Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu,tunakoelekea ni full kusifia,Nchi imekuwa ya ovyo sana,juz makonda kawazalilisha mdee na Bulaya na vyombo vingi vikarusha uzalilishaji huo,3: Kituo cha #EastAfricaRedio kimekutwa na hatia ya kurusha maudhui yenye kukashifu utendaji wa Serikali katika uteuzi wa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) na kupewa onyo kali pamoja na kutozwa faini ya Shilingi milioni 3.
Kosa la Star Tv ni nini, sijaona hapo juuƘimeeleweƙa hasa ƙwa hili la star tv😊
Ni kwel hao clouds ni vinara wa kuponda upinzan na kufagilia serikali ya ChattleTV zote ni CCM hivyo sina tatizo wapigwe sn tu, safi TCRA
Aisee wanakaba mpaka penalti.MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevitoza faini ya Sh milioni 30 vyombo vya habari sita, kwa kukiuka kanuni na maadili ya utangazaji ikiwamo redio ya Clouds FM kuzungumzia supu ya pweza kuimarisha tendo la ndoa katika muda ambao wasikilizaji wanaweza kuwa watoto.
Mbali ya Clouds FM, vyombo vingine vilivyoadhibiwa ni East Africa Radio, na televisheni za Star, Sibuka, na Global Tv na Duma Tv.
Akisoma uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema vyombo hivyo vilikiuka kanuni za mawasiliano kwa nyakati tofauti.
Mapunda alisema redio ya Clouds FM kupitia kipindi chake cha Jahazi, walihamasisha vitendo vya ngono, kwa kutumia supu ya pweza katika kuimarisha tendo la ndoa kwa muda ambao wasikilizaji wanaweza kuwa watoto.
Alisema baada ya kusikiliza utetezi wao, wanatozwa faini ya Sh milioni saba na kupewa onyo kali baada ya kuwatia hatiani kwa kosa hilo.
Katika shauri lingine, kituo cha Duma TV kimetozwa faini ya Sh milioni saba na kufungiwa kuchapisha maudhui kwa muda wa mwezi mmoja ili wajipange na kuzifahamu kanuni na kuzingatia weledi na maadili ya utangazaji.
Mapunda alisema Duma ilikutwa na hatia ya kukiuka kanuni kwa kuchapisha na kutangaza maudhui yenye lugha isiyo na staha na iliyo na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanaume na wanawake.
Alisema redio ya East Africa imetozwa faini ya Sh milioni tatu na kupewa onyo kali kwa kukiuka kanuni hiyo, kwa kurusha maudhui ya kukashifu utendaji wa serikali kupitia uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kutumia lugha ya kashfa dhidi ya utendaji wake.
Vilevile Global Tv imetozwa Sh milioni saba na kupewa onyo kali, baada ya kupatikana na hatia ya kuchapisha picha ya mnato na kutangaza maudhui yasiyokuwa na lugha ya staha na yenye kushabikia vitendo vya mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja.
Mapunda alisema maudhui hayo, yangeweza kuwaumiza na kuwakwaza waumini wa dhebebu la Anglikana na Watanzania kwa ujumla. Pia, alisema Sibuka Tv inatozwa faini ya Sh milioni tatu baada ya kupatikana na hatia ya kushabikia mauaji ya kutisha katika muda, ambao watoto wanaweza kuwa sehemu kubwa ya watazamaji.
Kuna tofauti kati ya neno kukashifu na kukosoa. Kilichofanywa hapa ni kukosoa ingawa kwa mazingira ya sasa kukosoa kunachukuliwa kama kukashifu ama uchochezi.3: Kituo cha #EastAfricaRedio kimekutwa na hatia ya kurusha maudhui yenye kukashifu utendaji wa Serikali katika uteuzi wa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) na kupewa onyo kali pamoja na kutozwa faini ya Shilingi milioni 3.
Acha wapigwe haswa wapuuzi snNi kwel hao clouds ni vinara wa kuponda upinzan na kufagilia serikali ya Chattle
Nimesema ƙimeeleweƙa ƙwa maana ƴa Uonevu ulioƙithiri , sijui ulinielewaje hapa😀Kosa la Star Tv ni nini, sijaona hapo juu
Hiyo sidhani hata watoto wa chekechea huwa wanaangalia wakati wowote wakiwa nyumbani au popote. Watangazaji na wanaotangazwa wote hawana mvuto kwa wasio wanachama wa CCM wakiwemo watoto.Vipi TBC 1 haipo?
Mtoto anayeangalia katuni na hajafika la saba habari inamsaidia nini?Kwenye suala la mizania TBC nawapa heko, Taarifa ya Habari eti ni PG 13 [emoji15][emoji848][emoji87]
Mtoto anayeangalia katuni na hajafika la saba habari inamsaidia nini?
Aiweke iweke, ipitishe kwa chinii.Pongezi kwa wasafi media ya Diamond
Waondoe na tangazo la TIGO linalomwonyesha mwanaume zuzu aliyeacha sh.10,000.00 siku ya kukumbuka kufungwa kwa ndoa yao alafu anakuta mzigo wa 50,000.00, mwishoni kabisa mwa tangazo ni aibu tubu, waliondoe.
Serikali hii ina mapeaa mengiiiiiiii.3: Kituo cha #EastAfricaRedio kimekutwa na hatia ya kurusha maudhui yenye kukashifu utendaji wa Serikali katika uteuzi wa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) na kupewa onyo kali pamoja na kutozwa faini ya Shilingi milioni 3.