Vitz 4WD na ulaji wa mafuta

Banned

Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
47
Reaction score
13
Salaam!
Nina gari aina ya Toyota Vitz 2NZ-FE(1.3L) 4WD ya mwaka 2000 ambayo nilinunua Show Room hivo sikujua kabisa kama ni 4WD mpaka nilipo google chasis number nkaona hilo gari huko beforward na kuona pia lina support 4WD.

Issue kubwa na hili gari ni ulaji wa mafuta ambao sikuwa nimeutegemea au nimeupigia hesabu kabla ya kununua gari,maana matarajio yangu nilitegemea icheze kwenye 13km/l on average na hii ni economical kabisa per day kulingana na umbali kuelekea kazini kwangu.
Kwa sasa inakula 7.5-8.2km/l na nilishaleta thread humu na nilizifanyia kazi recommendations zote ikiwemo kutumia 5w-30 oil viscosity lakini pia nilibadili spark plugs nakuweka zile zile nilizokuta kwenye gari i.e NGK plugs ambazo sio za sindano.
Pia nilipeleka gari likasafishwa Nozzels na air clearner ilikua mpya lakini ilisafishwa pia na mafundi wakanishauri ubadirishaji wa tabia za uendeshaji!
Baada ya marekebisho yote haya sijaona mabadiliko yoyote katika Ulaji wa mafuta.

Lakini katika kusoma soma mitandao nkaona huko mitandaoni watu wakisema kuwa ulaji wa mafuta Vitz za 4WD hauko economical ukilinganisha na zile za 2WD/FF.
Na baadhi ya wachangiaji wenye Vitz za hivo wakaonesha fuel economy yao inacheza hapo hapo kama yangu.

Na baadhi yao wakileta mjadala kuwa ukiondoa shaft ya 4WD basi fuel economy itakua vizuri zaidi wakati wengine wakisisitiza kabisa kuwa ukiondoa 4WD shaft kwa gari ambayo ilitengenezwa iwe 4WD maana yake gari itatumia nguvu zaidi na fuel economy itashuka zaidi.

Sasa mimi mpaka hapa nilipofikia nafikiri hili swala la 4WD ndo linafanya gari hili lisiwe na Fuel economy nzuri ila nataka mawazo yenu maana mimi sio mtaalamu wa haya magari na isitoshe sijui kama gari yangu shaft ya 4WD iko ON/OFF maana gari lilikua used from Japan.
Ila nataka kujua impact ya hiyo shaft kuwa ON/OFF vs Fuel economy.

Ikumbukwe uki google hili gari wanakuonesha fuel economy ni 6L/100Kms ambayo ni sawa na 16Km/L on average.
2000 Toyota Vitz, U Modification - all pics, specs, parts and prices

Natanguliza shukrani!
 
Pamoja na 4wd inachangia ulaji mafuta je gari yako ukiendesha inakuwa na pulling nzuri. Kwa maana kuwa iwe nyepesi na kasi kwenye kuondoka maana kama haina nguvu inaweza kuwa na piston ring zimechoka kunasababisha gari kutumia mafuta mengi.
 
Kumbe ndo maana watu huwa hawashauri mtu kununua gari hapa Bongo!
Kama mentality ya watanzania wenyewe ndo hii!
Of course kununua gari bongo inabidi kuwa na umakini wa hali ya juu maana wauza magari wengi wadanganyifu sana na hutumia kutokujua kwa mteja kama namna ya kufosi mauzo. Muanzisha thread anasema hakujua kama gari in 4WD na kama muuzaji angekuwa na ethics angemuambia kuwa ni 4WD!
 
Pamoja na 4wd inachangia ulaji mafuta je gari yako ukiendesha inakuwa na pulling nzuri. Kwa maana kuwa iwe nyepesi na kasi kwenye kuondoka maana kama haina nguvu inaweza kuwa na piston ring zimechoka kunasababisha gari kutumia mafuta mengi.

hii ni much more of experience mkuu!
Labda ntajaribu kumpa mtu mzoefu anipe feedback!
japo kuna mda huwa naiona inakua nzito!
 
Hula 7.5-8.2l wakati gani?
Kwenye foleni?
unapotumia gea ndogo?
au
Unapokuwa highway?

LABDA

4WD hazina matatizo kwenye kutumia, nilishawahi kutumia sprinter, it was just ok
Na sasa natumia BREVIS, still iko OK.

Hilo litakuwa ni tatizo binafsi za mashine, tusisisngizie 4WD kuwa ndio tatizo.
 

Mara nyingi gari nalitumia kwenda kazini speed nayotumia average 35km/h
BaraBara haina foleni kabisa about 1Km ndo kuna barabara ya vumbi na vibonde vya hapa na pale!
Bado naamini hii consumption sio ya kawaida kwa gari la 1300cc!
 
Mara nyingi gari nalitumia kwenda kazini speed nayotumia average 35km/h
BaraBara haina foleni kabisa about 1Km ndo kuna barabara ya vumbi na vibonde vya hapa na pale!
Bado naamini hii consumption sio ya kawaida kwa gari la 1300cc!
Pole.
TUangale jinsi mfumo wa mafuta unavyoweza kuwa:-
Tank-fuel pump-pipes-petrol filter-nozzles
ambapo baade huunganishwa na:-
mfumo wa umeme(Sensors), plugs, na combustion chamber na hasa kama ama piston au bore holes zikiwa zimelika.

piga less na angalia kamamashine yako inavuta mpaka 7 au 8 ili kujua uzima wa mashine na associated accessories.

Gearbox ikiwa haifanyi kazi vizuri, nayo huchangia sana.

Kiufundi, kimoja kati ya hivyo kinaweza kuwa ndio chanzo cha utumiaji wa mafuta mengi.

Fanya tracking ya mfumo for problem determination/shooting.

Usikubali kubadilishiwa haraka haraka vyombo na mafundi, usipoangalia watakuambia ubadili hado Bodi.
 

Nina IST 4WD inanipa 445 km kwa lita 40..niliitoa Mpanda mpaka Tunduma geji inasoma Empty
 
pole saana kaka, Gari yako hio itakua full time 4wheel drive sidhani kama ina button ya diff lock ndo maana inakula saana wese, iingekua na button unaondoa nakutumia kawaida baadae unapoitaji unaweka hio ina saidia kwenye issue kama yako,mimi na mazda tribute ni 4wd aka AWD ina diff lock button na inakula kwa 9.kitu /litre hadi nane km sometimes. hapo nakushauri huitoe hio system ya 4WD,4WD inaongeza load kwenye engine maana gari yako ni front wheel drive ambayo diff ya nyuma inatumika kama 4wd ku push yani rear lockers so hapo ni kutoa diff ya nyuma ila kibongo bongo naona uta haribu gari tuh.hio uza tafuta nyingine.
 

maana nilishampatia scenario fundi kashanambia kubadili sijui nozzels!
Then ikigoma hapo akabadili sijui vitu gani kwenye Engine!
 
maana nilishampatia scenario fundi kashanambia kubadili sijui nozzels!
Then ikigoma hapo akabadili sijui vitu gani kwenye Engine!
Hata mfumo wa kuingizia hewa, kuanzia kwenye air cleaner waweza kuwa chanzo pia.
Tafuta proffessional fundi, waweze kukusaidia. Watafute jamaa wa DT Dobies au Toyota ili wakusaidie. HUwa wako cheap wakiwa kwenye magereji yao binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…