Vituko ndani ya JamiiForums

Vituko ndani ya JamiiForums

Ewaaaaa hivyo hivyo au jaman wanaume wenzangu naomba mnisaidie shemeji yenu analalamika nawahi haraka kukojoa khaaaaa watu wanayaweza ndio ya huyo mkaka dada tena me nilikuwa naelewana nae sababu ya thread zake anazoleta za mastory sasa hivi nabaki kumshangaa tu kuna siku nilimquote kwahiyo umeshabadirika jinsia umeshakuwa mwanamke tena hajanijibu nikamwambia ni jf pekee wanaume wanabadirika jinsia tokana na mazingira
Hahaha na wengine wanabadilika jinsia kutokana na post,post nyingine utamkuta ni mwanamke,ukienda nyingine ni mwanaume
Bora yule anaejiitaga sexless
 
Yaan mjukuu wa chifu ananishangaza sana kipindi yupo mwanaume alikuwa mshkaji wangu sana nilikuwa nafatilia sana thread zake toka awe mwanamke ushkaji umeisha hata nikimuuliza kwahiyo umebadilika jinsia hanijibu kabisa
Jamaa alikua ana mastori ya kibabe sanah, nashangaa siku hizi au wamemnaniiii
 
Ila member's wa humu uongo walionao sijui hata kama shetani anawahitaji!!!

Kuna mwingine alileta uzi hapa akidai amemaliza masomo yake nchini China mda kurudi nyumbani Tz umefika akadai a nahitaji binti wa kula naye bata hapa bongo!!!

Kurudi kufatilia nyuzi zake za nyuma miezi michache alisema anaishi dar mazense tena alileta kisa cha yeye na mke wake, nikajiuliza huu uongo ni kwa faida ya nani!!!!!!
Kuna mtu aliwahi sema husband material ni wanajeshi sasa sijui yule braza ni Mjeda?
 
Back
Top Bottom