Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Mada ya Mfahamu James Ngomero: Bingwa mtuhumiwa wa zile maiti 11 za watoto hospitali ya Mwananyamala imenikutanisha na watu wengi ambao kwa namna moja ama nyingine tunaweza kuwa tunafahamiana kabisa...

Si hilo tu bali nimegundua sehemu kubwa wanaJF Dar wengi ni wakazi wa Mwananyamala/Kinondoni katika ujumla wake...

Kuishi Mwananyamala pekee ni chuo tosha... Ikiwapendeza kwa uwingi wetu tunaweza kuwa na huu uzi wa vituko vya Mwananyamala mtaa kwa mtaa... Naamini kama umeishi Mwananyamala hutokosa cha kusimulia.

1. Madawa ya kulevya: Mwananyamala eneo lote la Mwananyamala A ni kituo na kitovu kikubwa cha madawa ya kulevya kuanzia wauzaji mapusha mpaka watumiaji... Hospital ya mwananyamala ina kituo cha kutoa tiba kwa mateja na nadhani ndio kituo kikubwa zaidi Tanzania.

2. Hospital ya mwananyamala: Ndio hospital maarufu zaidi yenye vituko na kashfa nyingi... Kuanzia kutoa mimba, kashfa ya vichanga 11, wizi wa maiti, rushwa... Maiti iliyofumuliwa na kutolewa madawa na madaktari kuiba hayo madawa,... Nk nk.

3. Matapeli: Hapo ndio kwake.. Mitaa maarufu ikiwa ni kuanzia kwa Kopa, A mpaka karibu na Kinondoni B, wale matapeli maarufu mmoja akijulikana kama doctor... Wale matapeli kiboko wa Jerry Muro, bar yao kubwa ilikuwa nyuma ya hospital ya Mwananyamala.

4. Ofisi na kampuni za mifukoni: Eneo lote la Kinondoni Mkwajuni mpaka Biafra ni hatari kwa shughuli hizo.. Utataka nini ukose.. Mihuri ya siri? Nyaraka za serikali? Mikataba mbalimbali, nyaraka za kusafisha mizigo.. Pesa bandia, madini bandia.. Kila kitu hukosi hapo. Mitaa hiyo ni maarufu kwa madaktari feki, Wanausalama, polisi, wanajeshi mahakimu, wanasheria, wabunge hata mawaziri nk.

5. Machangudoa, wasagaji, mashoga, Mario nk... Mtaa wa wibu ndio kama kitovu cha mashoga.. Ukiwasikia kina anti abuu, anti Ali hiyo ndio ilikuwa mitaa yao.. Habari za Machangudoa na wasagaji zinajulikana wazi.. Kinondoni na Mwananyamala ndio headquarters.

6. Wezi, vibaka majambazi, wakora nao wako: Ukisikia roba za mbao na watu wanaitwa mbavu Mwananyamala ndio kwao.

7. Wachawi wanga na waganga Wamo pia.. Mwananyamala kuna military base kubwa sana/KILINGE ya wachawi.... Lile anga limechafuka.

8. Wasanii wanamuziki wa aina zote: Bongo movies, Taarab, na kadhali kaliba yote hii kwa sehemu kubwa chimbuko ni Mwananyamala.

9. Wahamiaji haramu: Wakongo, Wamalawi, Wakenya, Waganda, Warundi nk... Sehemu kubwa wamejazana Mwananyamala.

Yako mengi ya kuandika kuhusu Mwananyamala siwezi kuyamaliza yote... Mengine yataandikwa na kusimuliwa na WanaJF - Mwananyamala Wing...
 
Nilishawahi kupita mitaa hiyo kwa miguu tena usiku mara kadhaa. Kuanzia Studio, Hospitali, Kwa Mama Zakaria, Ujiji, Kwa Kopa na sikuwahi kukabwa. Labda nilikuwa na malaika mlinzi.

Ila pale Mwananyamala A na kwa Kopa, Ujiji kuna sura si za Amani kabisa
 
Nilishawahi kupita mitaa hiyo kwa miguu tena usiku mara kadhaa. Kuanzia Studio, Hospitali, Kwa Mama Zakaria, Ujiji, Kwa Kopa na sikuwahi kukabwa. Labda nilikuwa na malaika mlinzi.

Ila pale Mwananyamala A na kwa Kopa, Ujiji kuna sura si za Amani kabisa
Ungepita kipindi hiko baba.
Sasa hivi wakabaji wote wameshakufa na wezi wengi wanaendesha boda boda
 
Kuna biashara inaendelea pale Minazini kuna nyumba imejengwa km madarasa ya shule (jina maarufu kwa wahaya).

Kipindi kile bao moja ilikuwa 1500, kulala 5000 mda wa biashara ni saa 7 mchana mpaka midnite. Vile vyumba vina milango miwili yanii unaingia mbele unatokea nyuma..

Wanaojiuza unawakuta wamekaa mlangoni pale chini mteja akija hakuna ata salamu ni speed tu ndani, kuna wamasai pale wao ni km walinzi wa ile biashara ukizingua kulipa wanakupa kichapo. Wateja wengine walikuwa wanakwenda kutolewa ndani ya room unakuta mteja amelipa 1500 ya mwendo mmoja yeye anaunganisha basi anaitwa mmasai fasta na bakora zake....

Pia hawa wamasai unakuta analipwa elfu 60 kwa mwezi ila mwisho wa mwezi anaambulia elfu 8 au 10 nyingne zote anakuwa anapewa huduma sana sana za buku 5 zile za kulala usk...HAPO ni MINAZINI.
 
Back
Top Bottom