Vitunguu vs Viazi Ulaya

Vitunguu vs Viazi Ulaya

Soko ni zuri sana ila inahitaji timing: Kwa mfano Vitunguu kutoka Tanzania huuzwa Kenya, Uganda, rwanda, Burundi, South Sudan!!

Lakini bahati mbaya wakenya ndio huchangamkia kuuza vitunguu huko kwa wingi kuliko Watanzania. Ukifika soko la Kilombero Arusha kuna wastani wa Tani 50 mpaka 70 zinazopelekwa Kenya kuanzia miezi ya March mpaka October. Waakati mwingine wakenya huenda mashambani huko Karatu kuchukua wenyewe na hata waganda na wanyarwanda pia.

Kwa hiyo unaweza kuona mtu kutoka Rwanda kwa umbali woote huo anaenda kuchukua vitunguu Karatu ama Singida. Lakiini inahitaji ucheze na hesabu za season.............Kwa mfano msimu wa mavuno na mauzo kwa Mkoa Wa Singida ni miezi ya February mpaka June baada ya hapo mavuno yanayoletwa kwenye soko la Ukombozi Singida (soko kuu la vitunguu ukanda wa kati) unakuwa chini sana mapaka kufikia magunia 50 kwa siku.

Kwa Karatu mavuno yanakuwa makubwa miezi ya May mpaka October.........Ikifika October wanahifadhi vitunguu kwenye maghala............. ingawa miezi mingine uzalishaji unaendelea kwa kiasi kwa sababu wanatumia sana kilimo cha umwagiliaji.

Ukiangalia hesabu hizo hapo utaona miezi ya October mpaka February kunakuwa na ombwe la upungufu kwa hiyo soko linakuwa zuri,..........kwa hiyo kama utalima kuanzia mwezi huu utavuna December na bei inakuwa nzuri tu.

Tena kwa large scale ndiyo nzuri kwa sababu utaweza kuuza mwenyewe sokoni badala ya kusubiri walanguzi shambani kwako. Kifupi bei ya vitnguu kwa gunia 1 likiwa shambani kwa muda huu ni Tsh. 60000 mpaka 70,000 (singida)....soko la Arusha ni sh 70000 mpaka 80000.

Kuna kingine nimeacha?

Watanzania tunafanyiana figisu sana, Mkenya akija hapa atalipia ushuru/kibali kimoja au viwili tu anavusha mzigo! Nenda wewe Mtanzania uone utitiri wa vibali sijui huwa unatokea wapi.

Sister wangu kabisa alishalishtukia hilo deal kitambo lakini alikwamishwa na utitiri wa mambo ya ushuru na vibali mpaka akaacha. Alipeleka mara moja tuu hapo Kenya.

Ajabu Wakenya wanavusha kila leo bila vurugu zozote! Nahisi tunabaniana
 
Back
Top Bottom