Vituko na vioja vya wadada wa benki

Vituko na vioja vya wadada wa benki

Wananipenda

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Customer kero is more pronounced in public service ila private sector wanajitahidi kwa customer care ila watumishi wanawake sehemu yeyote ni kero ila Mimi huwa sikopeshe nakuchana makavu on the spot but kama una cash let say below Laki 5 ni bora kwenda kwa wakala au mobile transactions
 
Ndio mimi ni mdada ila siwezi kumjibu mtu hovyo wala kumringia ringia mtu
Great!

Wanaofanya hivyo wengi wanakuwa hawajitambui ni nini wanafanya,hawajieshimu

post using my macbook air using jamiiforums app
 
Pamoja na huduma mbovu za baadhi ya wafanyakazi wa benki labda wateja wengine nao wana matatizo. Au wengine mnaenda benki tofauti kila siku?
Benki yako(yaani una akaunti hapo muda mrefu) lazima utakuwa unajulikana na wahudumu wengi tu na mnaweza kuwa marafiki kitu ambacho kitakusaidia kupata huduma nzuri ambayo unastahili kuipata hata ukiwa huna rafiki.
Mimi ninapo-bank nawajua wahudumu wote hadi branch manager kwa sababu hii labda ndio maana napata first class service,wafanyakazi wote wa bank hadi walinzi wa security company wananifahamu na ni 'marafiki'
Habari ya kuibiwa hela na teller ukishafahamiana na hawa watu haipo,tena muda mwingine unakuta foleni kubwa au system down unamuachia hela anakugongea tu muhuri system ikiwa fresh anamalizia transaction.
Tuwaheshimu wengine na sisi watatuheshimu.
kufahamiana na wahudumu kisiwe kigezo cha kupewa huduma ``first class``....huduma inabidi zitolewe kwa kufuata sheria na taratibu zakazi,kwa hiyo siku ukienda benki nyingine usiyofahamika utaanza kujipendekeza pendekeza ili ufahamike?,hela yangu halafu mtu aniletee pozi,mi siwezi vumilia huo ujinga ,labda ndo maana wanawafungia kwenye vile vi-cube,nahisi hata akili zao zinafungwa (kwa baadhi lkn)
 
Wakuu za mida hii?

Leo nimeona tuwaangazie hawa dada zetu wa benki ambao baadhi yao wanadharau sana kitu ambacho ni kinyume na maadili ya kazi zako.Mkuu tutajie jina la hiyo benki tuanzie hapo kwanza.

Kuna kipindi rafiki yangu alienda benki moja kuulizia wamefikia wapi mchakato wa kuwaita kwenye " interview " cha ajabu yule dada akamjibu nanukuu " unadhani ukijipitisha hapa ndio utaonewa huruma" .

Mimi pia kuna dada benki teller alinidharau wakati ananihidumia nikamuangalia tu.

Je wewe umekutana na lipi kutoka kwa hawa Maofisa wa kike wa benki?

Nawasilisha.
 
Wakuu za mida hii?

Leo nimeona tuwaangazie hawa dada zetu wa benki ambao baadhi yao wanadharau sana kitu ambacho ni kinyume na maadili ya kazi zako.

Kuna kipindi rafiki yangu alienda benki moja kuulizia wamefikia wapi mchakato wa kuwaita kwenye " interview " cha ajabu yule dada akamjibu nanukuu " unadhani ukijipitisha hapa ndio utaonewa huruma" .

Mimi pia kuna dada benki teller alinidharau wakati ananihidumia nikamuangalia tu.

Je wewe umekutana na lipi kutoka kwa hawa Maofisa wa kike wa benki?

Nawasilisha.

Walikuwa kwenye period hao plus its possible wewe mwenyewe utakuwa una haiba ya kike, which makes for a bad combo.
 
Hao wengi wao wamepewa kazi kwa kutoa rushwa, lakini wanatuletea nyodo ambao hatuna kazi.
 
Washamba tu yan wanataka ukifika dirishan uanze kuwatetemekea utadhan ni malaika..
 
***** mmenikumbusha miaka ya nyuma hivi.

Niliingia benki moja nikaenda kwenye dirisha la maulizo,
Mungu wangu nilivojibiwa kuhusu kufungua akaunti, niliambiwa subiri, kweli asee ilikuwa subiri ya maana.

Nikasema poa na utu uzima wangu huu huyu mtoto ananichezea akili??
Nikachukua ki begi nikaingia kwa meneja, nikamwambia bwana nina vijihela hapa, nataka kufungua akaunti,
Akaniambia umeenda maulizo??
Nikamjibu ndio toka saa tatu mpaka sasa saa sita nimeambiwa nisyubiri au kwa kuwa mi sina suti??

Asee meneja akanifungulia nikaweka mzigo wangu, mwisho akaniahidi atalifanyia kazi na aliniomba radhi kiukweli.

Nilichoshangaa siku moja yule dada alinikuta offucine anatafuta kazi akanipa nyaraka zake, nikaamuambia nitampa taarifa aje kwenye usaili

Mungu anisamehe nilimpa taarifa kuwa anatakiwa aje kwenye usaili siku mbili baada ya usaili wenyewe.

Aliumia mnoo lakini nilishatubu asee, mi hata madirishani siku hizi siingii aseee
duuu teh teh teh aise ila wamezidi sana ukikaa vibaya wana kutapeli kabisa.
 
Kwa Tanzania mteja ni fala c bank c bar c mgahawani kokote hovyo 90%
Uko sahihi mkuu,hebu fikiria hata muhudumu wa bar!!!jamani hebu katizeni hapo Kenya muone tofauti iliyopo shida kubwa ninayoiona ni elimu na kupata kazi hiyo kwa mgongo wa ndugu,rafiki na mapenzi pia.
 
kuna mdada benki tela alinimind eti nimempa hela huku nimezikunja kwenye mafungu ya laki moja moja. nikamjibu ndio kazi yako kukunjua. hela zangu mwenyewe bado unitukane tena mbele za watu, shubaaaaamit
 
duuu teh teh teh aise ila wamezidi sana ukikaa vibaya wana kutapeli kabisa.
Sio wa kuwachekea, ndio maana mi nikifika hua nafuata utaratibu, nikimaliza wajibu wangu akijichanganya tuu mi hua nauzunguka mlango naenda kwa bosi

Kuna mmoja alinikera, nikamwambia ukiniona hapa mara mbili ujue nimeleta hela ambayo hata ukistaafu na ukasamehewa na mikopo hutoipata.
Nilikuwa nishachanganyikiwa,
 
Uko sahihi mkuu,hebu fikiria hata muhudumu wa bar!!!jamani hebu katizeni hapo Kenya muone tofauti iliyopo shida kubwa ninayoiona ni elimu na kupata kazi hiyo kwa mgongo wa ndugu,rafiki na mapenzi pia.
Hakuna mapenzu, wengi ngono mkuu
 
***** mmenikumbusha miaka ya nyuma hivi.

Niliingia benki moja nikaenda kwenye dirisha la maulizo,
Mungu wangu nilivojibiwa kuhusu kufungua akaunti, niliambiwa subiri, kweli asee ilikuwa subiri ya maana.

Nikasema poa na utu uzima wangu huu huyu mtoto ananichezea akili??
Nikachukua ki begi nikaingia kwa meneja, nikamwambia bwana nina vijihela hapa, nataka kufungua akaunti,
Akaniambia umeenda maulizo??
Nikamjibu ndio toka saa tatu mpaka sasa saa sita nimeambiwa nisyubiri au kwa kuwa mi sina suti??

Asee meneja akanifungulia nikaweka mzigo wangu, mwisho akaniahidi atalifanyia kazi na aliniomba radhi kiukweli.

Nilichoshangaa siku moja yule dada alinikuta offucine anatafuta kazi akanipa nyaraka zake, nikaamuambia nitampa taarifa aje kwenye usaili

Mungu anisamehe nilimpa taarifa kuwa anatakiwa aje kwenye usaili siku mbili baada ya usaili wenyewe.

Aliumia mnoo lakini nilishatubu asee, mi hata madirishani siku hizi siingii aseee
Hii inaitwa jaza ujazwe sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila nmb mwanjelwa wanawake ma teller wezi balaaa. Yaani hawamwibii anayetoa laki tatu au tano nane wanadeal na anayetoa hela milioni moja na zaidi wakijua wazi hutahangaika kuhesabu pale kwamba utajichoresha. Wanakuchomolea elfu kumi tu basi.
Nimelizwa mara mbili jamani wafanyakazi wa benki mateller muwe na huruma hizo ni laana tu msiwe na tamaa na hela zetu.
Nmb mwanjelwa ni mojawapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom