Vituko vya utotoni

Vituko vya utotoni

GIRITA

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
4,432
Reaction score
5,864
Napenda kutoa salam kwa ndugu zangu humu jukwaani vijana kwa watu wazima.

Moja kwa moja kwenye mada...Maisha yana Mapito mengi sana.

Lakini Mimi nitawaletea vituko, nilivyowahi kuvifanya utotoni ambavyo mpaka sasa bado navikumbuka havijafutika kichwani kwangu na amini kila mmoja amewahi kupitia na kufanya mambo kulingana na akili ya utoto ilivyomtuma na yeye kuona yuko sahihi kabisa.

Kulingana na Mazingira niliyopitia katika makuzi yangu nitaeleza matukio machache au vituko nilivyovifanya utotoni mpaka Leo huwa nakumbuka nabaki kucheka peke YANGU.

~Tukio LA kwanza~
Ilikuwa miaka ya 2000 hivi tulikuwa tunaishi mkoa wa Mwanza maeneo ya iLuganzala karibu au jirani na kiwanda cha bia TBL..sasa nyumba tuliyokuwa tunaishi nyuma YAKE kulikuwa kuna njia ndogo watu wanapita kuelekea mnadani, sabasaba kununua mahitaji yao.

Kuna MTU alikuja nyumbani akaleta elfu kumi kipande akatupa watoto tukawa tunaichezea....ikawa zile siku za watu kwenda sabasaba tunakaa njiani na kile kipande cha elfu kumi... tunawategeshea watu wanaopita kwa kukifunika na, mchanga...halafu tunakaa pembeni.

MTU mzima anapita akiiona ile teni ilivyofunikwa na mchanga anaikanyaga taratibu na kiatu halafu anaikota kwa umakini watu wasimuone basi...ile akiinuka aondoke anaona ni kipande cha hela,sisi tunaanza, kumcheka...anapata hasira akitaka kuondoka nayo... tunaanza kulia kwa sauti kubwa mpaka anaamua kuitupa..tunaichukua tunaitegesha tena.

Tulikuwa tunawasumbua watu wazima sana mpaka tulipotaka kupigwa ndiyo tukaacha huo mchezo, na ule wakumwita MTU anayetembea halafu unamwambia umedondosha akigeuka mnacheka mnakimbia.

~Tukio LA pili~
Hii nilikuwa kama darasa LA NNE wilaya x,mkoa z..Mimi na mshikaji kwangu sana kipindi hicho alijukana kama HB...huyu alikuwa ananipiga tafu sana maisha ya shule...mkitoka mapumziko ananunua misosi mnakula na kusaza...kutokana na ushkaji kuzidi ikabidi tuunde kundi LA muziki Mimi na yeye kwa sababu nilipenda sanaa,muziki,kuchora,n.k

Tukawa tunafanya mashindano ya kurap
Pale skuli kila inapofika SAA NNE muda ya break...tunaenda nyuma ya madarasa tunaanza kushindana kurap...tulikuwa tunaandika hadi mashairi tunaya rap kwa ufasaha na ustadi mkubwa kama wasanii kweli,tulikuwa tukishindana na kundi LA jamaa wengine wikiongozwa E...zawadi kwa washindi ilikuwa ni Mapapai ya kuiva maana kulikuwa na mipapai kwenye eneo LA kanisa jirani na shule.

Sasa siku moja kulikuwa hakuna masomo wanafunzi wanacheza tu sikumbuki kulikuwa na tukio gani,tukaamua tufanye tour kila darasa tunaingia tunarap....tulianza darasa LA jirani ya darasa letu tukapiga rap yetu vizuri....kuingia darasa linalofuata mambo yakawa si mambo.

Tulikuwa tunashika kalamu mfano wa maiki tunaimbia sasa ile tu natoa maiki YANGU tuanze kazi Mimi na HB...akatokea jamaa flani aliyekuwa ananizidi kimwili sijui miaka maana nilikuwa mdogo mdogo, ile naanza kuimba nilikuwa mbele pale ubaoni wanafunzi wote wanatusikiliza...jamaa akaniambia unaimba nini wewe unanuka mdomo!!!...aisee nilipata hasira halafu ilikuwa mwezi wa ramadhani...hali ya mdomo kuwa tofauti ni kawaida kwa mfungaji nilimvuta jamaa nikamrukia na kichwa...ile kumuachia damu...anamwagika damu puani kama maji,hakuna aliye amini kwa udogo wangu kama ningeweza kumvujisha mchuzi yule bigy hadi maticha walibaki wanashangaa kama ni kweli au ni muvi.

Nikawa mpole sana kama nimenyeshewa na elnino...nikapelekwa ofisini nikatandikwa bakora nyingi sana.

Nikaambiwa nikamlete mzazi ampeleke yule jamaa hospitali, nikaenda home nikamwita faza ...kufika shule faza akanitetea akasema sipiganagi bila kuchokozwa, kwa hiyo bigy ndiyo mchokozi.

Alipoambiwa sababu akabaki anacheka ... .akaniambia nimpeleke jamaa hospitali akatibiwe nikampeleka akapata tiba...Ila baadae nikawa namuonea huruma Ila nikawa naogopeka pale skuli mpaka Leo sijawahi pigana tena.

Najua nimewachosha wakuu ni katika kubadilishana mawazo ili kufurahi na kuondoa stress za maisha karibu na wewe utupe Tukio lako enzi za utoto...huku ukisikiliza ngoma ya songa enzi za utoto.

Wasalaam G.R.T
 
Uzi wa utotoni huu hapa wakuu ndugu zangu!!!
 
Pamoja sana mkuu@baron de montesque
 
Haaahaaa!!! Umetisha mkuu baron.
 
Baada ya kusafisha viti vya sherehe tukatoka na kuanza kucheza mpira tukisubiri tupewe pilau kama mshahara wa kazi tuliofanya,tulikuwa watoto wa hapohapo mtaani na ilikuwa mida ya jioni.. baada ya kucheza na kucheza wee pilau haliji ikafika mida ya samoja jioni wageni wa sherehe wakaanza kuingia si tupo nje tunawacheki tu mpk tukaanza kumsema vibaya mama mwenye sherehe!😂
Ilivyokaribia mida ya saa mbili tumechoka na kila mmoja Sasa hapo anatakiwa asepe kwao pilau hakuna!
Ktk group tuliokuwepo kulikuwa na dogo yeye tulikuwa tunamzidi kidogo na kaka yake tulikuwa tunamuita mzimu!!
Hasira za kunyimwa pilau tukazihamishia kwa dogo,tukaanza kumwambia aende kwao maana kwao palikuwa ni mbali kidogo tofauti na sisi,dogo akawa hataki!! Akala mitama na makonzi akaanguka kwa pembeni kulikuwa na majani akawa analia!
Si tukaendelea na stori zetu ile punde kupita ghafla dogo akaamka halafu kabadili sauti yani sauti kana kwamba anataka kuuwa mtu huku kashikilia mawe!! Mweeee hapakukalika kutegemea na usiku ule watu tulichanja mbaliga kundi moja lilikimbilia upande mwengine na wengine tukakimbilia kwengine ambapo kulikuwa ndo nyumbani ninapokaa.. Sasa dogo alikuwa anatukimbiza huku akiendelea na zogo lake ambalo lilizidi kutuchanganya maana hapo unajua ukisimama tu jiwe plus na zile kelele zake plus kaka yake tunamuitaga mzimu😂😂 hofu ilikuwa juu ya hofu!!

Sasa nilipokaribia nyumbani,nilijua kabisa hapa ni nyumbani ila ilibidi nipapite😂 maana nilikuwa spidi ya 4G na ili niingie ndani ilibidi nipunguze spidi Kisha nifungue mlango nizame ndani jambo hilo niliona ni mchakato jiwe lingenikuta isitoshe kelele za yule dogo zilikuwa nazisikilizia hapo na hapo😂
Nikaliunga zaidi na zaidi!! Bahati nzuri tulifika kwenye nyumba moja kulikuwa hakuna mtu taa zimezimwa halafu kunamauwa ile tunataka kujificha tukasikia mwenzetu aliekuwa mwishoni anaangua kicheko Cha haja!!
Kumbe fala lile lilitufanyia mchezo dogo aliekuwa anatukimbiza alikuwa anatuogopa! Hivyo wakati anaanza kutukimbiza alitukimbiza kidogo tu so aliekuwa wa mwisho yeye ndo alijua kuwa dogo kaacha kutukimbiza na wakati huo watu tumeshachanganya balaa jamaa alichokifanya akapokea sauti ya dogo so sisi tukazani ni dogo bado yu nasi😂😂 fala yule alituweza wapuuzi wengine wakaanza kunishangaa ati nimepitiliza kwetu wkt mi nilipiga hesabu ya haraka nikaamua kuunga wala hata sikuwajibu nilikuwa nahema Kama mbweha kila mmoja alirudi kwao yuko hoi na pilau tulilikosa alieunga sauti ndie alieondoka na furaha
Godfrey popote ulipo jua we ni kenge 😂😂
 
hahhahahah, si ndio nimecheka maana eti mwaka 2000 akiwa mtoto, ili hali mie nilishakazwa, nimepigwa p.um.bu hadi zimenikifu. jahahahahahahahahah
Ohoohooo!!!da Atari sana...kwa hiyo wewe ni jimama?
Basis dondosha kituko chako cha enzi za kuvaa raizoni...na mokasee!
 
Sio jimama, sema "kumbe wewe ni sawa na mama yangu mzazi..."
Sie zamani hatukuwa na vituko kama nyie ujue.
hahahahahahaha
 
Baada ya kusafisha viti vya sherehe tukatoka na kuanza kucheza mpira tukisubiri tupewe pilau kama mshahara wa kazi tuliofanya,tulikuwa watoto wa hapohapo mtaani na ilikuwa mida ya jioni.. baada ya kucheza na kucheza wee pilau haliji ikafika mida ya samoja jioni wageni wa sherehe wakaanza kuingia si tupo nje tunawacheki tu mpk tukaanza kumsema vibaya mama mwenye sherehe!😂
Ilivyokaribia mida ya saa mbili tumechoka na kila mmoja Sasa hapo anatakiwa asepe kwao pilau hakuna!
Ktk group tuliokuwepo kulikuwa na dogo yeye tulikuwa tunamzidi kidogo na kaka yake tulikuwa tunamuita mzimu!!
Hasira za kunyimwa pilau tukazihamishia kwa dogo,tukaanza kumwambia aende kwao maana kwao palikuwa ni mbali kidogo tofauti na sisi,dogo akawa hataki!! Akala mitama na makonzi akaanguka kwa pembeni kulikuwa na majani akawa analia!
Si tukaendelea na stori zetu ile punde kupita ghafla dogo akaamka halafu kabadili sauti yani sauti kana kwamba anataka kuuwa mtu huku kashikilia mawe!! Mweeee hapakukalika kutegemea na usiku ule watu tulichanja mbaliga kundi moja lilikimbilia upande mwengine na wengine tukakimbilia kwengine ambapo kulikuwa ndo nyumbani ninapokaa.. Sasa dogo alikuwa anatukimbiza huku akiendelea na zogo lake ambalo lilizidi kutuchanganya maana hapo unajua ukisimama tu jiwe plus na zile kelele zake plus kaka yake tunamuitaga mzimu😂😂 hofu ilikuwa juu ya hofu!!

Sasa nilipokaribia nyumbani,nilijua kabisa hapa ni nyumbani ila ilibidi nipapite😂 maana nilikuwa spidi ya 4G na ili niingie ndani ilibidi nipunguze spidi Kisha nifungue mlango nizame ndani jambo hilo niliona ni mchakato jiwe lingenikuta isitoshe kelele za yule dogo zilikuwa nazisikilizia hapo na hapo😂
Nikaliunga zaidi na zaidi!! Bahati nzuri tulifika kwenye nyumba moja kulikuwa hakuna mtu taa zimezimwa halafu kunamauwa ile tunataka kujificha tukasikia mwenzetu aliekuwa mwishoni anaangua kicheko Cha haja!!
Kumbe fala lile lilitufanyia mchezo dogo aliekuwa anatukimbiza alikuwa anatuogopa! Hivyo wakati anaanza kutukimbiza alitukimbiza kidogo tu so aliekuwa wa mwisho yeye ndo alijua kuwa dogo kaacha kutukimbiza na wakati huo watu tumeshachanganya balaa jamaa alichokifanya akapokea sauti ya dogo so sisi tukazani ni dogo bado yu nasi😂😂 fala yule alituweza wapuuzi wengine wakaanza kunishangaa ati nimepitiliza kwetu wkt mi nilipiga hesabu ya haraka nikaamua kuunga wala hata sikuwajibu nilikuwa nahema Kama mbweha kila mmoja alirudi kwao yuko hoi na pilau tulilikosa alieunga sauti ndie alieondoka na furaha
Godfrey popote ulipo jua we ni kenge 😂😂
😀😀 utoto shida sana unapitia mambo kama yote ya ajabu👊
 
Sio jimama, sema "kumbe wewe ni sawa na mama yangu mzazi..."
Sie zamani hatukuwa na vituko kama nyie ujue.
hahahahahahaha
Inawezekana una umri sawa na Dada YANGU wakwanza...maza ni mkubwa sana.
Tupe tukio LA utoto wako...mbona kuna ma dingi wanatupaga vituko vyao vya uchalii umri wako mbele zaidi yako.
 
Baada ya kusafisha viti vya sherehe tukatoka na kuanza kucheza mpira tukisubiri tupewe pilau kama mshahara wa kazi tuliofanya,tulikuwa watoto wa hapohapo mtaani na ilikuwa mida ya jioni.. baada ya kucheza na kucheza wee pilau haliji ikafika mida ya samoja jioni wageni wa sherehe wakaanza kuingia si tupo nje tunawacheki tu mpk tukaanza kumsema vibaya mama mwenye sherehe!😂
Ilivyokaribia mida ya saa mbili tumechoka na kila mmoja Sasa hapo anatakiwa asepe kwao pilau hakuna!
Ktk group tuliokuwepo kulikuwa na dogo yeye tulikuwa tunamzidi kidogo na kaka yake tulikuwa tunamuita mzimu!!
Hasira za kunyimwa pilau tukazihamishia kwa dogo,tukaanza kumwambia aende kwao maana kwao palikuwa ni mbali kidogo tofauti na sisi,dogo akawa hataki!! Akala mitama na makonzi akaanguka kwa pembeni kulikuwa na majani akawa analia!
Si tukaendelea na stori zetu ile punde kupita ghafla dogo akaamka halafu kabadili sauti yani sauti kana kwamba anataka kuuwa mtu huku kashikilia mawe!! Mweeee hapakukalika kutegemea na usiku ule watu tulichanja mbaliga kundi moja lilikimbilia upande mwengine na wengine tukakimbilia kwengine ambapo kulikuwa ndo nyumbani ninapokaa.. Sasa dogo alikuwa anatukimbiza huku akiendelea na zogo lake ambalo lilizidi kutuchanganya maana hapo unajua ukisimama tu jiwe plus na zile kelele zake plus kaka yake tunamuitaga mzimu😂😂 hofu ilikuwa juu ya hofu!!

Sasa nilipokaribia nyumbani,nilijua kabisa hapa ni nyumbani ila ilibidi nipapite😂 maana nilikuwa spidi ya 4G na ili niingie ndani ilibidi nipunguze spidi Kisha nifungue mlango nizame ndani jambo hilo niliona ni mchakato jiwe lingenikuta isitoshe kelele za yule dogo zilikuwa nazisikilizia hapo na hapo😂
Nikaliunga zaidi na zaidi!! Bahati nzuri tulifika kwenye nyumba moja kulikuwa hakuna mtu taa zimezimwa halafu kunamauwa ile tunataka kujificha tukasikia mwenzetu aliekuwa mwishoni anaangua kicheko Cha haja!!
Kumbe fala lile lilitufanyia mchezo dogo aliekuwa anatukimbiza alikuwa anatuogopa! Hivyo wakati anaanza kutukimbiza alitukimbiza kidogo tu so aliekuwa wa mwisho yeye ndo alijua kuwa dogo kaacha kutukimbiza na wakati huo watu tumeshachanganya balaa jamaa alichokifanya akapokea sauti ya dogo so sisi tukazani ni dogo bado yu nasi😂😂 fala yule alituweza wapuuzi wengine wakaanza kunishangaa ati nimepitiliza kwetu wkt mi nilipiga hesabu ya haraka nikaamua kuunga wala hata sikuwajibu nilikuwa nahema Kama mbweha kila mmoja alirudi kwao yuko hoi na pilau tulilikosa alieunga sauti ndie alieondoka na furaha
Godfrey popote ulipo jua we ni kenge 😂😂
Unajikuta unakimbizwa na sauti....unatumia nguvu kujiokoa yeye katulia zake haahaa!!!kuna umri flani huwezi kupitwa na tukio LA ubwabwa mtaani hata kwa dawa...hasa kwa sisi wa uswazi shida sana.
 
Utotoni nilikuwa napenda sana kukamata panzi na nilikuwa napenda sana kuwachezea , kuna siku tulikuwa na mama na Baba katika njia fulani ilikuwa na maua mengi sana, nikaona nyuki katika ua, akili yangu ikaniambia yule pia ni panzi ebwana ww si nika mshika mkononi nikambananisha asiniponyoke kilichofuata ilikuwa ni kilio njia nzima .
 
😀😀😀 utoto maji ya moto hukuweza kutofautisha panzi na nyuki mkuu👍
 
Back
Top Bottom