Vituko vya mama mjamzito

therocky

Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
13
Reaction score
8
Habari wana jamvi Kuna hili swala ambalo najua sio geni miongoni mwenu na pia nimelisikia kwa muda toka muda mrefu achilia mbali kulishuhudia.

Ni kuhusu mama mjamzito anapopata tu hiyo mimba basi anakuwa na tabia tofauti na alizokuwa nazo awali, mathalani kupenda chakula cha aina fulani au kuchukia kitu au vyakula fulani(ambavyo kabla alivipenda sana) na mambo mengine mengi.

Sasa concern yangu hapa ni kuwa mimi mke wangu wiki hii anatimiza miezi mitatu ya ujauzito wake(ni wa kwanza) lakini mpaka sasa simuoni kama kawa na tabia yoyote mpya na pia sioni kama kabadili sana vyakula alivyokuwa anakula zaidi tu ya kusema anajisikia uchovu wa hapa na pale na kulala sana na kichefuchefu kiasi.

Sasa kwa nini sioni hizo tabia au vituko hivyo? Au kuna miezi kadhaa akifikia ndio huwa hivyo? Naombeni msaada hapo, kwa ma-daktari au wenye uzoefu na haya mambo.

Asanteni.
 
mshukuru Mungu.....
 
Huo uchovu, kulala na kichefuchefu ndio utofauti wake, sio wote wanaweza kuchagua vyakula na pia sio wote wanaoweza kulala, kuchoka, kupata kichefuchefu, kutapika ama kutema mate. Hivyo km mkeo hachagui kuna anaechagua. Na kila mimba ina vituko vyake...
 
Asante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…