Naamini kilichoandikwa siyo kazi ya RA, bali naamini ni kazi binafsi ya mhariri kilaza kwa jina la Deodatus Balile, akitaka kuyaiga yaliofanywa na Salva na timu yake wakati wa kampeni ya 2005 dhidi ya Dr.Salim.
Baada ya Salva kuyafanya aliyoyafanya, mambo yake yakawa safi, baada tuu ya mkulu kuingia magogoni, Salva huyo, akaula. Sasa huyu kilaza Balile anataka kuiga tembo ... kwa kujikomba komba kwa JK kwa staili ile ile akisubiri Salva apigwe ubalozini akiamini labda yeye ataitwa!.
Kwenye fani ya habari, jamani, hizi njaa zetu wakati mwingine zitatuua!. Hapa kwa wanafani, mheshimiwa sana Balile, amejidhalilisha japo nakizi alichoandika sio majungu, wala hakutunga bali ni hard facts ila tatizo ni jinsi alivyoziwasilisha ikiwemo kutaka kulisha watu maneno.
Credibility ya Magazeti ya Mtanzania, ilishashuka zamani wanachofanya sasa ni kuimalizia tuu, naomba mimi niwe wa kwanza kuitabiria Habari Corp kifo cha mende mara tuu baada ya uchaguzi kwa sababu wanamdhania RA ataendelea kubebwa ili na yeye awabebe, no way,
kwa vile itakuwa ndio term ya mwisho kwa mborongaji, atahakikisha haborongi tena ili aache legacy, with nothing to loose, wasitegemee tena kama atawategemea wapambe wa style ya RA, atawatosa ili angalau wasizidi kumchafua.
Kwa wale wenye mapenzi mema na Dr. Slaa, this is not a big deal, he is human, tit for tat za aina hii ni too low kwa mapambano ya kupigania maslahi ya taifa.
Balile ya timu yenu, endelezeni kazi nzuri mnayoifanya, your days are numbered na malipo ni hapa hapa duniani!.