Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

CC: katibu wa chama cha walipa kodi wakubwa Tanzania ndugu mrangi Mzee wa OVA...!
Mshana Jr mochwari hpo mwananyamala nna kisa fulani,ilikuwa miaka 99,98
Enzi hizo nataka kusafiri sina hela mara paap
Kuna dili tukaletewa hilo dili sasa mochwari
Ilikuwa lazima ihusike😂😂
Nakumbuka hilo dili ------- na baharia moja wa zamani anaitwa bozen deki
Kulikuwa na mkomoro mmoja alikaa sana bongo
Sasa huyo mkomoro kumbe aliwapiga wakomoro wenzake,sasa baada ya kufatiliwa sana kuhusu madeni bongo na kwao
Ilibd mkomoro mbongo atengenezewe mchongo kama kavuta...
Hapo watu tushaaidiwa 1.5mln
Ikafanyika mchongo ili jamaa aingizwe mochwr
Zugazuga jzz band,watafutwe jamaa waende uona mwili wa jamaa kama kavuta
Miaka ile mochwr alikuwepo mzee nani
Tukqmsomesha sana akaelewa,
Aise yule mkomoro kauzu aliingia mochwr
Jamaa wakatafutwa wakaja uona mwili wakakubali 😂😂😂
Wakampotezea jamaa
Jamaa alikuja toka hakukaa sana bongo akaenda ufaransa huko ndiko akaja kufa kiukwelikweli
😂😂😂

Ova
 
Mimi bwana nilipata dili ya maiti.. Niwapelekee kurasini baharini.. Mimi badala ya maiti nikaenda kariakoo nikanunua mdoli mkubwa ile ya kutundikia nguo .. Kisha nikaufanyia featuring ya sanda marashi nk
Kumbe jamaa wananifuatilia .. Nikapeleka mzoga wangu feki baharini wakafanya yao.. Kisha nikapewa kibunda cha 3M na mzoga niurudishe mochwari.. Kufika home na fuko langu la 3M jamaa wakanipigia simu kwamba nisihangaike kuhesabu zile pesa ni famba.. Na walifanya hivyo kwakuwa niliwapelekea mzoga famba[emoji24][emoji24][emoji24][emoji31][emoji31][emoji31][emoji31][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hahaha...ile hela tuliyopewa si nkasafiri ilikuwa 99 hivi nlipofika dizonga nakumbuka
Tulikabwa,pigwa loba
Hela ile haikuwa na baraka tulipata kidhuluma
Tukaipoteza kidhuluma😂😂😂

Ova
 
So yalikuwa haya makaburi ya kwakopa?
Ndiyo hayo hayo
Makaburi yalikuwa yanavituko sana hayo
Tushawahi kufanya mpango wa kuhamisha
Mwili wa mzee mmja hivi alizikagwa,mtoto
Wake kwa sababu hakuwepo kwenye mazishi
Alikuwa ulaya aliporudi bongo akaniambia
Mwanangu lazima baba tumfukue pale tukamzike tena makaburi ya kinondoni
Huyo mtoto wake alikuwa njema alafu ulaya kitambo sana ahh tulifanya process,msiba ukaanza up upya akazikwa kinondoni

Ova
 
Teh teh haya maisha
Mshana Jr itabidi sasa
Tuandike kitabu tuuzee😂😂😂

Ova
 
Hahaha...ile hela tuliyopewa si nkasafiri ilikuwa 99 hivi nlipofika dizonga nakumbuka
Tulikabwa,pigwa loba
Hela ile haikuwa na baraka tulipata kidhuluma
Tukaipoteza kidhuluma[emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
Hahaha[emoji23] hizi pesa nadhani huwa zina maruhani
 
Hivi unamjua Rashid Mandanje?
Nilikuwa nakaa nyumba ya jirani nao huyo mwamba, hahahaa kila siku wajomba hapo maskani nilikuwa dogo janja enzi hizo, huyu jamaa kanifundisha ngumi jiwe, yaani hata kama uko na mwili tofali ukizibuliwa lazima channels zi scramble!..A kwa mwinyijuma CCM pale kwa pembeni.

Hawa kina Ndanje walikuwa watatu km sijakosea na ndugu zake...
 
Acha utani
Emb endeleza story
 
Kidogo huku kwetu Mwanza ,Kirumba inafuata nyayo za Mwananyamala
 
Na vp kile kisa yule baharia alizikagwa makaburi ya kopa pale na macheni ya dhahabu
Usiku wahuni wakaja kumfukua unakmbka kisa kile Mshana Jr

Ova
Huyo jamaa alikuwa anaitwa MZEE MBAGA ni maarufu sana mpk mtaa anaoishi ukawa unaitwa kwa jina lake mpk leo mtu wa mwananyamala ukimuambia naenda mitaa ya kwa mzee MBAGA anakuelewa faster
nyumba yake pembezoni kuna TRANSFOMA na illikuwa inatazamana na maskani ya timu ya SWAZI INTER kwenye uwanja wa MAALIM BOFU
huyo mzee alikuwa mtata mtaani tulikuwa tunaiogopa nyumba yake kishezi yaan ukipita unamuona kwa ndani getini amekaa getini anakutazama kwa macho makali

mwanae aliporudi ULAYA alikuta kaburi la mshua wake juu kuna matakataka limekuwa dampo kibao mixer wanauza mikaa
ndo akafanya utaratibu wa kuhamisha mabaki ila sijajua kama alifanikiwa au vipi mana miaka fulani ya nyuma nilikuwa nikipita nilikuwa nalikuta lile kaburi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…