LOVINTAH GYM
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 459
- 653
ACCOUNTING CONCEPTS
Hizi ni sheria ambazo hutumika katika kutengeneza ripoti za kiuhasibu na kutunza mahesabu ya kibiashara.
Kila kitu kina imani yake, hizi concepts ni kama imani zinazoongoza taratibu za kiuhasibu.
1. GOING ON CONCEPT.
Hapa ni kuamini kuwa biashara unayoianzisha haitakuja kufeli, yani hio biashara itaendelea vizazi kwa vizazi.
Ni vizuri kuamini hivi kwasababu, ili kufanya wawekezaji waweze kuwekeza katika biashara yako, wanokukopesha pia wataweza kukukopesha bila hofu kuwa utafunga biashara yako mda wowote.
2. BUSINESS ENTITY.
Biashara na mwenyebiashara ni vitu viwili tofauti.
Usieende kumdai mtu nyumbani kwa bidhaa zilizokopeshwa kwaajili ya biashara, au kwenda kuchukua vitu vya nyumbani kwake kwaajili ya pesa zilizokopwa na biashara.
3. MONEY MEASUREMENT CONCEPT.
Kila kitu kinatakiwa kurekodiwa kwa kutumiwa pesa na si vinginevyo, Hata kama ulipewa zawadi ya cherehani iwe asset yako wakati wa kuanzisha biashara basi lazima ujue ile cherehani ina thamani ya kiasi gani na urekodi kiasi cha pesa ambayo ungetumia kununua ile cherehani.
Ndio maana hata huduma kama za hospitali, bado tuna convert kutumia pesa. Japo huenda ile huduma ingeweza kuwa na gharama kubwa zaidi au ndogo zaidi.
4. DUAL ASPECT CONCEPT.
Kila kitu kina credit na debit entry yake hii lengo ni kusaidia mahesabu yaweze kuwa sahihi zaidi.
Mfano:
Biashara imenunua machine ya shillion 200,000
inamaana kwenye cash account yako umetoa shillingi 200,000 ambayo hio tarekodiwa upande wa credit wa cash, ambao ndio upande wa kutoa.
Ila tutakuwa tumepata machine kwa shillingi laki mbili, ina maana tutarekodi shillingi 200,000 upande wa debit wa machine account.
5.COST CONCEPT.
Mali za biashara zinatakiwa zirekodiwe kwa ile ile pesa iliyonunuliwa na si vinginevyo, inamaana haitoongezeka thamani kutokana na kuongezeka kwa bei au kupungua thamani kutokana na kupungua kwa bei.
Mfano:
Ulinunua nyumba kwaajili ya biashara kwa gharama za shillingi million 50 , basi hata thamani za nyumba katika eneo hilo zikipanda wewe itabaki ile ile, na kumbuka lazima utoe gharama za uchakavu (depreciation amount).
6. REALIZATION CONCEPT.
Hutakiwi kuiweka kwenye mapato yako pesa ambayo kazi yake hujaimaliza.
Mfano:
Fundi cherehani kalipwa shilliong 20,000 na mteja kwaajili ya kushonea nguo yake.
Fundi cherehani atakiwi kuiweka kama mapato hio 20,000 kwasababu bado hajamaliza kutengeneza hio nguo na kumpa mteja wake. Kwahiyo itahesabika kama deni la biashara (liability).
Itahesabika kama mapato (revenue) pale tu mteja atakapoichukua na kuondoka nayo.
Mfano 2:
Mteja kalipia gym membership fees ya mwaka mzima kiasi cha shillingi 1,000,000
Inamaana hutakiwi kuihesabia kama mapata million 1 yote, mpaka mwaka utakapoisha na yeye kumaliza kuitumia ndio utaihesabia kama mapato.
7. MATCHING CONCEPT.
Kwa kila mapato yanayopatikana kwenye biashara basi kuna gharama pia zimetumika na zinatakiwa kuonekana kwa pamoja.
Mfano:
Unauza ticket za ndege na kwenye kila ticket utakayouza ualipwa shillingi elfu 10, ukafanikiwa kuuza ticket 10 katika mwezi December, ina maana kwa mwezi huo una commission ya shillingi 100,000
Malipo yake utalipwa mwanzoni wa mwezi January mwaka unaofuata.
Ila kwa muhasibu anatakiwa a rekodi mapato uliyoongeza katika kampuni ya zile ticket 10, pia anatakiwa arekodi commission ambayo utalipwa kiasi cha 100,000 na itabidi zirekodiwe mwezi December na sio January.
Hufanyika hivi ili kurahisisha wawekezaji kuelewa kuwa kwa kipato hiki basi kuna gharama kiasi flani ilitumika.
8. ACCRUAL CONCEPT.
Kwenye biashara unatakiwa kurekodi shughuli inapofanyika sio kurekodi siku ambayo utalipwa kwaajili ya io shughuli.
Mfano:
Umeuza bidhaa kwa mkopo za shillingi 5,000
Basi ni lazima urekodi kuwa umefanya mauzo ya shillingi 5,000 kwa mkopo na sio kukaa ksubiri mpaka ulipwe ndio uanze kurekodi.
Hii inasaidia account za biashara kuwa zinaeleweka kiurahisi.
Mfano 2:
Bado hujalipa kodi ya sehemu ya biashara kiasi cha shillingi 300,000
Ina maana unatakiwa urekodi kuwa kodi ya mwezi huu ni shillingi 300,000 ila bado nadaiwa kwenye accrual expenses ambayo ni liability.
9. PERIODICITY CONCEPT.
Ripoti zote za biashara zinatakiwa ziwasilishwe kwa wawekezaji kwa siku ile ile ambayo ziliwasilishwa mwaka jana, hii inasaidia kufananisha na kujua maendeleo ya biashara kiurahisi.
Zipo ripoti ambazo hutengenezwa baada ya mwezi, au miezi 3 au miezi 6 hizo zinakuwa ni kwaajili ya matumizi ya ndani ya office.
#accountingconcepts #biashara #uhasibu #swahili