Ile siku ya mwisho ndo tumemaliza mtihani wa physics form 4 hiyo.
Msimamizi akasema mmoja ajitolee kwenda kuhakiki kama mitihani imefungwa.
Kuna jamaa yangu mmoja alikua kakaa nyuma kabisa ndo alitolea kwenda, kwanza alivaa viatu chini ni kama vina chuma hivi ilikua anapita kwa mikogo na majigambo na zile koh koh koh za viatu vyake mpaka pale mbele hadi wasimamizi nahisi walikasirika kwa ule mwendo wake wa mikogo.
Sasa huyu mwamba alikua na kigugumizi na anakuaga na wenge sometimes, ile wameuliza enhee tuambie mtihani umefungwa?? Jamaa anasema hapana haujafungwa umwfunguliwa, wakiuliza tena jamaa anakazana kua pepa limefunguliwa.
Aloo jamaa walikasirika kumbe mchizi ni wenge ti wala hakua na nia ya kuwasumbua, ila ile mikogo yake wala hawakuamini kua kakosea kwa wenge.
Bahati nzuri walimu wanaomjua wakamtetea hakulazwa bakora.