Vituko kwenye daladala

Vituko kwenye daladala

fakalava

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2015
Posts
4,459
Reaction score
6,027
Leo katika kuvuta kumbukumbu nikajikuta nakumbuka baadhi ya vituko kadhaa nilivyowahi kuviona au kukumba navyo kwenya daladala.

Nitavitaja baadhi.

1. Kuna siku nikapanda daladala, ilikuwa ni mwanzo wa Kituo ila wakati naingia ndani ya gari tayari kulikuwa na watu wameingia ndani.
Kuna jamaa alikuwa amekaa katikati ya viti viwili, yaani ile double sit yeye kakaa katikati kitu ambacho kiliwapa watu ugumu wa kukaa pale hasa wanaume
Kumbe ilikuwa ni timing akiona mwanamke mlangoni anaingia kwenye gari anasogea ili huyo mwanamke akae naye. Hasipo kaa pale basi atarudi tena kukaa katikati ya sit.
Baada ya kuliona hili nilifanya utafiti kidogo, nikagundua kuwa baadhi ya wanaume hasa kwenye usafiri wa umma upenda kukaa na wanawake, kadhalika wanawake upenda kukaa na wanaume.

2. Kuna maeneo ambayo usafiri ni wa shida, kama vile: Mbagala, Gongolamboto, Kimara, nk. Maeneo hayo mara nyingi abiria wa kusimama ni wengi kuliko wanaokaa, abiria hawa hukaa kwa mtindo wa kuelekezana makalio, lakini mara nyingine utakuta lijamaa limesimama kwa kumuelekea mwanamke mgongoni. Jamaa akishajioset mkao huo hata kondakta amwambie asogee, hatosogea katu. Lakini utashangaa mwanamke kakaliwa hivyo ila yeye katulia kana kwamba ni jambo la kawaida.

3. Hii imewai kunitokea! Nimeshuka pale Gongolamboto nikapanda gali (Hiace) la Chanika, nilikaa sit ya mbele kwa upande wa nyuma yaani sit ya nyuma ya dreva.
Nyuma ya dreva pale kuna kibench, nikaona watu wanaanza kukaa pale kisa akaja mama mmoja kajaziajazia akaniambia nikae vizuri na yeye akae, akaona simuelewi nikaona anavusha nguu mmoja akauweka katikati ya miguu yangu na mguu wangu mmoja ukawa katikati ya niguu (mapaja yake), kumbe route hiyo hilo ni jambo la kawaida.
Safari ikaanza, kumbe wanawake wana kamchezo kao! Mara nikahisi kama mguu wangu kiasi fulani umebanwa na mapaja ya yule mama, mara nikahisi nyuzi joto zinapanda.
Nikiwa nimejifanya kama nimeangalia chini kumbe namsoma huyu mama nikaona kumbe kila akifanya hayo anaangalia muitikio wangu ukoje. Kwa kweli hii safari ilinipa mtihani japo niliimaliza salama.

Je, wewe uliwai kukuta na kituko gani kwenye usafiri wa umma, kikakushangaza, kikakusisimua, kikakufurahisha, au kikakushutua.
 
Kuna wanawame washenzi sana kwenye madaladala..
Huwa wanapenda kuona mtu anapata mfadhaiko tu
 
Back
Top Bottom