Vituko vya kwenye daladala

Vituko vya kwenye daladala

The Initiator huru

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
1,993
Reaction score
2,635
Kama wewe ni mtumiaji wa usafiri wa daladala, pasipo na shaka umewahi kukutana na vituko kadha wa kadha vya baadhi ya abiria, makondakta au madereva. Embu kila mtu aweke vituko alivyowahi kuvishuhudia.
mimi vyangu ni hivi vifuatavyo.

1. Mimi niliwahi shuhudia kondakta akilumbana na mama mmoja, tangu mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari, mama alikua na ujasiri sana kwani pamoja na ukorofi wa kondakta ilibidi awe mpole. Kwa tafsiri ya haraka haraka mama yule ni kama ana uwezo wa kutumia nguvu za giza (kurog) kwani mara nyingi alitoa vitisho juu ya hilo, hii ilipelekea abiria wote kukaa kimya pasipo kuingilia ugomvi hata pale konda alivyokunjwa shati abiria waliishia kucheka tuu .

2. Mdada kunisukumia makalio yake makusudi
-Kuna siku nimepanda daladala nimesimama baada ya safari kidogo gari ikapakia tena abiria alikua ni mwanadada mrembo tuu na mwenye makalio ya wastani. Mara akasimama mbele yangu cha ajabu alikuwa akijitahidi sana kunibana na makalio yake licha ya mimi kuyakwepa mara kwa mara
Ewe mdau embu tupia visa vyako........................
 
Kuna siku nilipanda daladala sasa kondi akampitisha abiria kituo alichotaka kushuka,basi abiria alivyo mtemi akasema hii nauli sikupi kwa vile umenipitisha kituo nilichotaka kushuka,basi kituo kilichofata abiria wengine kushuka na yeye akashuka bila kulipa
 
Kuna siku tulikimbiza tax iliyotaka kutugonga tukiwa kwenye daladala. Tukaifukuzia had I buguruni mataa kutokea TOT lkn tulikuwa tunaenda kimanga.

Aisee kufika konda akafikia kuvunja site mirror za ile Gari bila kujua alikuwa anaendesha nani. Kucheki ni mjeda na family yake. Abilia wote tukala Kona tuksmuachia kesi konda. Kwa nini avunje site mirrors. Na sisi ndio tulimjaza kichwa
 
mimi konda kama hatoi tiketi akija namwambia nishakulipa
 
Kuna siku nimepanda daladala za kkoo kuja makumbusho via tandale uzuri....sasa jioni hua ni za kugombania...kuna mama alikosa seat, akamuomba msichana fulani sistaduu..."Naomba nikae mwanangu" yule msichana alimjibu bila kupepesa macho "siwezi kukupisha ukae"
Maneno aliyotamka yule mama mpaka leo siwezi kuyasahau, alimwambia yule msichana..."naomba upate ugonjwa mkubwa utakaokufanya ukae tu"...sio siri hata mimi niliogopa.
 
Tukio namba moja nadhan,liliwah kutokea nikiwa Tanga. Natoka bush huko, naenda Tanga town, kwa magara ya nauli buku tatu. Sasa tukiwa ktk ya vijiji vya pori ikaibuka ubishani ktk ya dada mmoja na kondakta.

Kimuonekana dada alikuwa na ka umbili kadogo tu, lakini anatema cheche balaaaa. Mabishano yalivyoendelea dada akasema, mnishushe sehem flan, yule konda akasema huko unakotaka hakuna kituo, Vituo vya kule pori viko mbalimbali kdgo. Konda alisem kumkomoa tu, maana hushusha na kupakia popote wanapopenda sema ni aliamua hivo tu

Dada alikuw na mizgo yake kafunga furush kwa kanga tu kama sikosei, yaan kafunga ki simplo simple tu, akasema aiseee NITAZIMA GARI SASA HIVI, SAFARI IISHE HAPA Konda akaendelea kubishana ,kuna watu wakamtonya, kuwa WATU WA KIJIJ HIKI, WASIKIE TU, KUNA MAFUNDI HAPO.
 
Kuna siku nimepanda daladala za kkoo kuja makumbusho via tandale uzuri....sasa jioni hua ni za kugombania...kuna mama alikosa seat, akamuomba msichana fulani sistaduu..."Naomba nikae mwanangu" yule msichana alimjibu bila kupepesa macho "siwezi kukupisha ukae"
Maneno aliyotamka yule mama mpaka leo siwezi kuyasahau, alimwambia yule msichana..."naomba upate ugonjwa mkubwa utakaokufanya ukae tu"...sio siri hata mimi niliogopa.
huyo mama nae mchawi tu, na laana ya hivyo wala haikubali.
 
Kuna siku nimepanda daladala za kkoo kuja makumbusho via tandale uzuri....sasa jioni hua ni za kugombania...kuna mama alikosa seat, akamuomba msichana fulani sistaduu..."Naomba nikae mwanangu" yule msichana alimjibu bila kupepesa macho "siwezi kukupisha ukae"
Maneno aliyotamka yule mama mpaka leo siwezi kuyasahau, alimwambia yule msichana..."naomba upate ugonjwa mkubwa utakaokufanya ukae tu"...sio siri hata mimi niliogopa.

khaaaaa
 
Mimi nilishuhudia mkaka kamalizia hamu yakke kwa mdada kwa daladala la kimara Tekeke (Coaster). Lilikuwa limejaza kweli kweli. Mara tukasikia dada akilalamika kuwa kachafuliwa. Yule yanki ghafla karudisha dude lake ghafla na kufunga zipu. Alivyozidi kuomba gari lisimamishwe,yule yanki akasema mwongo, mbona mimi hapa imepita wapi? Mbona mimi pakavu??.
Mimi kisa hicho kilinifikilisha zaidi kuwa kumbe vijana wakiwa na ukame wawezaa kumalizia hamu zao kwenye madaladala!!
 
Mbagala toangoma mida ya jioni kuelekea usiku.
Gari imejaa jamaa amekaa na mtoto wa kike siti ya nyuma dirishani. Akaanza kutongoza akitaka akamle kimasihara bila kuomb huduma moja kwa moja. Akamwambia tushuke wote utakaposhuka . Kumbe Dada alikuwa hajafika maelewano, tukaanza kusikia kelele "wee kaka vipiiii".
" Mbona sikujuii'
"Unataka ushuke na Mimi uniibie au"

Mara "mwiziiiiiiiii" jamani "mwiziiii"

Kaka ukome kunitisha "eti ushuke ninaposhukia".

Jamaa akaona isiwe soo akaomba kushukia njiani hapo misheni huku washika day tukimsindikiza kwa Maneno na nasaha za jinsi ya kuongea n mwanamke sio kushurutisha atakuja are kimasihara.

Naomba kuwasilisha
 
Kuna siku tulikimbiza tax iliyotaka kutugonga tukiwa kwenye daladala. Tukaifukuzia had I buguruni mataa kutokea TOT lkn tulikuwa tunaenda kimanga.

Aisee kufika konda akafikia kuvunja site mirror za ile Gari bila kujua alikuwa anaendesha nani. Kucheki ni mjeda na family yake. Abilia wote tukala Kona tuksmuachia kesi konda. Kwa nini avunje site mirrors. Na sisi ndio tulimjaza kichwa
😂😂😂😂😂😂. Umenichekesha sana
 
Wazee wa VIP wakiwa wanakuja ICC pale Arusha, sa kila baada ya dk kadhaa anatua mtu kia, mnazuiliwa, so siku jiyo kuawa na jam kinyama.
Baada ya wenye nchi zao kupita, tukaanza kupambana na jam letu, tukiwa tumefika mataa ya sanawari, kukawepo na gari ndogo mbele yetu, afu sie ndo kwa mat tuko nyuma yake. Taa zimeruhusu jamaa hatoki, sa dereva wetu alikuwa mtu wa stori sana. Pamoja na kuwa tulichukua muda mrefu kwa jam lakini hatukuwa bored maana ilikuwa ni bandika bandua na vichekesho balaa.
Sasa baada ya gari ya mbele kuzigua kutoka, mshikaji akashuka huku anatukana kaenda moaka kwenye gari na kwa namna alivyokuwa anasema kwa sauti, jamaa wa gari ya mbele alimsikia. Kufika si kawakuta wajeda. Mwana na mwili mkubwa alisukuma mwenyewe ile gari ya wajeda kuiweka pembeni
 
Back
Top Bottom