Vituo vya mafuta katikati ya mji na makazi ya watu Dar: Bomu linalosubiri maafa makubwa

Nieshangaa kuna mjini Songea kuna jamaa kanunua nyumba 5 katikati ya makazi ya watu na kuzivunja anajenga kituo cha mafuta, hii ni sawa kweli?
Yule jamaa kazi yake ni kununua Nyumba za watu kubomoa na kujenga petrol stations
 
maana wanaonunua apartments za million 300 nao tuwaweke fungu gani? Hata hao nao sio money laundering wengi ni za urithiπŸ₯±
 
Yaani ni Mwenye Enzi Mungu tu wa ndio anaweza kututoa kwenye hili janga walahi uwiii [emoji3062]
 
Nchi hii ina mabomu kila Kona,hospitari mgonjwa wa mguu,anapasuliwa kichwa,wa kichwa anapasuliwa mguu!!
Polisi,watu wanachukuliwa nyumbani wanauliwa,then inatangazwa walikuwa wanajibizana na risasi na polisi,wakauliwa
 
Jana wezuia ujenzi wa vituo hivyo kwa.miezi 3.

Wamiliki wengi wa vituo hivyo ni jamaa zetu asili ya mashariki ya Kati.

Tutegemee kikaango kikali kukinuka
 
Ninapowaambia kuwa CCM ni janga. Waliopitisha hii sheria na kusimamia utekelezaji ni viongozi wa CCM

Sasa hivi wanatukomoa, wanasubiri tuwatoe madarakani kwa kuwanyima kura ndo utaona mambo yatakavyoanza kuwiva.

Hawana ubinadamu. Wenyewe kwa wenyewe wanauana
 
Kutoka Kibada mpaka round about ya kwenda darajani vipo 7! Umbali usiozidi 5km
Tunapohamasisha kwenda ulimwengu WA gesi, hivi vituo inabidi viongezeke na kuwa Karibu na watumiaji, ni salama zaidi mitungi ya gesi kuuzwa vituo vya mafuta kuliko Sasa inavyouzwa masokoni na vibanda visivyokuwa salama!! Watanzania tupunguze wivu usiokuwa na tija!! Kituo Cha mafuta/gesi kinakuletea madhara gani!? Hakuna sehemu imeandikwa kuwa kituo Cha mafuta ni sehemu ya Moto, by the way nyumba zinaungua zaidi ya vituo vya mafuta!! Nishauri wanaohusika kuaratibu kuwashauri wenye navyo wazingatie taratibu zote za usalama na Sio kuanza kuwasumbua na kuwawezesha Ewura, OSHA, na Nemc kufanya hii biashara kuwa kisima Chao cha rushwa kila uchao!! Tunaimba energy invasion Huku tunajikata mkono
 
Hapa Tandale barabara nzima toka Sinza hadi Kanisani kulikua hamna vituo. Sasa hivi vimeota kama uyoga na tunafurahi kwasababu walau taswira nzuri inaonekana. Yale majumba mabovu yote wameyabomoa.
 
Vinazidi kuchipuka kila kona ya mji

Sent using Jamii Forums mobile app
Utamaduni wa kimachinga.

Kutembeza huduma.
Utofauti ni kuwa Hawa wa vituo hawana filosofia ya miji inakuaje kwahiyo wako kama wakimbiza bidhaa gulioni wakipona magari mengi tu wote wanaenda kujazana huko.

Na mamlaka zinaongozwa na watu wenye like mind..wanasahau, kwa kufanya hivyo wananyong'onyeza uchumi.

Kwenye sayansi ya mipango miji kuna kitu kinaitwa "Catchment Area" ambayo huwa ni eneo kimipaka ambapo huduma fulani inakuwa na uwezo wa kujitosheleza kuwahudumia watu na yenyewe kukua.

Kabla haujaruhusu kituo kipya Je kituo kilichopo kimefanyiwa tathmini?! Mapungufu yake ni yapi!? Huduma hafifu!? Watu wanakosa huduma?! Je kikiboreshwa kwa maana ya kuwekeza zaidi kwenye kuongeza bidhaa kwa maana uwezo wa kuhifadhi mafuta na kuwekewa njia rahisi za kutoka na kuingia, kuongeza dispensing pumps, kutengeneza special access kwa aina Fulani ya magari na mitambo iliyosahaulika kinaweza kufikia mlinganyo service na uhitaji unaotakikana?!

Haya kwa sehemu kubwa hayafanyiki. Na si ya kufanywa na serikali pekee kama mchezeshaji kwenye uwanja Wa maendeleo ya Ardhi ila pia ni muhimu kwa wafanyabiashara pia kujijengea utaratibu wa kufanya haya. Kwa serikali na wafanyabiashara hili ni muhimu sana kwani linawasaidia kulinda mitaji. Na mitaji iliyolindwa inatengemeza soko thabiti.

Kinachoendelea Sasa mikopo ni mingi kwenye kuwekeza ndani ya hizi huduma, ila Matokeo yake ni kuwa nyingi hazifikii full potential maana catchment ni ndogo na inaendelea kuwa infringed kila kukicha. Utaratibu wa kutumia mita 250 ni maono finyu kwa Kweli. Defaulters wa mikopo kwa uwekezaji huu ambao ni aina ya holela iliyodhibitiwa itakuwa kubwa sana... Na itapelekea parasitic development( biashara zinazoanzishwa kufuata biashara nyingine) kufa wakati zisipotarajia.

Happy new year
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…