;Mtaa wa Livingston ndipo zinakouzwa kwa bei rahisi,ila mtaa wa Lumumba pia Bin Slum wapo kule unaweza kuwatembelea japo bei zao siyo rafiki sana kwa mjasiriamali wa kileo.
 

Asante sana mkuu,Mungu akubariki sana kwa maarifa haya.

Ila nimecheka sana hapo uliposema sokoni nako zimeingia akili mpya maana umenigusa hapo hahah.
 
Ahsante boss kwa mrejesho mzuri ubarikiwe sana
 
Mkuu hapa umemaliza kila kitu.
Ubarikiwe kwa mchango wako huu wengi tutanufaika.
Je kwa kawaida mtaji wa kuanzia unatakiwa uwe milioni ngapi mkuu ili na sisi wengine tujue tunajipangaje?
 
Mkuu hapa umemaliza kila kitu.
Ubarikiwe kwa mchango wako huu wengi tutanufaika.
Je kwa kawaida mtaji wa kuanzia unatakiwa uwe milioni ngapi mkuu ili na sisi wengine tujue tunajipangaje?
Bro post #7 nililifafanua hili pitia ujitathimi.
 
Mkuu kwa vyote alivoandika hapa mtaji wake ni kama kiasi gani? Na duka la spea lililokamilika kabisa mtaji wake unaweza kuwa kiasi gani?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, nakuombea pepo kabisa aisee.. nina ndoto nyingi sana yaani, mojawapo ni hili duka la spea.. acha niusave huu uzi, naamini Kuna siku utakuja kunisaidia sana.. barikiwa mkuu.
 
Mkuu kwa vyote alivoandika hapa mtaji wake ni kama kiasi gani? Na duka la spea lililokamilika kabisa mtaji wake unaweza kuwa kiasi gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakumbuka kuna post nililijibu hili huko juu,tulisema at least mill15 unaweza ukaanza nayo but hata 10mill inawezekana japo inakuwa ktk hali ya ugumu kiasi ila muhimu ukituliza akili unatoka.

Kwa kiwango hicho unaweza kuwa na kila item niliyoandika hapo juu japo kitu kimoja kimoja au viwili viwili ambapo ndo wengi tusiokuwa na mitaji mikubwa tulivyoanza/tunavyoanza biashara.
 
Sawa mkuu, acha tujipange tu na wakati ukifika tutafanya.. umekua msaada mkubwa sana, na hizi ID ipo siku tutaziweka kando na tutafanya vitu vingi tu mkuu.. barikiwa
 
Wakuu huu uzi umesimama Sana.. Tunashukuru kwa maelezo yakujitosheleza.

Naomba mlielekeze namna ya kuusave huu uzi maana ntauwitaji Sana
 
Nimejifunza kitu Hapa.
 
Hongera sana sana mkuu yani umeniongezea madini vibaya sana umenisaidia sana hapo kwenye muingiliano mimi nimefungua auto spare nina miezi mitatu nalo bado vitu vilikuwa vinanipiga chenga
 
Hongera sana sana mkuu yani umeniongezea madini vibaya sana umenisaidia sana hapo kwenye muingiliano mimi nimefungua auto spare nina miezi mitatu nalo bado vitu vilikuwa vinanipiga chenga

Vipi biashara inaendaje mkuu?

Tupe experience yako kidogo boss.
 
Naomba mawasiliano yako mkuu
 
kitu kikubwa ni kuangalia ni aina gani ya magari yanatawala mfano TOYOTA,BMW,NISSAN AU MENGINEYOO ukijua hili ni vyepesi kujua unanunua spear za magari gan kwa wingi coz unauhakika wa kutokaaaaaa
 
Niongezee kidogo hapo kwa Sir_Mimi, kama mtaji wako ni mdogo nashauri kuanza na Lubes alizozitaja sir_mimi changanya na filters na vitu vingine vidogo vidogo mathalani Plugs, Fuel pumps na vifaa vingine vya service... Hapa utakimbiza mdogo mdogo huku ukikuza mtaji.

Hapo unaweza anza ata na 4M, ila hakikisha hukai sehemu ya peke yako, tafuta eneo lenye maduka ya spare utauza baadhu ya spares at kwa kupiga winga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…