Vituko vya watoto wa-kishua

Vituko vya watoto wa-kishua

Tutafute ela,

Kama ilivyo ada wanajopo tupeane laini laini za ndugu zetu hawa"high price life"watoto wakishua..

Kiukweli ukitaka usiwe na stress jaribu kukaa nao hawa, wana-exposure sana anaweza kupa hela akasema "keep change" hawa wakishua wakike, hata prof jay ashaambia"keep change, unamawazo mengi, itakufariji wikend "hizo ndo depo zao...Mambo ya kuhongana hawajui

Tukija kwenye ngeli hapa ndo intaneshno skuli au havard, wanajua ile lugha, wanamwaga yai wanatema matusi hataree ka kwenye movie..

Ngeli kwao si janga ka huku kwetu yes no watu wanakutolea mimacho, wao wanamwaga tena kwa kasi ukitoa macho hayupo hawamjui Ras simba

Raga sana, hata movie zao ni classic na wakianza kusimuliana we was acheche inabidi usepe utapata shida hebu imagine movie imetoka jana saa6usiku wao wanayo...au yametoka matrail wanayo...

Misosi sasa hapo ndo utafurah na roho yako, akinunua kiepe au kuku anagusa gusa maji kidogo hawazi, mi nikienda na mwantum viepe vinatujua...wale sio ka wanaume wa mikoani kula kilo2 za ugali mtu mmoja..ndo maana uchumi unashuka.

Basi bana ndo vurugu zao hapo ujasikiliza nyimbo zao hahaa unawezahisi wanataka kulala, unakuta wanaskiliza msanii wa Finland au Slovakia sijui Slovenia mi na ww hatuwajui kibaya zaidi unakuta anatumia mp4 ya ka m1 iv na hawazi...

Wao kulia sio mpaka msiba, wao kulia hata akijiskia analia ila analia kishua sio ka kaweka vuvuzela..

Upande wa nguo ka sio mvumilivu unaweza anza kulia kimoyo moyo maana sio kwa vinguo vyao AF brand ka gucci. Lv.d&g aisee kibegi simple laki7 mwanangu wa geto analipa semester pale chuo..

HAAA WAKISHUA RAHAAAA jazieni jazieni maana dah
Mwanaume wa dar on fleek
 
Tulianza vuzuri sana nimemrekebisha mambo mengi ila kwenye swala la jikoni hakutaka kabisa. Siku nyingine anasemwa na marafiki zake lakini wapi. Mwisho wa siku mi nikajiona kama mpitaji tu. Sikua na la ziada.
Majukumu ya mwanamke kwa mwanaume si kupika wala kuosha vyombo.
 
Hao madogo ni wapuuzi sana. Kuna mmoja alikua demu wangu ila hajui kupika. So akija geto analala na movie na instagram. Hata vyombo haoshi mikucha mirefu mpaka kulee..

Sasa kuna siku katoa boko. Nimetoka class nikafika geto nikamkuta kalala mi nikabadilisha nguo nikaenda uwanjani kipiga tizi. Kumbe kajishtukia akasema eti ajaribu kupika wali,, mamamaaaaa yan wali umetoka bokoboko, chini umeungua, hayo mafuta na chumvi ni hatari. Hatukufika mbali nikashindwa.

Sema sekta nyingine alikua good. Anaweza kuja na kuku mzima nawaita washikaji tunapiga. Au kwenye ulabu. Wanajua kutoa pesa.
Kwan mke wako huyo mkuu we si ungevumilia tu mikuku hiyo au kujifanya mgumu??
 
Kwan mke wako huyo mkuu we si ungevumilia tu mikuku hiyo au kujifanya mgumu??
Hahaa.. Mkuu washikaji walinilaumu kinoma sema nilikua sina budi kuachana nae. Ki ukweli yapo mengi nikianza kuelezea kuna watu itakua rahisi kunifahamu au kumfahamu yeye. Hasa niliosoma nao those days
 
Watoto wa Mbowe wanaishi kwenye hii kauli..

"keep change,unamawazo mengi,itakufariji
wikend"
 
Hao madogo ni wapuuzi sana. Kuna mmoja alikua demu wangu ila hajui kupika. So akija geto analala na movie na instagram. Hata vyombo haoshi mikucha mirefu mpaka kulee..

Sasa kuna siku katoa boko. Nimetoka class nikafika geto nikamkuta kalala mi nikabadilisha nguo nikaenda uwanjani kipiga tizi. Kumbe kajishtukia akasema eti ajaribu kupika wali,, mamamaaaaa yan wali umetoka bokoboko, chini umeungua, hayo mafuta na chumvi ni hatari. Hatukufika mbali nikashindwa.

Sema sekta nyingine alikua good. Anaweza kuja na kuku mzima nawaita washikaji tunapiga. Au kwenye ulabu. Wanajua kutoa pesa.
Ila swala la kupika ni janga hata wa huku kwetu tatizo labda wapike mapishi mapya ya mende
 
Umenikumbusha, kuna toto moja la kiume about 25yrs nikimrudisha mshua wake yani huwa ananikera daddy daddy hana tofauti na dada zake wao USA, Dubai wanakwenda kama tunavyokwenda sie tandale posta
 
...hivi sasa ni saa mbili kamili,
..kwa saa za Afrika Mashariki!
Kwa heshima tu nimekudharau...jiulize kwanini?!! Mana hata bando hujachangia ka mtafutaji usingeingia chitchat saa2 ungeingia jukwaa la uvuvi ufugaji au kule kwa wajasiliamali..ndo hiviii
 
Kama ni kweli unajituma na manisha unafuga Kuku na huku umejiajiri kama boda boda unafaa kuongezewa mtaji.
Mkuu we una element za lipumba MCHUMI MCHWARA bora dikteta uchwara
 
sijawahi kutana na wa kishua,,,,,,,,,,,,!!
Haaa kwani wana mabango mkuu?
Kwa haraka ni lazima uswitch ubadiri viwanja kiufupi uwe misheni town soi kila siku lia lia..sometym unabadirika ata fegi ka uvuti siku iyo unawasha,unaingia kiwanja chochote wapo ka makopo ya plastik yan wamejaa..
Kinachofata ni mpangilio wa stories tu sio mambo ya sisiem mara bashite..unakuta mtu wa mipango ka unamiliki kampuni
Af maeneo ka ayo unaweza chomoka na madili kibao...haaaaahhh
 
Nasisi tulio huku kijijini tutawapataje mkuu...maana naona hizo mandhari ni za mijini ......
 
Nasisi tulio huku kijijini tutawapataje mkuu...maana naona hizo mandhari ni za mijini ......
Mkuu dunia sio kijiji tena ni jiji kwani nauli ya mjini na matanuzi shingap
 
Nasisi tulio huku kijijini tutawapataje mkuu...maana naona hizo mandhari ni za mijini ......
Wewe huko pambana na watoto wa Mtendaji wa Kijiji au Mwenyekiti wa Kijiji, pia wapo watoto kutoka familia zile zinazo ogopwa kwa Uchawi.

Mabinti kutoka katika Makundi hayo niliyo kutajia, wana vijitabia vinarandana na Wa-kishua kutoka Mjini..[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom