Vituko kwenye chumba cha mtihani

Nimekumbuka Miaka flani pale Makumira walituwekea kamera kwenye hall.
Wasimamizi wakawa wachache.

Tukawa tunaongea kwenye paper bila kupepesa kichwa
Ikawaje sasa,,, mlistukiwa auπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Namkumbuka mwanangu mmoja, NECTA Form 2, 2010, pepa ya Bailojia tushatumia kama dakika 40 ndani ya chumba cha mtihani. Pepa imekaza vibaya. Mbele ya macho ya msimamizi jamaa kachomoa bonge la karatasi kutoka kwenye soksi yake. Kila mtu anamshangaa jamaa na atakachofanywa na msimamizi. Lakini huwezi amini msimamizi akawa anampita tu wala haoni.
Yule jamaa alikuwa na itikadi za mambo ya nguvu za giza.

Lile tukio lilituchekesha na kuleta mzuka siku ile ndio lilikuwa stori ya shule.

Huyu jamaa tukiwa form4 alikuja kupotelea misitu ya pugu na kazimzumbwi alipokwenda kutafuta mitishamba kwenye mambo yake ya uganga na tiba za jadi mpaka wa leo jamaa hakurudi tena.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimechekaaa sanaa, mie nilikutwa ila hakikua changu, kilidondokea kwangu vibaya.
Sitaki kukumbukaaa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
kuna mwamba mmoja alistukiwa kuwa ana kibomu akaona isiwe shida akamtupia mwenzake pembeni (walishirikiana kikiandaa).., mwisho wa siku alidakwa yule alierushiwa kibomu akatolewa nje
 
Mtu kakutwa na Kibomu....
MSIMAMIZI: We mbona umeingia na Karatasi ya Majibu humu

MWANAFUNZi: Hata katika Computer kuna External kama Computer imejaa basi External inasaidia.... sasa Mi Ubongo wangu umejaa ndo nimehamishia humu
 
Form 2
Kibomu gazeti kile kilikuwa kimegawanywa mara sita, sasa upande jamaa aliofungua mmiliki wa kibomu wadau wote tunaziona zile Empire za Mali ,Wwangendaba 😁 na ndipo swali lilipo yeye anahangaika kutafuta.

Jombaa alikuwa mita chache toka kwa jirani aliyekuwa na kiboma gazeti akihangaika , mwamba yule chini ya uangalizi mkali wa tuliomzunguka , ile msimamizi kageuza mgongo , Jombaa akasimama kama jeti paap mpaka kwa mmiliki kibomu akakwapua lile karatasi.

Sehemu iliyotufanye tule fire ni jamaa mwenye alinyang'anya mmliki wa kibomu aliongea kwa sauti kali.

''Wewe kenge sisi tunafeli huku nyuma wewe hapo umekaa na majibu ,huoni Zwangendaba hii hapa''πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜› kofi la kumseti mwenye kibomu.
Kilichofuata pale nyuma tulijua maana ya wasimamizi wa mtihani ni watu gani.

Ila sijui miujiza gani ulimfanya msimamizi mkuu aligeuza maamuzi maana darasa zima lilibuka na kicheko Mzee yule alisema hawa watoto wahuni waacheni wajifie huko.

Mitihani iliyokuja mbele Mzee anatangaza wenye Magazeti ya Zwangendaba yatolewe mapema.
 
Nimekumbuka Miaka flani pale Makumira walituwekea kamera kwenye hall.
Wasimamizi wakawa wachache.

Tukawa tunaongea kwenye paper bila kupepesa kichwa
Hahaha unahoji swali umekaza shingo mbayaaa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtu kakutwa na Kibomu....
MSIMAMIZI: We mbona umeingia na Karatasi ya Majibu humu

MWANAFUNZi: Hata katika Computer kuna External kama Computer imejaa basi External inasaidia.... sasa Mi Ubongo wangu umejaa ndo nimehamishia humu
wakuu afu kumbe wasimamizi huwa wanajua tunaigilizia afu wanavunga kutuchora tu
 
Kuna ile tabia msimamizi anasimama anaganda nyuma ya anayefanya mtihani!
Sasa kuna mwamba mmoja yeye alikuwa back bencher, siku ya pepa akabeba kibomu na kula maharage, mixer mayai sijui na matakataka gani!
Basi kwenye pepa msimamizi kama kawaida kaenda kusimama nyuma yake, mwamba akaanza kuachia ushuzi tu, msimamizi akayoyoma pale mwamba akatoa kibomu chake na kupiga chabo huku akiendelea kuachia ushuzi, majirani zake walikoma kwa kweli.. ila nia yake ilitimia!!
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]Duuh hatarii sanaa aisee...
 
In short ni kwamba, kuna msukuma mmoja alipiga mshindo magoli mawili ya mfululizo ndani ya chumba cha mtihani,
Ilikuwa mock exams, siku ya jumanne kwenye mathematic. Hii ni baada ya ghaka kubuma.
 
 
In short ni kwamba, kuna msukuma mmoja alipiga mshindo magoli mawili ya mfululizo ndani ya chumba cha mtihani,
Ilikuwa mock exams, siku ya jumanne kwenye mathematic. Hii ni baada ya ghaka kubuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…