Vituo vingi vya kulelea watoto yatima vimekuwa ni sehemu ya upigaji

Vituo vingi vya kulelea watoto yatima vimekuwa ni sehemu ya upigaji

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Habari ndugu wana jamii forums wenzangu,

Siku ya leo naomba niwasilishe hili tatizo ambalo nimeliona, nimekuwa ni mtu wa kujitolea kwa kile kidogo Mungu anachonibariki sehemu mbalimbali na kwa watu mbali mbali wenye uhitaji hapa nchini.

Changamoto niliyoikuta au kuiona misaada inayotolewa haiwafikii walengwa kama inavyokusudiwa. Mfano mkubwa ni hivi vituo vya kulelea yatima unapotoa msaada kama mchele, sukari na vitu vingine ukweli ni kuwa vitu hivi hawavitumii walengwa wamiliki wamekuwa wakiviuza kwenye maduka ya kawaida na muda mwingine kuvitumia wao wenyewe.

Ninaomba sana wahusika wajirekebishe vinginevyo nitawataja kwa majina pamoja na kuorodhesha idadi ya vituo hivyo.

Screenshot_20221217-075741.png
 
Back
Top Bottom