Tajiri Sinabay
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,333
- 3,619
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😆😆😆😆 duh watu mnajiongeza sikuwaza ati.Huyo hajaelewa.... anaombwa aende uvinza...🏃♀️🏃♀️🏃♀️
Wenye vibamia tunateseka sana
Duh nilijilaumu sana, unajuwa kumkosea mtu ambae ni mpole sio mshari (kwa ninavodhania) roho inakuuma wewe mtenda kosa.Usiwaze! Wala sikumaanisha
Ni vizuri tukiwa kama vijana kuhamasika kwa wingi kujiunga na jeshi la kulinda nchi 😆😆😆😆
Pole! Sikumaindi nilichukulia umenitania tu.Duh nilijilaumu sana, unajuwa kumkosea mtu ambae ni mpole sio mshari (kwa ninavodhania) roho inakuuma wewe mtenda kosa.
Nilikumbuka zamani kidogo (nadhani ni 2017)
Niliwahi kuwa na rafiki mtandaoni facebook, alikuwa ni mrangi yule dada, alikuwa mzuri balaa wale macho yao yanakuwa kama ya wazungu weupe. Urafiki wetu ulikolea hasa, kama unavyojuwa urafiki wa mtandaoni (sikuwahi kumtongoza wala kuwazia) alikuwa anapenda sana maudhui yangu ya vichekesho kupitia picha (nilikuwa natengeneza mwenyewe kipindi hiko na zilikuwa zinatrend karibia nchi nzima kwenye magroup ya FB)
Siku moja nikaichukuwa moja ya picha za yule dada ambayo aliipiga akiwa amejisitiri vizuri tu, nikachukua na picha ya dada mwingine ambae ni mbaya mno kimwonekano (umbo)
Nikazi editi.
Picha ya yule mdada mwingine pembeni yake nikaweka msosi uliopikwa vizuri mno hadi unatamanisha kuula.
Picha ya yule rafiki yangu sasa nikaeditia pembeni yake miguu ya kuku miwili ikiwa kwenye sahani imeungua upande.
Picha ilileta maana kwamba wanawake mazuri kimuonekano sio mafundi kwenye mapishi.
Nikaichapisha kwenye akaunti yangu huku nikidhani akiona atapenda.
We! amekuja kuiona ni baada ya masaa kadhaa tangu niiweke, asee hiyo siku nilitishiwa hadi kifungo.
🙏🙏🙏Pole! Sikumaindi nilichukulia umenitania tu.