Sura-ya-Kwanza
JF-Expert Member
- Nov 17, 2007
- 568
- 12
Huu ni Uhujumu wa Uchumi. Period!
Kuna umuhimu wa kuwa na emergency meeting ya bunge letu.
Huu sio wakati wa mazingaombwe!
Hii kuongeza gharama ya posho kwa hawa jamaa kwenda kulala tu kule, nina uhakika 99% ya wabunge hawana uchungu na wengi hawajui kama jamaa wamegoma kuuza mafuta leo, maana wao wanalipwa lita 2000 kama sikosei kwa mwezi, Dawa ni sheria ichukue mkondo tu si ipo!
Hii kuongeza gharama ya posho kwa hawa jamaa kwenda kulala tu kule, nina uhakika 99% ya wabunge hawana uchungu na wengi hawajui kama jamaa wamegoma kuuza mafuta leo, maana wao wanalipwa lita 2000 kama sikosei kwa mwezi, Dawa ni sheria ichukue mkondo tu si ipo!
Sheria ya Udhibiti wa Makosa ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 1984 inatamka makosa yafuatayo kuwa baadhi ya makosa ya kuhujumu uchumi, ni pamoja na yale yote yenye kusababisha hasara kwa mamlaka ya serikali.
Kwa vile wamesababisha serikali kutopata ushuru, basi hii itawafaa,yaani sheria ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 1983/84Sheria ya uhujumu uchumi ya mwaka 1984 inavieleza vitendo vya uhujumu uchumi kuwa ni pamoja na vitendo vya rushwa na kuhodhi mali au bidhaa ili kusababisha bei kupanda au kushuka.
Kwani jamani kama mafuta hamna kwenye depot si kiasi cha kutuma magari 2 tu ya watu wa wizara, kukiwa na Polisi na TISS mbrs kukagua kujua ukweli???
Una hisa katika hayo makampuni ya mafuta?Huku ni kuwaadhibu wananchi wasio na hatia. Lakini pia EWURA pia wanastahili lawama. Inaonekana hawakufanya homework yao vizuri. indicative prices ziko chini sana. Matokeo ndiyo haya.
Sheria ya Uhujumu Uchumi,Sheria ya Mafuta na ile ya EWURA.Zatosha kuwatoa kwenye Industry.Mwanzoni walisema wanaomba kwanza stock yao iishe ndio washushe bei. Sasa wanadai hawana mafuta. Huu ni ubabe wa kijinga kabisa. Washughulikiwe.
Hivi Serikali ikiamua kutaifisha hivi vituo hawa jamaa si wanaweza kukimbilia mahakamani na kuibwaga serikali? Ni nini sasa kifanyike ili tuwabane kila kona na kuwaondoa kabisa kwenye hiyo biashara bila kuathiri utawala wa kisheria? Naombeni jibu!!
Shibe ni mwana malevya, hao Oilcom wamelewa pesa sasa wanafanya vituko. TPDC nafikiri haiukuachishwa kiubaya ilikuwa ni kuwapa watu wengine chance ya kuonyesha uwezo wao. sasa wameleta jeuiri lazima kutakwua na mkono wa mtu humo, kama siyo fisadi kutoka mjengoni dodoma.
Unajua nchi kama Rwanda na Burundi wamethiliwa na vita ila kama ungeniambia nichague wapi niishi ningeenda Rwanda, principled country, huwezi kuamka leo ukanzisha sheria yako unayoijua ya ulaji ukafanya implemetation za kijinga kama Tanzania.
Tuzidi kushukuru kwa kuwa wapumbavu, hatuna choice, kila kitu ndiyo mzee.
Kwa nini Waziri na EWURA wajiuzulu?Hiyo conclussion kwamba wamedanganya mmeitoa wapi?....wanafanya hivyo kwa sababu wanajua hakuna serikali pale,hizo kamba zao za kusema stock imekwisha ghafla ni upumbavu wa hali ya juu na uwongo wa kitoto,serikali lazima wapate sababu za kueleweka na zinazokubalika kisheria kwanini hawakuagiza mafuta on time wakati wamepewa hilo jukumu na kama kuna uzembe au any sabotage hawa ng'ombe lazima watiwe adabu,na uchunguzi(physical) kwenye mapipa yao lazima ufanywe sio data zao zao za kupikwa...hakuna mtoto hapa wa kudanganywa na tunajua hizi ni deal zao za kilafi tuu ili kupata super profit,dawa ni kuwafuta kwenye biashara ya mafuta forever na kuwafikisha mahakamani kuwachapa fine za kuwafilisi mpaka mali zao,hatuwezi kuvumilia sabotage kama hizi za kurudisha nchi nzima nyuma kiuchumi na kutishia usalama wetu...inakuwaje leo oil price ikipanda new York nao wanapandisha for the same reason lakini ikishuka eti stock ni ya mwezi uliopita? sasa ni time ya kuwafanya mfano kwa watu wote wenye tabia kama hizi na kuhakikisha hakunasector/mtu atatuchezea kwa namna hii tena...ni EWURA/waziri wa nishati nao watimuliwe kwa uwongo wao wa kusema last week kuna mafuta ya kutosha na Ewura wameshindwa kuwadhibiti hawa walfi wakti kuna sheria kibao zilikuwepo za kuwatia adabu lakini hawakufanya kitu...lazima kuwe na zero tolerance kwenye vitu kama hivi la sivyo tutazidi kuwa maskini tuu.
Mlitaka waende kwenye magazeti na TV ndio mjue wanafanya kazi?Hivi Mizengo Pinda anafanya nini?... Mbona kwenye critical interventions za serikali yeye anakua mtu wa kujivutavuta.
Ngeleja wizara imemwelemea, waziri mkuu kaingia mtini, Rais anajikausha... Kazi ipo.
Hapo ndo unapomkumbuka Lyatonga,...