nipo geita eneo lina udongo wa mfinyanzi,
Kitunguu kinastawi sana kwenye eneo kavu kiasi hasa wakati wa kiangazi na kama kuna maji ya kutosha ya kumwagilia ila gharama za pembejeo ni kubwa sana. Kwa mfano kwa maeneo ya Singida ambako ni eneo la pili kwa Tanzania kwa kulima vitunguu mavno wakati wa kiangazi ni kama gunia 60 mpaka 80 na gharama ya kilimo ni shilingi laki 9 mpaka 1100000.
Wakati wa masika gharama ya kulima ni kama shilingi 700000 mpaka 800000 lakini mavuno ni chini ya gunia 60.
Gharama hupungua kutokna na kwamba huitaji kumwagilia lakini pia mavuno hushuka kutokana na kwamba kitunguu hakihitaji maji mengi.
Eneo la Mang'ola Karatu ambako linaongoza kwa uzlishaji gharama za kilimo cha kitunguu ni kubwa kutokana na pembejeo kuwa aghali hasa madawa na mbolea (1,700,000 mmpaka 2,000,000 kwa eka) lakini uzalishaji ni mkubwa hadi gunia 160.
Vitunguu vina bei nzuri sana hasa miezi ya September hadi march kutokana na maeneo ya uzalishaji mkubwa hasa Karatu uzalishaji kupungua.
Lima lakini vitunguu vinahitaji uangalizi mkubwa................Process
Kuotesha kitaluni mpaka wakati wa kung'oa ni siku 45
Kupandikiza mpaka kuvuna ni miezi 3
Note: mimi si mkulima lakini kuna study nilishawahi kuwa involved na maeno hayo nilifika.
Maundumla na
Slave mpo hapo?