Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Mkuu mbona unapenda utata kausha bhana
 
Mkuu mbona unapenda utata kausha bhana
Mkuu njoo PM bhana nimekucheck tuyajenge...then hao watu wengine achana nao awana madhara wana stress zao tu Topic ya ngomero ipo sehem nyingne...pia hakauna sehem ata moja mtu yoyote aliyesema amemkuta james anaua zaid ni tetesi na maneno yake akishalewa hizo issue za kuchimba makaburi zipo na anafanya kweli issue ya kuifadhi maiti za vichanga kinyume na taratibu kwel alifanya na pia polis alipelekwa sie sio mahakama wala atujui kwanini yupo uraiani mpka leo..hakuna mwenye evidence kuwa alikuwa anakula nyama ya mtu, anachinja watu n.k
 
Kombe la Dunia Mwaka 199O
Mwananyamala nzima..
TV tulikuwa tunaangalia kwa Mzee Tabu Jumanne Mangala..
alikuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza...
Lazima Uoge ndo uingie ukacheki Game ndani
Tena TV ilikuwa inawekwa nje uani.....
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
nimekaa sana Manjunju kwa mjeda mmoja, pia nimekaa Ujiji pale mahakama ya simu, rafiki yangu aliwahi kuishi kisiwani hapo Muigizaji TEA nae alikuwa anakaa pande hizo kwa mama mmoja Mkinga aliyemgeuza mumewe Ndondocha wanadai alikuwa mchafu sana huyo TEA haipiti wiki Mama mwenye nyumba hawajakwaruzana nae, Pale Kisiwani Bangi inavutwa hadharani, Pande za Ujiji madirisha karibu yote lazima ukute yamekatwa watu wanaweza vutia bangi dirishani kwako na huwezi wafanya chochote, kwa wale wapenda urahisi soko la mwananyamala ndio lina bei chee ya mchele, maharage na mahitaji mengine ya kunyumba
 

Mkuu nafuatilia sana comment zako [emoji24], nacheka kishenzi, unaonekana mtoto wa kihuni wa Mwananyamala uliyestaarabika ambae unaijua kiundani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…