dripu
JF-Expert Member
- Jan 30, 2017
- 1,310
- 1,141
Najua mko powah wote.
Moja kwa moja niende kwenye kastore kangu nilipokuwa mdogo.
Mimi nakumbuka nilipokuwa mdogo mgeni akija nyumbani ilibidi wawe wananifungia chumbani maana wakimnunuria soda mgeni nilikuwa naenda jikoni nachukua kikombe na kuanza kuendesha kwenye meza huku simuangarii mgeni wala mama nakuwa busy na kuunguruma kama gari nikizunguka meza.
Ila mama jicho analonikata na kuanza kusema kacheze huko basi, sasa mimi ndio naigonga ile soda mpaka mwenyewe mgeni ananimiinia soda nasepa zangu ila kuna wageni wengine noma kweli walikuwa wanajikausha mpaka wananinunulia soda yangu kimbembe mgeni akiondoka mama alikuwa ananichapa hatari.
Sijui nyie vituko vyenu vilikuwa vya aina gani?