Leejay49
JF-Expert Member
- Feb 10, 2023
- 16,388
- 51,970
Ikawaje sasa,,, mlistukiwa au😃😃Nimekumbuka Miaka flani pale Makumira walituwekea kamera kwenye hall.
Wasimamizi wakawa wachache.
Tukawa tunaongea kwenye paper bila kupepesa kichwa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ikawaje sasa,,, mlistukiwa au😃😃Nimekumbuka Miaka flani pale Makumira walituwekea kamera kwenye hall.
Wasimamizi wakawa wachache.
Tukawa tunaongea kwenye paper bila kupepesa kichwa
🤣🤣🤣 sitaki kukumbuka
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Apo wa kupiga chabo wanapiga chabo wakupenda umbea kushangaa wanashangaa ile siku kilinuka sana aisee kuna teacher alipigika na jamaa [emoji1][emoji1]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimechekaaa sanaa, mie nilikutwa ila hakikua changu, kilidondokea kwangu vibaya.Jamaa alikamatwa na kibomu kwenye mtihani , msimamizi akawa anaenda mbele kufuata stepla ili aje akibane na karatasi la mtihani Kama ushahidi, jamaa aliekamatwa akakikwapua kile kibomu kutoka kwa msimamizi akakimeza . Msimamizi akabaki mdomo wazi akaishia kumtimua kwenye chumba Cha mtihani Ila akashindwa kumshtaki sababu ushahidi hakuwa nao.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ile siku ya mwisho ndo tumemaliza mtihani wa physics form 4 hiyo.
Msimamizi akasema mmoja ajitolee kwenda kuhakiki kama mitihani imefungwa.
Kuna jamaa yangu mmoja alikua kakaa nyuma kabisa ndo alitolea kwenda, kwanza alivaa viatu chini ni kama vina chuma hivi ilikua anapita kwa mikogo na majigambo na zile koh koh koh za viatu vyake mpaka pale mbele hadi wasimamizi nahisi walikasirika kwa ule mwendo wake wa mikogo.
Sasa huyu mwamba alikua na kigugumizi na anakuaga na wenge sometimes, ile wameuliza enhee tuambie mtihani umefungwa?? Jamaa anasema hapana haujafungwa umwfunguliwa, wakiuliza tena jamaa anakazana kua pepa limefunguliwa.
Aloo jamaa walikasirika kumbe mchizi ni wenge ti wala hakua na nia ya kuwasumbua, ila ile mikogo yake wala hawakuamini kua kakosea kwa wenge.
Bahati nzuri walimu wanaomjua wakamtetea hakulazwa bakora.
Hahaha unahoji swali umekaza shingo mbayaaa.Nimekumbuka Miaka flani pale Makumira walituwekea kamera kwenye hall.
Wasimamizi wakawa wachache.
Tukawa tunaongea kwenye paper bila kupepesa kichwa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Form 2
Kibomu gazeti kile kilikuwa kimegawanywa mara sita, sasa upande jamaa aliofungua mmiliki wa kibomu wadau wote tunaziona zile Empire za Mali ,Wwangendaba [emoji16] na ndipo swali lilipo yeye anahangaika kutafuta.
Jombaa alikuwa mita chache toka kwa jirani aliyekuwa na kiboma gazeti akihangaika , mwamba yule chini ya uangalizi mkali wa tuliomzunguka , ile msimamizi kageuza mgongo , Jombaa akasimama kama jeti paap mpaka kwa mmiliki kibomu akakwapua lile karatasi.
Sehemu iliyotufanye tule fire ni jamaa mwenye alinyang'anya mmliki wa kibomu aliongea kwa sauti kali.
''Wewe kenge sisi tunafeli huku nyuma wewe hapo umekaa na majibu ,huoni Zwangendaba hii hapa''😛😛😛 kofi la kumseti mwenye kibomu.
Kilichofuata pale nyuma tulijua maana ya wasimamizi wa mtihani ni watu gani.
Ila sijui miujiza gani ulimfanya msimamizi mkuu aligeuza maamuzi maana darasa zima lilibuka na kicheko Mzee yule alisema hawa watoto wahuni waacheni wajifie huko.
Mitihani iliyokuja mbele Mzee anatangaza wenye Magazeti ya Zwangendaba yatolewe mapema.
wakuu afu kumbe wasimamizi huwa wanajua tunaigilizia afu wanavunga kutuchora tuMtu kakutwa na Kibomu....
MSIMAMIZI: We mbona umeingia na Karatasi ya Majibu humu
MWANAFUNZi: Hata katika Computer kuna External kama Computer imejaa basi External inasaidia.... sasa Mi Ubongo wangu umejaa ndo nimehamishia humu
Wasimamizi wengine utasikia SAIDIANENI ILA SITAKI KELELEwakuu afu kumbe wasimamizi huwa wanajua tunaigilizia afu wanavunga kutuchora tu
hahahahahahaha...Wasimamizi wengine utasikia SAIDIANENI ILA SITAKI KELELE
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]Duuh hatarii sanaa aisee...Namkumbuka mwanangu mmoja, NECTA Form 2, 2010, pepa ya Bailojia tushatumia kama dakika 40 ndani ya chumba cha mtihani. Pepa imekaza vibaya. Mbele ya macho ya msimamizi jamaa kachomoa bonge la karatasi kutoka kwenye soksi yake. Kila mtu anamshangaa jamaa na atakachofanywa na msimamizi. Lakini huwezi amini msimamizi akawa anampita tu wala haoni.
Yule jamaa alikuwa na itikadi za mambo ya nguvu za giza.
Lile tukio lilituchekesha na kuleta mzuka siku ile ndio lilikuwa stori ya shule.
Huyu jamaa tukiwa form4 alikuja kupotelea misitu ya pugu na kazimzumbwi alipokwenda kutafuta mitishamba kwenye mambo yake ya uganga na tiba za jadi mpaka wa leo jamaa hakurudi tena.
Kuna ile tabia msimamizi anasimama anaganda nyuma ya anayefanya mtihani!
Sasa kuna mwamba mmoja yeye alikuwa back bencher, siku ya pepa akabeba kibomu na kula maharage, mixer mayai sijui na matakataka gani!
Basi kwenye pepa msimamizi kama kawaida kaenda kusimama nyuma yake, mwamba akaanza kuachia ushuzi tu, msimamizi akayoyoma pale mwamba akatoa kibomu chake na kupiga chabo huku akiendelea kuachia ushuzi, majirani zake walikoma kwa kweli.. ila nia yake ilitimia!!
In short ni kwamba, kuna msukuma mmoja alipiga mshindo magoli mawili ya mfululizo ndani ya chumba cha mtihani,
Ilikuwa mock exams, siku ya jumanne kwenye mathematic. Hii ni baada ya ghaka kubuma.