Vituko vya sekondari 1990s,wahenga tukutane hapa

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,117
Reaction score
1,966
Tujikumbushe vituko ambavyo tulivifanya kipindi tunasoma sekondari 1990s.

Kuwakaribisha form one kwa kipigo mabwenini,ilikuwa lazima form aliyekuwa akijiunga na secondary za bweni lazima alipata kipigo

Form one amewahi kulipa ada kwangu nikiwa form six,nikijifanya Mimi ni Mwl.

Kutongoza mademu ni kiingereza tu,na mkifunga shule ,vijana wa kiume wanaona raha kupiga stories na wanafunzi wa kike ambao nao walikuwa likizo pale mtaani.

Mkiwa kwenye group la watu,wale wa secondary ni kiingereza tu


Hakuna furaha kama siku umetumiwa barua kwa njia ya post,ikasomwa parade ulikuwa unaonekana bora sana kuliko wengine

Vijana ambao hawajaenda sekondari,haitatokea hata Siku moja akamtongoza binti aliyekuwa secondary, walikuwa wanawaogopa sana

Ongeza na mengine
 
Mtu aliyekuwa na viungo vya kuongeza kwenye mboga alionekana bora sana
 
Kutengeneza appetite hiyo inaitwa,mafuta vitunguu na dagaa. Welcome form one usiku mnazima taa sasa apo ndo wanachapika. Unampa shiling20 akalete sabuni sukari na chenji
 
Kutengeneza appetite hiyo inaitwa,mafuta vitunguu na dagaa. Welcome form one usiku mnazima taa sasa apo ndo wanachapika. Unampa shiling20 akalete sabuni sukari na chenji
[emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Kwa wale wa Azaboy, form I alikua akiwa mzembe tunamvua buti na kuchukua counterbook..pia tukienda kwenye michezo wao wanatangulia mbele..
 
Dah...asubuhi chai ya maziwa...mkate wenye jibini...Mayai...na juisi halisi....mchana...mazagazaga Mengi na mtindi juu...usiku ndiyo balaa.... Tuliosoma kabla ya Uhuru tulifaidi sana....
 
Kutengeneza appetite hiyo inaitwa,mafuta vitunguu na dagaa. Welcome form one usiku mnazima taa sasa apo ndo wanachapika. Unampa shiling20 akalete sabuni sukari na chenji
Hapo kwenye viungo nimetengeneza hiyo sana [emoji6][emoji23][emoji23]
 
Hakuna jipya . Mpaka leo watu wanafanya
Mkuu mpaka sasa, kuna wanafunzi wanatumiwa barua za posta,
Au vipi Siku hizi form one wanakula kichapo Siku aliyoripoti
Au anamwagiwa maji kitandani,ili asubuh akaanike godoro,ili wamcheke kuwa form one amekojoa kitandani[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] sidhani kama yapo
 
Sitasahau Siku boyfriend amenitumia barua....halafu ikapitia kwa headmistress,...akaisoma master parade...loh
 
Nakumbuka mwalimu wa Geography alikuwa anafundisha sifa za Jangwa. Akasema the whole area is BARE........!
Kule nyuma mwanafunzi akaropoka SIMBA!
Nilicheka sana baada ya kumuuliza ana maana gani. Akasema ni mchezaji wa Pamba FC ya Mwanza![emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Shikamoooni wooootee mliokua secondary kipindi hicho
 
Nafuatilia comment za wahenga

Shikamooni na nawaheshimu mnooooo

90 sekondari..aiseeeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…