Vituo vya mafuta katikati ya mji na makazi ya watu Dar: Bomu linalosubiri maafa makubwa

Vituo vya mafuta katikati ya mji na makazi ya watu Dar: Bomu linalosubiri maafa makubwa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Tujiulize maswali haya
Je mipango miji inaruhusu vituo vya mafuta katikati ya miji na makazi ya watu?
Je sera ya mamlaka ya viwango na ubora inaruhusu vituo vya mafuta katikati ya miji na makazi ya watu?
Vipi wizara ya miundombinu?
Vipi wizara ya mazingira?
Jeshi la zimamoto je nalo haliwezi kuhusika hapa?

Kimsingi pamoja na tahadhari zote za usalama zinazochukuliwa lakini bado haishauriwi kuwa na vituo vya mafuta katikati ya miji na makazi ya watu. Na sheria ya vituo vya mafuta inasema kuwe na umbali USIOPUNGUA kilometer 5 nadhani kati ya kituo kimoja hadi kingine

Mafuta ni kitu kinachoweza kulipuka kwa haraka sana na kusababisha maafa makubwa ya watu na vitu kwa muda mfupi mno.. Hata magari yake na sehemu za kuhifadhia hayo mafuta zina alama kubwa za tahadhari ya hatari INFLAMMABLE (VILIPUZI)

Ni taasisi gani imeruhusu hili jambo la hatari kiasi hiki katikati ya mji na makazi ya watu na bila kuzingatia umbali kama sheria inavyotaka?

Kuna kampuni imeotesha vituo vya mafuta kila kona ya jiji ndani na nje, kwenye makazi ya watu, kwenye misongamano, kwenye maofisi na hata karibia kabisa na ofisi za mamlaka ya juu ama nyeti... Mtandao wa hivyo vituo unaleta mashaka na kutia hofu kubwa hasa katika kipindi hiki dunia inapopambana na ugaidi wa kila aina

Imagine itakuwaje kikatokea kikundi cha magaidi (Eeh Mungu tuepushe) kikakamata vituo vinne tu katikati ya jiji na kuvilipua... !? Ninini kitatokea?

Miundombinu yetu na vifaa vyetu kwenye kupambana na majanga makubwa ya moto bado sana... Tumewekeza kwa nguvu sana kwingine kote lakini sio kwenye kikosi cha zima moto... Tunaishi tu kwa kudra za mwenyezi Mungu...!

Kampuni husika iliyootesha vituo husika ndani katikati ya jiji la Dar imeishia kupigwa faini ya Tsh bilion tatu... Achilia mbali kama zitalipwa ama la ... Swali la kujiuliza je tuko tayari kuhatarisha maisha ya mamalioni ya watu na mali zao kwa ajili ya bilion 3? Maana baada ya kupigwa faini pengine ataruhusiwa aendelee na biashara.. NADHANI...!

Ni ngumu kumwambia abomoe kwakuwa pengine ana nyaraka zote muhimu za kumruhusu kufanya ujenzi na kufanya biashara..! Akizuiwa ndio mwanzo wa kushikana uchawi na pengine hakuna aliye tayari kufanya hivyo! Kwakuwa pengjne kila mmoja kala kwa urefu wa kamba yake!

Ni mpaka pale tutakapopigwa tukio moja baya kubwa na la kustukiza ndio akili zitatukaa sawa! Lakini tutaunda na tume? Jibu ni ndio kwakuwa huo sasa umekuwa utamaduni wetu...!
 
Afu Hivi Vituo mbona Vimeibuka kama Uyoga ndani Ya muda mfupi Kama miezi Mitano Iliyopita?.....!
Kuna kitu kinaitwa timing...ukikosea kidogo tu umepigwa bao... Hivyo vituo kwasasa havihamishiki la sivyo fidia yake si ya kitoto ndio maana vimeishia kupigwa faini ambayo hata hivyo itapungua sana na kulipwa kwa mafungu... Ukikomaa utaambiwa nenda mahakamani
 
Nilijaribu kuvihesabu nilishindwa nikaishia 11 maana kila siku vinaongezeka. Kufikia mwakani vitazidi 15 nahisi
Inawezekana ni wale ambao walikuwa Morogoro road wamekimbilia huko kwakuwa miundo mbinu ya sasa Ubungo Kibaha sio rafiki tena
 
Mshana Jr Una uhakika na hio 5km kituo hadi kituo? Kitu ambacho kinanishangaza ni pale ambapo vituo viko bega kwa bega. Hii nimeiona Kigamboni, au vituo viwili umbali usiozidi 200m!
Yeah hiyo ndio sheria ya zamani labda iwe imebadilishwa ngoja nitaisaka.. Mimi hapa Kibada mpaka mjimwema nimeshahesabu si chini ya nane
 
Mshana Jr Una uhakika na hio 5km kituo hadi kituo? Kitu ambacho kinanishangaza ni pale ambapo vituo viko bega kwa bega. Hii nimeiona Kigamboni, au vituo viwili umbali usiozidi 200m!
Kilomita 5 umbali toka kituo hadi kituo SIO kweli.
Ni mita 200 katika upande mmoja, ila kama barabara inawatenganisha haiangalii umbali.

By the way uchawi na milipuko wapi na wapi? Kwa nini wachawi wanajibadili kuwa paka usiku kwa nini asije na sura yake halisi ama mtu wa tatu huwa halali ni mwili na akili tu zinapumzika ila roho ipo macho.
 
Back
Top Bottom