Vituko mitandaoni. Tupia chako
Showcase of Creative but Weird Animal Photo Manipu.jpeg
 
Juzi kati niliona tangazo Facebook kampuni ya Vunjabei Bidhaa Za Majumbani wanatangaza wanahitaji vijana wa mauzo mshahara 450000 nauli na kula juu ya kampuni chap nikachukua namba akapokea dada mmoja nikajitambulisha nikamwambia Niko tayar basi AKANIAMBIA nifike ofisini na kitambulisho au namba ya nida na barua ya serikali ya mtaani kwangu.

Kwa kuwa nilikuwa busy hio ijumaa nikaomba niende jumamos ofisini AKANIAMBIA nifike saa 7 mchana.

Basi nikafika mpaka ilala ofisin kwao nikapokelewa kuingia ndani nikakutana na watu wengi vijana Kwa wazee wamekula shati nyeupe suruali nyeusi na tai nyeusi Salamu yao ni GOOD MORNING BILLIONAIRE nikajiuliza mchana huu good morning au naota NIKATOKA ukumbini kwenda nje nikakuta jua Kali nikarudi ndani.

Supervisor mmoja ananiambia hapa kijana Salam yetu ni good morning Billionaire maana wewe ni tajiri ajae moyo Wang ulijaa sana furaha mithili ya mwanaume aliyefanikiwa kutoa bikra ya Binti mshika ibada.

Basi yule dada AKANIAMBIA kesho utaanza kazi na eneo lako ni temeke yote wewe utakuwa afisa masoko wetu.

NIKASEMA asante Mungu Leo hii nakuwa afisa masoko na elimu yang ya ufundi umeme veta
Basi leo NAFIKA OFISINI NAULIZWA tukupe bidhaa Gani ukauze vyombo mafuta viti au kapeti NIKASEMA viti ndo nimepewa viti hivyo nahangaika navyo JUANI ila mshahara sio 450000 ni. Commission utalipwa kutokana na mauzo ila hawanijui jion sirudi ofisini na Hela naenda kubetia kmmmk😂😂😂😂
20241008_033501.jpg
 
Back
Top Bottom