Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Mwenyekiti wetu hajui kusoma na kuandika ukaanzishwa utata akasema anajua kuandika na kusoma.

Wakakutanishwa siku hiyo ya kumtest kama kweli anajua kusoma na kuandika akaambiwa andika Chama Cha Mapinduzi.

Akaandika Chama Ha Mapundusi

Mwandiko kama bata.

Kampeni za 2015 akawa ananadi sera nanukuu

"Vijana nipeni kura mimi na nyinyi hatuna ugomvi ndiyo maana mnapovuta bangi napajua ila sijawahi kuwaleta polisi, kama kuna yeyote kawahi kusumbuliwa na askari kisa bangi aseme"
Dah,mkuu umenichekesha balaa hadi my kids hapa wananishangaa!
 
Ukiona mgonjwa wako amelazwa mwananyamala hospital hesabia amekufa


Kuna watu kama 5 huku mtaani vijana walilazwa hospitali ya mwananyamala na wakafa na wengi hufa karibia na alfajiri ,mpaka watu wakawa wanatania endapo mtu akitaka kwenda kutibiwa hospitali ya mwananyamala ..mie siwezi kwenda kutibiwa hospitali ile kama nikiwa mahututi


Sema madaktari wao wapo poa sana nimechonga vyeti vya ugonjwa feki vingi
Kiuhalisia kabisa ni kwamba ile hospital imejengwa juu ya makaburi na ni njia kuu ya mapito ya wachawi na kuna kilinge kikuu pale ndio maana hospital ile ni special case.. Imeshindikana
 
Kamanyola gesti karibu na Bakule... Ukiingia hapo hata ufanyeje lazima upigwe chabo... Nasikia zile chabo zinalipiwa...
[emoji23] [emoji3] [emoji23] wanaita deo lazima uliwe deo hapo gesti kamanyola ukiinuka tu kuelekea milango ya gesti aliyekuuzia room ndio anauza tena mchezo analipwa then anatoa sign kwa wazee wa deo room unayopewa socket ya taa na feni vipo direct yanii ukizima taa na feni inakuwa Off..ile upate upepo wa feni na taa iwe ON wazee wadeo wapo dirishani....hapo kamanyola pametoa mashoga wengi sana kule dirishani ktk chabo
 
[emoji23] [emoji3] [emoji23] wanaita deo lazima uliwe deo hapo gesti kamanyola ukiinuka tu kuelekea milango ya gesti aliyekuuzia room ndio anauza tena mchezo analipwa then anatoa sign kwa wazee wa deo room unayopewa socket ya taa na feni vipo direct yanii ukizima taa na feni inakuwa Off..ile upate upepo wa feni na taa iwe ON wazee wadeo wapo dirishani....hapo kamanyola pametoa mashoga wengi sana kule dirishani ktk chabo
Duu unaifahamu vema.. Sitaki kuuliza zaidi
 
Matokeo yalikuwaje mkuu?
Ngoja nikupe matukio ya siku ya uchaguzi halafu utasema mwenyewe unahisi matokeo yalikuaje.

Afisa mtendaji akagundulika kua anawapigisha kura wazee na vilema kwa kuwatikia CCM hata kama hawataki, kuna mlemavu wa urefu alisimamia visigino akakuta jamaa anatiki CCm akaanzisha utata Afisa akapigika askari wakaingilia.

Kuna mama alikutwa na chupa ya chai imejaa kura zilizokua zimetikiwa tayari.

Askari walikua wamejazana na magari ya maji ya kuwasha wakihimiza watu wasikae eneo hilo kabisa.

Wasimamizi na ambao walikua wanapanga tukio ni makada wa chama na mmoja ni mtoto wa mgombea.

Of course CCM tulishinda
 
Mi kimboka nilichukua demu, nikamwambia uwanja wa mauaji wapi, akasema nimfuate, ila moyoni nikawa najiuliza huku anakonipeleka kama kuna usalama, tukaingia gheto moja chafu chafu, yaani mashuka yana ramani ya nchi zote zilizopo duniani, mpaka sasa hivi sijajua zile ramani kama ni mikojo ya walevi au many ejaculations za masela..

Tukaanza mambo, mara demu anaanza kusema we msenge nini, fanya fasta niwahi kiwanja, daah, yaani mzuka wote ukaisha, maana nilikuwa sijazoea lugha kali kama za huyu chakalaa wa kike, yaani unanitukana katikati ya mchezo, maana anataka nifanye kama kuku kitu ambacho sijakizoea, ila kiukweli sikumaliza maana wazungu wote walighairi na kuamua kwenda kuendelea kuweka makazi kwenye korodani

Sitaisahau na sitamsahau huyu mpenzi aliyenipiga kibuti mpaka mzee mzima nikaamua kujitoa muhanga mitaa ya kimboka, maana kule mahala kunatisha mazee usiombe, halafu mbaya zaidi nilizama nikiwa nimevaa suti jezi la kazini, ila nahisi masela na wenyewe walikuwa hawanielewi ndio maana wakawa wananiangalia kwa macho ya wasiawasi, maana nilikuwa sifananii kabisa kuzama hayo maeneo, ila kunatisha, maana kule unaweza liwa supu ndugu zako wasione hata unyayo
 
Manyau nyau alikuja kuondoa uchawi kufika pale Ubaa Corner (Baa ipo Makaburini) akasema mbele anaona bahari tu hawezi kusogea mbele akarudi kwao, akakaa akaja tena, akafika sehemu ni maskani kuna gogo limewekwa hua tunakaa kupiga stori.

Akatoa jidude fulani hivi akasema huu ni ub00 kila aliyekaa hapa alikua anafir.wa ndiyo maana mtu akikaa hapa kuondoka hua hataki.

Yaani alichomaanisha ni kua vijana wote wa pande zile marinda yaliliwa na wachawi
Khaa...[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] aisee nimecheka hatari!!! Hebu hao waliokuwa wanakaa hapo watuambie walikuwa wanajisikiaje??...[emoji23] [emoji23]
 
Nimeishi na kusoma mwananyamala.Kuna mganga mmoja wa kienyeji alikuwa anaitwa profesa vulata (sijui yupo wapi nowadays).Kuna jirani yetu alienda na nduguze kupata tiba ktk clinic yake.Wakati tiba na manyanga yakiendelea,ghafla mpiga nyanga akashuka na dari puuuuu hadi chini alipokuwa mgonjwa na nduguze.Mgonjwa na nduguze walitoka mbio acha tu.
 
Wapi DJ Manga P?Alikuwa anatuburudisha pale Masai kipindi hiko Hakuna Club bali kuna vyumba vya kulala wageni na Bar halafu Manga P anakuja kila Alhamisi au Ijumaa kutuburudisha na oldies za 80s. Hii ndio ilianza kuvutia wateja hadi Club ikaanzishwa.

Kipindi hiko hapo opposite kuna kibanda choka mbaya ila kina michipsi na mishikaki mitamu na bei ya kutupa ukichanganya na miguu ya kuku.
 
Back
Top Bottom