Vituko jikoni, Let us share and have fun

Vituko jikoni, Let us share and have fun

Ushawahi pika kwenye msiba ukaweka pilipili iliyopikwa kwenye rojo ya nyama ukifikiri ni nyanya iliyokuwa grated? I swear that day sintokaa nisahau. Ilikuwa jioni giza lishaanza kuingia, chakula kinapikiwa nje mwanga hautoshi, nikanyanyua pilipili badala ya nyanya. Ilicost kwa kweli, money and time.
 
hahhahahh...
mi siku ya.kwanza napika pilau I was 12,nliivisha wali vizuri then nkaeka pilau masala kwa juu nkaongeza na maji ya baridi nkakoroga na kuwasha jiko upya....hhehehe lilitokea bokoboko hataree lenye harufu ya pilau,ilibidi tule hvohvo kesho yake mama ndo akanifundisha kupika pilau
 
na kupika uji ilikuwaga changamoto sana ,kila nikipika lazma utoke.na mabonge au mzito sana,basi.mama alikuwa ananisema sana,baba ye hajali sana mana anapenda kula,hadi nlivokuja kujua siri ya uji ni kuchemsha maji na ukishaanza kukoroga usiache hadi uive...
ingine siku moja usiku nmechoka mamma kanambia nichemshe maziwa ndo niyaeke kwenye friji,nkaweka pressure cooker,sikuifunika lakini,nkawasha jiko nkaishia zangu kulala,mama kawahi kuamka alfajiri jikoni kakuta kumejaa.moshi sufuria jeusiii,shukuru Mungu sufuria lilikuwa zito,maziwa yalichemka hady yakakauka, plate ya jiko nyekunduu jiko nilijisahau likawaka usiku.mzima...hehehehhe nilichezea kchapo sitasahau,sijui ningeunguza nyumba,thanx God the worst didn't happen..
 
Jamani niko peke yangu, so nimekuwa busy the whole day kiasi kwamba mchana sijala. So nikaona ngoja nipike mboga mayai kidogo ili nile na wali, mpango wa kwanza ningekula ugali na uporo wa kuku kaanga. Nikaona chakula ni kigumu na hivi sijala mchana, so nikaopt kwenye wali na mboga mayai. Nimekaanga vitunguu, hoho na nyanya, nikavunjia yai la kwanza (la kienyeji) ikawa poa, kuongeza la pili limeharibika. Hivyo nikaharibu mboga yote.

Imagine ilibidi nianze upya, na kwa uangalifu maana mayai nimevunjia kwenye bakuli 2 tofauti badala ya kuvunjia moja kwa moja kwenye mboga.

Haichekeshi, inauma.
 
hahhahahh...
mi siku ya.kwanza napika pilau I was 12,nliivisha wali vizuri then nkaeka pilau masala kwa juu nkaongeza na maji ya baridi nkakoroga na kuwasha jiko upya....hhehehe lilitokea bokoboko hataree lenye harufu ya pilau,ilibidi tule hvohvo kesho yake mama ndo akanifundisha kupika pilau
Ha ha haaaaaaaa, pia ulijaribu maana at 12 bado mdogo kuweza kupika pishi kama pilau. Mie kuna siku hivi nilivo pilau lilinicheza, lilitoka bondo hilo. Kisa mchele wa mbeya nlikua sijazoea kupikia pilau nkajua unaekwa maji mengi kama basmati. Lkn mpk leo nimekua fundi wa kupika pilau la mchele wa mbeya
 
Nilikua naunga maharage ya wali jion
Wakati nachuja tui nikajisahau, yale machicha ya nazi nikayaweka kweny maharage badala ya tui,
Kuja kutahamaki doh..... acheni tu, na hakukua na mboga nyengine
Nilicharazwa na mama sitosahau.... mpaka leo hii nipo makini sana jikon

I like this
 
Pindi najifunza kupika Ugali, si nikapika mbichi, manake niliweka unga hata maji hayajachemka. We nilichokifanya ni kutupa batini kabla mtu hajaona Halafu nikaanza upya!!

Hahahaaa...ilinitokea kama yako, nimesonga ugali mbichi, nikaenda kuutupa kimya kimya...nikarudia kusonga mwingine nao ukawa mbichi....nikauandaa hivyo hivyo...ila nilinuna hadi nililalaaaa kwa hasiraaa.....!
 
Ndo kujifunza hivyo my dear.
 
Jamani niko peke yangu, so nimekuwa busy the whole day kiasi kwamba mchana sijala. So nikaona ngoja nipike mboga mayai kidogo ili nile na wali, mpango wa kwanza ningekula ugali na uporo wa kuku kaanga. Nikaona chakula ni kigumu na hivi sijala mchana, so nikaopt kwenye wali na mboga mayai. Nimekaanga vitunguu, hoho na nyanya, nikavunjia yai la kwanza (la kienyeji) ikawa poa, kuongeza la pili limeharibika. Hivyo nikaharibu mboga yote.

Imagine ilibidi nianze upya, na kwa uangalifu maana mayai nimevunjia kwenye bakuli 2 tofauti badala ya kuvunjia moja kwa moja kwenye mboga.

Haichekeshi, inauma.
pole sana.

hio ya mayai mie ishanipata na mie, na kila siku tunaambiwa tukiweka mayai tuvunjie moja moja kwenye kibakuli lkn hatuskii.
 
eh...eeh! nliwahi kutia omo kwenye chips nikijua ni chumvi halafu sku hiyo hakukuwa na umeme nilikuwa natembelea mshumaa...dah!
hee, hio omo uliweka wapi hata ukachanganya madesa? pole sana
 
hee, hio omo uliweka wapi hata ukachanganya madesa? pole sana

nlitia kwenye chips ndugu, mi nikitaka kuchoma chips nmezowea kuinyunyizia chumvi kabsaa! kopo lilokuwa na omo lilkuwa size moja na kopo la chumvi, fasterfaster natafuta kwenye kagiza si nikakamata omo..loh, nilikasirika na kughairi kupika siku hiyo tukanywa maji na biskuti tukalala!
 
Duh, bora hata ingekua sukari zingelika.
 
Nakumbuka kuna siku mama alilazwa, halafu nikatakiwa kesho yake nimpelekee chai.

Nikajikaza usiku mzima napika chapati, kesho yake nikapeleka chapati shapeless kabisa, zipo na mapembe kama sh 20.

Lol, wenyewe wanasema shape mbwembwe tu almuhimu utamu.
 
Kabla ya kuwa mtaalamu jikoni lazima uboronge kwanza tena vingine hata haviliki ni vya kumwaga tu. Hongera kwa kumshawishi sister wako ajiunge hapa.

Hahahah hii ya dada angu

Siku tukatamani mchuzi wa nazi.....mie nikaandaa kila kitu yeye akakuna nazi mana yeye ndo mpishi siku hiyo saaa basi tui la nazi hilo lita 2 lol bibk jingi utasema linataka kupikiwa mchuzi wa shughuli lol nkamwambia abla (dada) hilo tui jingiiii sana weee akanishikisha adabu nkae kimyaaa....

Habibty ulipikwa mchuzi ma hotpot mawili kwa wingi nyama yenyewe kilo 1 alafu mwepesiii kama wa maji hahahahahhahahaha nahiyo chumvi na ma ndimu acha tu ila huwezi amini nipishi hodari sana nowadays kwenye mapishi namugopajeeee......

Mkiona id Sherose jf chef ni yeye anakuja soon
 
Back
Top Bottom