Vituko mitandaoni. Tupia chako
JIFUNZE KWA MOURINHO🗣️

Jose Mourinho anasema nilipokuwa kocha wa Inter Milan alikuja mbele yangu mchezaji Zlatan Ibrahimovic akasema nataka kuondoka klabuni hapa ili nikashinde ubingwa wa UEFA.

"Wasaidizi wangu walihofia wakiamini kuwa hatuwezi kushinda bila yeye, hata wachezaji wenzake hawakutaka tumpoteze".
Hata mimi nilipata hofu lakini nikasema pengine ukiondoka tutashinda.

Kisha nikasema kama ataondoka tutajaribu kumsajiri Samuel Etoo ambae alikuwa anacheza Barcelona ambayo Etoo alitaka kwenda.
Niliamini kuwa Diego Milito na Etoo wanaweza kuleta kitu cha tofauti kimbinu ndani ya timu yetu.

Mazungumzo yakafanyika Ibrahimovic na Etoo wakabadilishana timu.
Ibrahimovic alidumu kwa msimu mmoja tu ndani ya Barcelona lakini Etoo alishinda mataji matatu mfululizo akiwa na Inter.

Kupitia kisa hiki tunajifunza kwamba kwenye maisha kuna wakati unatakiwa kuwaacha baadhi ya watu waondoke kwenye maisha yako hata kama unawapenda kupita maisha yenyewe....

Inawezekana Mungu amepanga ushinde makubwa ukiwa bila wao kwa sababu uwepo wao unaziba milango ya watu wengine waliobora kuja kwenye njia yako na kukusaidia kufikia malengo yako.

©JIFUNZE KUJIFUNZA
Safi sana.
Kupitia njia kama hizi tulishawafuta wengi.
Kuna watu hudhani wana thamani kubwa zaidi kuliko aliyetuumba.
 
FB_IMG_17303779634665915.jpg
 
Ni wazi Rais Samia ameonyesha uwezo mkubwa wa kuongooza na kuizamisha CHADEMA. Ndiyo maana nasema tusimharibie. CCM imeonyesha uwezo kufunika upinzani kwa theluji nzito ya hoja na mipango mikakati mizuri kabla na baada ya uchaguzi.
Ama kweli siasa ni sayansi.
Magufuli alitumia nguvu kuivunja Chadema, Samia anatumia sayansi kupunguza nguvu za Chadema.
Ushauri wangu kwa chadema, Mbowe awaachie wengine nao watumie maarifa yao kupeleka mbele chama hicho.
 
Ex girlfriend wa Elon Musk alimblock Elon kwenye Twitter baada ya kupata mpenzi ,Amber Heard alimuacha Elon musk kwasababu alipata mpenzi mpya twitter ,kitendo hiki kilimkera Elon Musk akaamua kuinunua twitter Kisha akamzuia ex wake kutumia mtandao wa twitter na kuibadirisha twitter kuwa na jina la X😁😁😁😁View attachment 3139184
Majibu ya ChatGPT baada ya kumuuliza ukweli wa hii stori
Screenshot 2024-11-01 112722.png
 
Back
Top Bottom