Vituko vya Mike Tyson

Roger Sterling

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2015
Posts
13,012
Reaction score
23,633
Moja kati mabondia bora kabisa kuwahi kutokea. Binafsi huwa navutiwa sana na vituko vyake enzi hiyo. Vilivyonivutia sana ni hivi...

Kwa mujibu wa Fat Joe. Siku moja Joe na Big Pun walibananishwa nje ya club (The Tunnel) na bouncers kama 8 hivi wakitaka kuwachapa baada ya kurushiana maneno. Enzi hiyo Joe na Pun ni mijitu ya miraba 16, na walikuwa na uwezo wa kupambana, ila walikuwa heavily outnumbered na wale bouncers, na mijamaa iko 7ft huko, so ikabidi wawe wapole ila too late.

Ghafla Iron Mike katokea, "wa'thup Joe and Pun! I got your back" (not quite sure that's what he said tho). Tyson akavua viatu, akaanza kuwakimbiza wale bouncers huku wakiwaomba kina Joe wawaombee msamaha kwa Tyson. Tunaongelea bouncers 8 wanamkimbia Mike. Joe na Pun walibaki kucheka na kushukuru miungu yao kwa kuepuka kipigo.

Story ya Ed Lover. Ed siku moja anaingia zake club moja, Manhattan. Akakutana na Mike anatoka nje. Mike akamuambia hiyo club hakuna issue, so wanaelekea club ingine in Queens, na Ed awafuate.

Ed akaacha gari yake pale club, akaingia kwenye msafara wa Tyson. Kufika club, bouncer akawachomolea kuingia sababu kulikuwa na dress code. Ilibidi mmiliki aitwe, ndio wakaingia.

Baada ya kula bata zito, muda wa kwenda home sasa Ed anamwambia Tyson ampe mtu amrudishe Manhattan alipoacha gari yake. Tyson akamwambia hapa wote tumechoka, akamuachia Bentley aliyokuwa anaendesha yeye, 450k worth.

So Ed akaenda home kwa mama ake kulala, akitegemea Tyson atamcheki kesho yake ili arudishe gari. Wiki ikapita kimya, wiki ya 2, mpaka mwezi mzima ndio manager wa Tyson anamcheki Ed kumuuliza kama ana gari yoyote ya Mike.

Ed akawapa address, wakaifuata gari. 15 years later, Ed anakutana na Tyson Las Vegas. Katika stori, Tyson anamwambia Ed kuwa ile Bentley alimuachia mazima, manager wake tu alipatwa na wivu ndio akamyang'anya.

Jamie Foxx's story. Wakati Jamie ndio anaanza ku-blow up, moja kati ya jokes zilizokuwa zinampa shangwe la kutosha ni ya kumuhusu Tyson. So siku moja anapiga show, watu wanakubali balaa, kufika kwa joke ya Mike...watu wote kimya, hakuna anayecheka. Kumbe mtu mzima yupo ukumbini mule, Jamie akaishiwa pozi kabisa. Long story short, Tyson alimwambia to tell the joke, but it better be funny.

Comedian Godfrey's. G siku moja yuko out and about, akakutana na Tyson akiwa dame ambaye jamaa anamjua. Yule dame akamsalimia mchizi, mchizi akamkana dame kuwa hamjui wala hajawahi kumuona maisha yake yote. Usifanye mchezo.

Ziko nyingi sana, ila hizo zilinivutia zaidi.
 
Ile aliyomvunja taya mwandishi wa habari je ?
 
Ile aliyomvunja taya mwandishi wa habari je ?
Haaaaaahaaaaa ilikuwa airport ile siku naoamgalia nilicheka maana Mike alikuwa anaenda paparazi yupo na yy kila akikata nae yupo nyuma basi ile anamrudia nikaona hii video vp mbona haitulii kumbe ndio vuruma Mike kakiwasha baada ya km sekunde 20 hv naona damu upande wangu wa kushoto wa camera nikaona dah...tyr tena mtu kavunjika taya!
 
So Interested. OP please shusha nondo zaidi za Mike If possible

One time Mike kakutana na baadhi ya members wa Ruff Rhyders red carpet, Sheek, Jadakiss, Ghost, na Eve kati yao. Mike akawa anamzingua Eve (harassment kiaina), manzi anawaangalia kina Jada wanamsaidia vipi. Jamaa wote (about 6 dudes deep) wakajikausha Eve apambane tu na hali yake. Hakuna aliyekuwa na ujasiri wa kumuambia Mike atulie.


The other time mtu mzima yuko gym anapiga tizi. Kuangalia kwenye vioo, anajiona kibonge and he doesn't like it. Akavunja vioo vyote gym. Mmiliki akazuga kama haoni, akajipa shughuli counter. Anyway, Tyson alivyomaliza akam-hug jamaa na akamtoa kiaina, akasepa zake. Ilikuwa Miami.
 
U made day!!!.
 
pesa nyingi na madawa vilimfanya awe kama chizi
sio sifa kuita vituko hasa kama hiko cha Bentley..ndo maana
Tyson hajui hadi leo alitumia vipi utajiri wa zaidi ya dolla milioni 300
akafilisika

ni hadithi za kusikitisha jinsi alivyozungukwa na 'wezi' waliojifanya washkaji


Siku mojaTyson alisimulia alikuwa akitaka watu waende kumfulia nguo
watu wanapigana nguo kugombea nguo zake wakafue
baadae ndo alikuja kugundua kumbe alikuwa anaacha pesa nyingi hadi dollar elfu 30
kwenye nguo ndo kilichofanya watu wapiganie nguo zake
alipofilisika wote wakamkimbia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…