The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,282
- 117,244
Miaka kama sabna iliyopita nilikuwa kwenye mizunguko city center mara kufika mtaa wa Lumumba CRDB kuna mtaa wenye ofisi za TRA hapo kulikuwa na kimgahawa cha watu wenye asili ya kiarabu.
Nikaingia nikaagiza chai ya maziwa na vitumbua viwili na katlesi mbili dah... Vitumbua vyake kwanza kwa macho tu vilikuwa tofauti
Vilikuwa vikavu kabisa.....kwa kawaida vitumbua huwa na mafuta lakini vya kwake vilikuwa vikavu...nikaanza kula dah.. vilikuwa laaini na vitamu ajabu...
Nimetembea kuanzia Zanzibar hadi Tanga sijawahi kula vitumbua kama hivi...ikawa kila nikienda City center napitia hapo
Siku moja kwenda pale nikakuta vutumbua tofauti nikauliza hivi vitumbua mbona sio vile vya siku zote
wakaniambia yule mpishi wa mwanzo kaondoka...duh.. nikauliza namba yake ya simu ili nijue kahamia mgahawa gani hawakunipa...
Mpaka leo navikumbuka vitumbua vile....yaani.....