Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Mada ya Mfahamu James Ngomero: Bingwa mtuhumiwa wa zile maiti 11 za watoto hospitali ya Mwananyamala imenikutanisha na watu wengi ambao kwa namna moja ama nyingine tunaweza kuwa tunafahamiana kabisa...

Si hilo tu bali nimegundua sehemu kubwa wanaJF Dar wengi ni wakazi wa Mwananyamala/Kinondoni katika ujumla wake...

Kuishi Mwananyamala pekee ni chuo tosha... Ikiwapendeza kwa uwingi wetu tunaweza kuwa na huu uzi wa vituko vya Mwananyamala mtaa kwa mtaa... Naamini kama umeishi Mwananyamala hutokosa cha kusimulia.

1. Madawa ya kulevya: Mwananyamala eneo lote la Mwananyamala A ni kituo na kitovu kikubwa cha madawa ya kulevya kuanzia wauzaji mapusha mpaka watumiaji... Hospital ya mwananyamala ina kituo cha kutoa tiba kwa mateja na nadhani ndio kituo kikubwa zaidi Tanzania.

2. Hospital ya mwananyamala: Ndio hospital maarufu zaidi yenye vituko na kashfa nyingi... Kuanzia kutoa mimba, kashfa ya vichanga 11, wizi wa maiti, rushwa... Maiti iliyofumuliwa na kutolewa madawa na madaktari kuiba hayo madawa,... Nk nk.

3. Matapeli: Hapo ndio kwake.. Mitaa maarufu ikiwa ni kuanzia kwa Kopa, A mpaka karibu na Kinondoni B, wale matapeli maarufu mmoja akijulikana kama doctor... Wale matapeli kiboko wa Jerry Muro, bar yao kubwa ilikuwa nyuma ya hospital ya Mwananyamala.

4. Ofisi na kampuni za mifukoni: Eneo lote la Kinondoni Mkwajuni mpaka Biafra ni hatari kwa shughuli hizo.. Utataka nini ukose.. Mihuri ya siri? Nyaraka za serikali? Mikataba mbalimbali, nyaraka za kusafisha mizigo.. Pesa bandia, madini bandia.. Kila kitu hukosi hapo. Mitaa hiyo ni maarufu kwa madaktari feki, Wanausalama, polisi, wanajeshi mahakimu, wanasheria, wabunge hata mawaziri nk.

5. Machangudoa, wasagaji, mashoga, Mario nk... Mtaa wa wibu ndio kama kitovu cha mashoga.. Ukiwasikia kina anti abuu, anti Ali hiyo ndio ilikuwa mitaa yao.. Habari za Machangudoa na wasagaji zinajulikana wazi.. Kinondoni na Mwananyamala ndio headquarters.

6. Wezi, vibaka majambazi, wakora nao wako: Ukisikia roba za mbao na watu wanaitwa mbavu Mwananyamala ndio kwao.

7. Wachawi wanga na waganga Wamo pia.. Mwananyamala kuna military base kubwa sana/KILINGE ya wachawi.... Lile anga limechafuka.

8. Wasanii wanamuziki wa aina zote: Bongo movies, Taarab, na kadhali kaliba yote hii kwa sehemu kubwa chimbuko ni Mwananyamala.

9. Wahamiaji haramu: Wakongo, Wamalawi, Wakenya, Waganda, Warundi nk... Sehemu kubwa wamejazana Mwananyamala.

Yako mengi ya kuandika kuhusu Mwananyamala siwezi kuyamaliza yote... Mengine yataandikwa na kusimuliwa na WanaJF - Mwananyamala Wing...
Msisiri B Shule ya msingi pale ndipo panaitwa "mbuzi kagoma kwenda" wanawake wanachota maji, anavutwa darasani anapigwa chuma mchicha ndani ya dakika 5 anarudi kwa mumewe na haitakaa ifahamike, hufanyika nyakati za jioni.
 
Ndio mji na sehemu pekee Tanzania iliyokuwa mjini tokea kitambo toka 1940 uko mwananyamala ni town kumechangamka watu kibao mpaka leo mwananyamala town,town kitambo since way way back...
Kuna ramani niliiona ya wakoloni wajerumani ya dar es salaam ikionesha miji mbalimbali dar ikiwemo mwananyamala,upanga,kariakoo na masaki
 
Lake Mwananyamara (lake) is located in Tanzania nearby to Mwananyamala, Makumbusho, and Mwananyamala. It is also nearby Tandale and Ndugumbi. The latitude of Lake Mwananyamara is -6.78333, and the longitude is 39.25 with the GPS coordinates of 06ยฐ 46โ€ฒ 59.98โ€ณ S and 39ยฐ 15โ€ฒ 00.00โ€ณ E.
 
Huu uzi wankumbusha mbaali sana ,mmezaliwa Mwananyamala,nimekulia tandale pale kwa Ally Maua sasa hivi eti Kijitonyama[emoji848]baadae tukahamia hapa mwanayamala ujiji Kona ya ile madrasa ya Shamsia na nyumba ya Julius Nyaisanga kwa mbele kidogo kuna msikiti ndo palikua uswazi hapo,nimekaa Kinondoni kule bwawani kwa Hanzuruni Mungula,enzi hizo kituo hakiiwti Biafra kinaitwa Hombos hotel au Kanisani

Ahsante kwa baba angu ,siku tuliyopangwa tukafundishwe kuvuta bangi wenzangu wananisubiri nje nkaitwa kwenda ndani nikapike wakanisubiri wakaona kimya wakasepa toka hapo wakanitenga wakaniambia Mimi mtoto wa baba!wale wadada wengine waliishia kua mateja tu.
Nashukuru kwa mzee kuhama pia maana I swear kule nisingesoma asehh!!

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Mwenyekiti wetu hajui kusoma na kuandika ukaanzishwa utata akasema anajua kuandika na kusoma.

Wakakutanishwa siku hiyo ya kumtest kama kweli anajua kusoma na kuandika akaambiwa andika Chama Cha Mapinduzi.

Akaandika Chama Ha Mapundusi

Mwandiko kama bata.

Kampeni za 2015 akawa ananadi sera nanukuu

"Vijana nipeni kura mimi na nyinyi hatuna ugomvi ndiyo maana mnapovuta bangi napajua ila sijawahi kuwaleta polisi, kama kuna yeyote kawahi kusumbuliwa na askari kisa bangi aseme"
[emoji2][emoji2][emoji23][emoji23][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] tembelea kwa mama Zakaria
Nimekukubali mzee baba,pale kwa mama Zakaria unashusha kibonde kile kama kauchochoro hivi[emoji28][emoji28][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]we nuksiii

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom