GIRITA
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 4,432
- 5,864
Napenda kutoa salam kwa ndugu zangu humu jukwaani vijana kwa watu wazima.
Moja kwa moja kwenye mada...Maisha yana Mapito mengi sana.
Lakini Mimi nitawaletea vituko, nilivyowahi kuvifanya utotoni ambavyo mpaka sasa bado navikumbuka havijafutika kichwani kwangu na amini kila mmoja amewahi kupitia na kufanya mambo kulingana na akili ya utoto ilivyomtuma na yeye kuona yuko sahihi kabisa.
Kulingana na Mazingira niliyopitia katika makuzi yangu nitaeleza matukio machache au vituko nilivyovifanya utotoni mpaka Leo huwa nakumbuka nabaki kucheka peke YANGU.
~Tukio LA kwanza~
Ilikuwa miaka ya 2000 hivi tulikuwa tunaishi mkoa wa Mwanza maeneo ya iLuganzala karibu au jirani na kiwanda cha bia TBL..sasa nyumba tuliyokuwa tunaishi nyuma YAKE kulikuwa kuna njia ndogo watu wanapita kuelekea mnadani, sabasaba kununua mahitaji yao.
Kuna MTU alikuja nyumbani akaleta elfu kumi kipande akatupa watoto tukawa tunaichezea....ikawa zile siku za watu kwenda sabasaba tunakaa njiani na kile kipande cha elfu kumi... tunawategeshea watu wanaopita kwa kukifunika na, mchanga...halafu tunakaa pembeni.
MTU mzima anapita akiiona ile teni ilivyofunikwa na mchanga anaikanyaga taratibu na kiatu halafu anaikota kwa umakini watu wasimuone basi...ile akiinuka aondoke anaona ni kipande cha hela,sisi tunaanza, kumcheka...anapata hasira akitaka kuondoka nayo... tunaanza kulia kwa sauti kubwa mpaka anaamua kuitupa..tunaichukua tunaitegesha tena.
Tulikuwa tunawasumbua watu wazima sana mpaka tulipotaka kupigwa ndiyo tukaacha huo mchezo, na ule wakumwita MTU anayetembea halafu unamwambia umedondosha akigeuka mnacheka mnakimbia.
~Tukio LA pili~
Hii nilikuwa kama darasa LA NNE wilaya x,mkoa z..Mimi na mshikaji kwangu sana kipindi hicho alijukana kama HB...huyu alikuwa ananipiga tafu sana maisha ya shule...mkitoka mapumziko ananunua misosi mnakula na kusaza...kutokana na ushkaji kuzidi ikabidi tuunde kundi LA muziki Mimi na yeye kwa sababu nilipenda sanaa,muziki,kuchora,n.k
Tukawa tunafanya mashindano ya kurap
Pale skuli kila inapofika SAA NNE muda ya break...tunaenda nyuma ya madarasa tunaanza kushindana kurap...tulikuwa tunaandika hadi mashairi tunaya rap kwa ufasaha na ustadi mkubwa kama wasanii kweli,tulikuwa tukishindana na kundi LA jamaa wengine wikiongozwa E...zawadi kwa washindi ilikuwa ni Mapapai ya kuiva maana kulikuwa na mipapai kwenye eneo LA kanisa jirani na shule.
Sasa siku moja kulikuwa hakuna masomo wanafunzi wanacheza tu sikumbuki kulikuwa na tukio gani,tukaamua tufanye tour kila darasa tunaingia tunarap....tulianza darasa LA jirani ya darasa letu tukapiga rap yetu vizuri....kuingia darasa linalofuata mambo yakawa si mambo.
Tulikuwa tunashika kalamu mfano wa maiki tunaimbia sasa ile tu natoa maiki YANGU tuanze kazi Mimi na HB...akatokea jamaa flani aliyekuwa ananizidi kimwili sijui miaka maana nilikuwa mdogo mdogo, ile naanza kuimba nilikuwa mbele pale ubaoni wanafunzi wote wanatusikiliza...jamaa akaniambia unaimba nini wewe unanuka mdomo!!!...aisee nilipata hasira halafu ilikuwa mwezi wa ramadhani...hali ya mdomo kuwa tofauti ni kawaida kwa mfungaji nilimvuta jamaa nikamrukia na kichwa...ile kumuachia damu...anamwagika damu puani kama maji,hakuna aliye amini kwa udogo wangu kama ningeweza kumvujisha mchuzi yule bigy hadi maticha walibaki wanashangaa kama ni kweli au ni muvi.
Nikawa mpole sana kama nimenyeshewa na elnino...nikapelekwa ofisini nikatandikwa bakora nyingi sana.
Nikaambiwa nikamlete mzazi ampeleke yule jamaa hospitali, nikaenda home nikamwita faza ...kufika shule faza akanitetea akasema sipiganagi bila kuchokozwa, kwa hiyo bigy ndiyo mchokozi.
Alipoambiwa sababu akabaki anacheka ... .akaniambia nimpeleke jamaa hospitali akatibiwe nikampeleka akapata tiba...Ila baadae nikawa namuonea huruma Ila nikawa naogopeka pale skuli mpaka Leo sijawahi pigana tena.
Najua nimewachosha wakuu ni katika kubadilishana mawazo ili kufurahi na kuondoa stress za maisha karibu na wewe utupe Tukio lako enzi za utoto...huku ukisikiliza ngoma ya songa enzi za utoto.
Wasalaam G.R.T