Vituko kwenye chumba cha mtihani

Sipati picha mlivyokua mnacheat sasa hadi kubadilishana papers ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ
Apo wa kupiga chabo wanapiga chabo wakupenda umbea kushangaa wanashangaa ile siku kilinuka sana aisee kuna teacher alipigika na jamaa ๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„
 
Apo wa kupiga chabo wanaoga chabo wakupenda umbea kushangaa wanashangaa ile siku kilinuka sana aisee kuna teacher alipigika na jamaa ๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„
Aisee,,nahisi huo mtihani ndo mliongoza kwa A za kutosha ๐Ÿ˜‚
 
Nakumbuka kuna watu shuleni kwetu walikua wanazimia kipindi cha mtihani wa fizi na math๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚,, yani nikikumbukaga hua nacheka sana
๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„Hao ndo vichwa maji sasa cha kuzimia n kipi uoga au pressure
 
Jamaa alikamatwa na kibomu kwenye mtihani , msimamizi akawa anaenda mbele kufuata stepla ili aje akibane na karatasi la mtihani Kama ushahidi, jamaa aliekamatwa akakikwapua kile kibomu kutoka kwa msimamizi akakimeza . Msimamizi akabaki mdomo wazi akaishia kumtimua kwenye chumba Cha mtihani Ila akashindwa kumshtaki sababu ushahidi hakuwa nao.
 
Hustlers never made but are born [emoji120][emoji120][emoji120][emoji3]
 
hahaha msimamizi atakuwa ka mind had back benchers
 
Ile siku ya mwisho ndo tumemaliza mtihani wa physics form 4 hiyo.
Msimamizi akasema mmoja ajitolee kwenda kuhakiki kama mitihani imefungwa.

Kuna jamaa yangu mmoja alikua kakaa nyuma kabisa ndo alitolea kwenda, kwanza alivaa viatu chini ni kama vina chuma hivi ilikua anapita kwa mikogo na majigambo na zile koh koh koh za viatu vyake mpaka pale mbele hadi wasimamizi nahisi walikasirika kwa ule mwendo wake wa mikogo.

Sasa huyu mwamba alikua na kigugumizi na anakuaga na wenge sometimes, ile wameuliza enhee tuambie mtihani umefungwa?? Jamaa anasema hapana haujafungwa umwfunguliwa, wakiuliza tena jamaa anakazana kua pepa limefunguliwa.
Aloo jamaa walikasirika kumbe mchizi ni wenge ti wala hakua na nia ya kuwasumbua, ila ile mikogo yake wala hawakuamini kua kakosea kwa wenge.

Bahati nzuri walimu wanaomjua wakamtetea hakulazwa bakora.
 
Mwamba ni miyeyusho kinyama๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Nimekumbuka Miaka flani pale Makumira walituwekea kamera kwenye hall.
Wasimamizi wakawa wachache.

Tukawa tunaongea kwenye paper bila kupepesa kichwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ