Kuna vitu nilienda kulipia manispaa ya kinondoni, ss ndani mule kuna crdb, basi nikakaa foleni wee kuja kutahamki kumbe system imegoma transfer hazifanyiki basi huyooo kwa uzoefu wangu mdogo nikaenda kwa wahasibu nilipie kwa cash, wakanijibu kistaarabu kwamba hawawezi kupokea cash mpaka bank wawataarifu, nikarudi bank nikaingia na kumwambia 'bi teller', waambieni basi kule watupokelee cash...weweee alivyonijibu kwa nyodo na dharau eti 'nani kakupa ruhusa kuenda kule'...mama mama mama wee kilichomkuta naona aliniota usiku, nilimbadilikia ghafla nilimfokea km mbwa nikamwambia hela yangu ndo inakuweka hapa so uwe na adabu nikampaka vzr sana alinywea km mchicha uliochemshwa!