KIUNGOMCHEZESHAJI
Senior Member
- Oct 4, 2013
- 120
- 255
Adolescence stage ni kipindi kati ya miaka around 16 hadi 22 hivi. Ni umri wa kubalehe kwa mwanaume na kuvunja ungo kwa msichana. Kisayansi unaitwa foolish age kwa sababu kijana ndo anaachana na utoto lakini hajaufikia utu uzima vile. Yupo hapo in between. Kijana anakuwa hajitambui vizuri. Mvulana anaanza kuongea besi la ajabu ajabu, msichana ndo anakuwa na sauti nnyororo na ngozi laini, hapo ndo vijogoo vinaanza kufukuzia. Mara nyingi ndo umri ambao vijana wengi hufanya majaribio masuala ya mapenzi. Nii umri ambao kijana asipopata maelekezo, malezi na ushauri mzuri kuhusu maisha basi ni rahisi kupoteza dira na mwelekeo wa maisha yake ya baadaye. Mimi kuna vituko nikikumbuka mpaka leo nacheka sana. Kweli wazungu hawakukosea kuita foolish age.
Mimi enzi hizo nilikuwa mpole sana. Nilikuwa mwoga sana kutaniana na binti (nilikuwa domo zege ile mbaya). Ila kinyume chake nilikuwa mtu wa dini sana, kanisani kwa sana mpaka wakanipa jina la utani Mchungaji. Nilikuwa nasoma sana biblia na vitabu mbalimbali vya dini. Basi Mchungaji na viongozi wa dini walinikubali mpaka wakawa wananipa nafasi kutoa masomo mbali mbali. kusema ukweli kimaumbile nilikuwa handsome (hata leo) mwenyewe najikubali, mweupe kiasi, mrefu, si mnene wala si mwembamba, umbile la wastani. Basi wasichana wakawa wananisumbua sana ila kila anayejaribu akawa anaambulia patupu.
VITUKO AMBAVYO SITASAHAU
Moja, Nikiwa nasoma O-level, kuna binti alikuwa ananisumbua sana, ana makeke ile mbaya. Anaitwa Veronica. Siku moja nilitoroka shule kabla ya muda. Ilikuwa shule ya kutwa. Njiani nikamkuta huyo binti na yeye katoroka. Tukapiga story za hapa na pale, basi tulipofika mahali pa kuachana, mimi nimefika geto, nikamuaga. Akasema nimsubiri ana kiu apite kwangu gheto nimsaidie maji ya kunywa nikasema poa, tulivyofika nikampa maji. Alipomaliza akakaa kitandani, akavua viatu akawa anasingizia joto akaanza kufungua vifungo vya shati. Nikajifanya sioni nikageuka upande mwingine kama natafuta kitu kwenye vyombo. Akaniomba apumzike kidogo kitandani, nikasema poa lakini mi naenda kuchota maji sijui nitakukuta? Hapo najichukulia ndoo natoka. Alipoona niko serious basi akaondoka. Siku nyingine alinitukana live akaniambia mashine yangu haifanyi kazi au sina kabisa.
Tukio la pili:
Nikiwa nasoma Advance, nilikuwa na misimamo yangu hiyo hiyo: nikiwa shule bro alihamishwa kikazi, basi likizo ikabidi nimfuate,. Nilipofika jinsi nilivyo serious na kazi na shule basi mabinti wakaanza fujo zao nagomaniwa kama mpira wa kona. Walipoona siwashobokei basi wakabuni njia mpya, msichana akiwa na wenzake anawaambia kuwa KIUNGOMCHEZESHAJI ni mchumba wake. Hii ilikuwa namna ya kuwakatisha wenzake tamaa. Wakati mimi sijui hili wala lile, siku moja wakaenda kuokota kuni porini wakakutana watatu wakapigana kwa ajili yangu kila mmoja anadai mimi ni wake. Daah, kesi ikaja mtaani ilikuwa soo, bro alikuwa amesafiri kwenda Marekani shemeji ndo kabaki home, palikuwa hapatoshi. Najitetea kwa shemeji wala hanielewi. Nikawafuata wasichana wote kwa wazazi wao kuwa kuna jambo la muhimu shemeji yangu anawahitaji. Wakaja, kumbe shemeji alikuwa hajui lolote, akashtuka tu watu wamekuja nyumbani nikawakalisha, ilikuwa kesi mbaya siku hiyo mwishoni wote wakakiri kuwa walijisemea tuu. Ndo ilikuwa pona yangu siku hiyo, na Mtaani nikawa gumzo. shemeji alikuwa ameshaamua kuwa wanasitisha kunisomesha.
Tatu, na la mwisho:
Bro akahamishwa tena kikazi, na tulipofikia ikabidi apangishiwe nyumba na mwajiri. Nyumba ya Mwenye nyumba na aliyotupangishia vikawa vinapakana. Wakati huo ndo nimemaliza form six najiandaa kwenda chuo. Mwenye nyumba alikuwa ana binti yake anasoma secondari. Akaja kuniomba nimfundishe binti yake tuition ya Geography na History. Nikakubali. Siku mbili za kwanza Mzee naye alikuwepo darasani ili kujiridhisha kama niko fiti, na kweli nilikuwa vizuri akaniappreciate. Siku zilizofuata akawa ananiacha tuu niendelee na binti yake. Siku moja natoka zangu town naendesha baiskeli nikamkuta binti njiani, nikampakia tunarudi zetu home. Nilipofika kuna kisehemu kina vichaka kidogo, binti akanitekenya, daah nusura niangushe baiskeli. Akaniambia kumbe wee mwanaume una nyege. Daah nilijisikia kuweweseka aisee. Tukaendelea mbele kidogo akasema nisimame ameangusha kitu. Nikasimama, akashuka akapandisha sketi ili nione mapaja, nikamwambia iko siku utakipata cha moto.
Siku nyingine, bro na shem wote hawapo. Yeye mzee na mama wote hawapo akaniita nimfundishe tuition. Nikaenda niko serious. Nilipoanza mara akanikatisha hajaelewa point vizuri. Akasimama akaja akanishika shati, akanikumbatia kwa nguvu, topic ikabadilishwa, kama ni ndege basi gia ilibadilishiwa angani. Katikati ya mechi mara ikasikika sauti ya pikipiki, uuuuwi, kumbe baba yake anarudi. Yule binti alikuwa na akili ya fasta, aliniamrisha nitokee mlango wa uani, na kwa nje kuna baiskeli yao kwenye fensi akaniamrisha niende nayo. Akachukua materias yangu akayaficha. Kilichoniokoa ile nyumba ilikuwa na eneo kubwa na imezungukwa fensi ya michongoma, kwa hiyo nikazunguka na kupotelea upande wa pili. Baadaye nikawa narudi kana kwamba natoka mjini. Nikafika kwao nikabisha hodi nikamkuta mzee nikamsalimia. Nikamwambia nimerudisha baiskeli nilikuwa nimeazima kwenda mjini mara moja, ya kwangu ina pancha. Mmmh Sitasahau siku hiyo.