kocha Nabi
JF-Expert Member
- Feb 1, 2022
- 709
- 1,881
- Thread starter
- #21
hivi madereva wa mabasi wanaipendea nini ile hotel ya singida pale, hasa mabasi ya kanda ya ziwa. nilikutana na mshkaki sijui wa juzi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Itakuwa ya huyo kiumbe hapo pembeni
🤣🤣🤣Itakuwa ya huyo kiumbe hapo pembeni
[emoji23][emoji23] Dogo Masta sana huyo, eti Mama nakunyaSiku moja baada ya zile shamra shamra za sikukuu nlikua natoka dom.
Kipimdi hyo gari zimeshona balaa kupata siti n mtihani.
Kupitia connection kibao nkawa nmepata ka siti ndani ya hyo basi.
Pembeni yangu kulikua na mdada ( maama tukisema mmama kias flan hajakidhi vigezo).
Nakumbuka alikua na watoto watatu.
Wale machalii hawapishani sana, tunasema wamezaliwa kama ngazi.
Mashine imeacha mnada mpya tu kash kash zikaanza, madogo ful usimbufu, mara huyu kamkwida mwenzie, mara huyu ametupa chupa ya maji n.k.
Yule dada hapo anakomaa kunyinyesha kale ka mwisho.
Mpka tumefika bahi, discipline ya wale watoto bado iko pwani.
YUle manzi nkaona akatafakariii, ghafla akakomaa kumnyonyesha yule mdogo mpka akashiba akalala.
Alivolala tu, akampa abiria wa ipande mwingine amshike mtoto mara moja.
Aisee, yule dada alimtembezea mtoto mkubwa kichapo HEAVY na hapo mashine inazidi kuyeya tu.
Dogo alikula kifinyo, alikua anapiga nduru kama yote lakn hakuna wa kumsaidia, maza mtu yuko bize kuonyesha ukakamavu wa kipondo.
Kwakua abiria tushachoka mayowe na usumbufu wote tumemyuti tunaangalia hyo show.
Dogo nafkiri akapiga hesabu, akaona hapa bi mdash ataniwahisha mawinguni, ikabd aje na tactic mpya.
Kilio ikageuka from mama, mamaaa, up to
MAMA USINIPIGE TENA NAJISKIA KUNYA, MAMA NAJINYEA MIMI.
Aaah hapo abiria tukaona sasa hii inataka kuharibu weather, ikabd tumwambie amteme tu maana dogo akikata chela mule ndani safari itakua ngumu.
Ndo chalii akaachiwa. I remember dogo hakuongeza neno, aliegemea siti akalala amekuja kuamka singida. Akashuka akakojoa, akarudi akafinya diko, akakata tena moto mpka almost mwanza.
maliasili ipo KibitiKwenye mwezi Wa 11 mwaka jana natoka MASASI kurudi DAR nimepanda WARDA EXPRESS chuma piriuu, bado ina maganda kwenye siti ,ac unaganda
Tumetoka Nangurukuru, chuma pigwa gia sana tupo mbali karibia na kituo cha ukaguzi wa maliasili kina choo cha kulipia upande wa kushoto kama unatoka LINDI nadhan no bungu pale.
Kuna msela brothermen kapiga modo akatoka nyuma mbio anawahi kwa dereva kufika pale dereva mambo yakakataa alitapika balaa, tapikia dashboard, dereva, aotibta dereva, kondakta , pale kwenye kigodoro kapachakaza. Jamaa walimind balaa ila ndio hakuna namna. Ikabidi tusimame hapo bungu gari ipigwe usafi .
hiyo kuna mbibi inaonekana aliwaambia abiria wa nyuma kuwa anataka kususu sasa kama mixer wamemwambia hapa tupo mjini haturuhusiwi. bibi kavumilia kashindwa kaja kwa dere kaangua kilio anataka kususu 🤣🤣🤣Chuma ya Adventure imetoka Kakonko mama mmoja katafuna menyu mchanganyiko kwenye mgahawa fulani na safari ikaanza. Baadae mama akaomba kuchimba dawa dereva agagoma. Akarudia kuomba mara ya pili wakagoma. Akawapa dakika 5 wasimame wakagoma, basi mama alivua pichu kwenye ngazi za gari akamwaga maji shwaaaaaaaa
hiyo mkuu VW GTI itakuwa 300 kph. mjerumani sio wa kumchezea.Nimemaliza kisahani halafu napigiwa honi na kiVolkswagen golf kinaomba njia huku kimeniwashia na taa.
Hicho kigari kinakimbia bwana. Nilikuwa na Gx110 mark2 grande, 180+kph(185-190) rpm 4. Ninauhakika hata ningekuwa na Fortuner nisingekapata kale kadude.hiyo mkuu VW GTI itakuwa 300 kph. mjerumani sio wa kumchezea.
🤣🤣🤣 pole sana kiongozi.Hicho kigari kinakimbia bwana. Nilikuwa na Gx110 mark2 grande, 180+kph(185-190) rpm 4. Ninauhakika hata ningekuwa na Fortuner nisingekapata kale kadude.
Njia ilikuwa imenyooka lakini kalikuwa kanapotea mbele ya upeo wa macho yangu nakashuhudia.
Saidia mtoto. Wacha ujingakingine hichoView attachment 2531751
Hatari sana hii1- Day moja nimetoroka chuo nipo Tanga kumuona mama na kula maisha kidogo.
Nipo home mida ya saa 3-4 asubuhi jamaa angu akanipigia simu kuwa kesho asubuhi raia zinasaini boom. Na utaratibu wa UDOM ulikua miyeyusho flan hivi.
Nikavaa chap, nikaaga home nikadaka basi la kampuni ya SATELITE linatoka Tanga Saa tano asubuhi lengo nishuke Chalinze niunge chuma za Dar za jioni.
Ile basi ni scania, ilikua inamwagika haswa yani, unasikia jiko la msweden linapiga mluzi tu. Kupita mkata kwa mbele kidogo dereva aliyumba yumba kukaa sawa tukasikia mzinga eneo la engine jamaa akayumba mpaka likakaa sawa parking. (Bahati nzuri nilikua siti za mbele)
Tukashuka, huku tunamuhoji dereva shida nini, akasema ule mzinga tumesikia aligonga KANGA (Hawa ndege kama kuku) kufunuliwa mashine tukakuta fan belt imekatika. Hakuna damu, dalili za damu wala manyonya. Ila dereva msimamo wake ni kuwa aligonga KANGA.
Ila hakika hatukumuona
2-DEREVA WA IBRA LINE YA MTWARA MWENYE UGONJWA WA KUSINZIA.
Siku naenda Lindi kazini, nikapanda IBRA LINE (not sure na hili jina kama ni IBRA LINE au IBRA classic)
NIkawa Siri ya mbele kabisa upande wa fala. Cha ajabu kondakta mwanamke akawa anakusanya vifuniko vya chupa za plastic akajaza kwa dashboard.
Muvi linaanza dereva kaingia jicho kama kapiga ganja, akanza kutafuna kifuniko na mwendo, kiisha lainika anatema anachukua kingine.
Kuka muuliza kondakta akaniambia asipofanya hovyo anasinzia kabisa,[emoji23][emoji23][emoji23]
3-ABIRIA KAZIMIA KWA SABABU YA MWENDO
Natoka dar kwenda Chimala Mbeya -2012, in summary gari iliharibika tukaondoka Moro 11 jioni kwenda mbeya. (basi la PRINCES MURO) hiyo chuma ilipigwa gia mpaka tukaanza kusali salamu Maria na Baba yetu.
Ilipigwa kiatu kufika iringa imezingua Tena. Taptizo lake ilikua gia zinaishia namba 3, ilirekebishwa. Iliondoka na Ukali sio wa kawaida (Yutong) ilipigwa gia mpaka kuna mother alizima. Tukamshusha makambako hospital, chuma ikarudi road na mto mwingi sana.