Vitz vs starlet

Wakuu naomba kujua kati ya izo gari mbili ....ipi ina ubora zaidi....? Kwa upande wa kula mafuta na usafiri wa umbali mrefu ...vilevile ni gari ipi inayo weza kudumu ...kwa mda mrefu......


Ni hayo tyu wakuu. ....wenye kujua wanijuvyeee

Vitz ndio mwisho wa matatizo,km una kahela ww tafuta kavitz ujiweke tu
 

Unalilia nini sasa

Umekuja na nondo zako za uongo badala ya kuzitetea unaanza kulia lia

Thibitisha 1/100 hata kama ni recommendations za hiyo sijui nini
 
Uzuri umeomba radhi, ulitakiwa ufute kabisa huo ukakasi wako.

Muuliza swali yuko clear, kati ya vits na starlet, ipi gari bora?

Kwa maoni yangu, kwa anayejifunza kumiliki gari, starlet iko poa. Haina magonjwa, bodi imara na spare part zake zipo za kutosha.

Vitz ni mayai flani, za kisasa hivi
 
Ha ha ha
 
Unalilia nini sasa

Umekuja na nondo zako za uongo badala ya kuzitetea unaanza kulia lia

Thibitisha 1/100 hata kama ni recommendations za hiyo sijui nini
kwa kauli hii ndio nimekuona kilaza kabisa na sito poteza time yangu kukujibu tena

"Unalilia nini sasa
Umekuja na nondo zako za uongo badala ya kuzitetea unaanza kulia lia"

Nimejibu maswali kama yako na kwenye thread hii zipo post zangu zaidi ya 15 nikielezea na kujibu kile ninachoulizwa na pia sijabadilisha kauli kwa kile ninachokiamini mm nimebaki na msimamo wangu ule ule wa standard ratio ya kmataifa kwa gari ndogo ni 1/100km pia nakwambia ww kuwa Google si sehemu pekee ya kupata taarifa usitegemee Google tu kuongeza maarifa na kupata information si kila kitu unakimbilia Google ukikikosa unarudi speed kuja kusema hicho kitu hakipo !!!!
Tazama hayo magari then angalia na ulaji wake wa mafuta nimekwambia matumizi au ulaji wa mafuta anapanga mtengenezaji kwa kuzingatia nguvu ya engine (HP) na kwa kiwango fulani cha speed (RPM) na nikasema magari ya ulaya ulaji wake wa mafuta ni mdogo sana sasa nashindwa kuelewa mtu ananibishia kitu ninachokisomea then unabisha kisa umekuta hakipo Google !!!!!! Ukwaju tanzanite miner
 

Mkuu kuna kitu umejichanganya ila haujajua. Mwanzo umezungumzia standard ni 1/100km, naamini ulikuwa unaamaanisha ni 1liter/100km na ndicho watu wanachokupinga.

Ila source uliyotuwekea inasema standard inapimwa kwa liter/100km. (l/100km). Ambapo kwa maana rahisi consumption ya gari ya mafuta inapimwa kuwa kwa 100km imetumia lita ngapi.
 
mkuu temana nae,kumuelewesha chizi unajipa kazi.
 
Nilichokisema ni standard ratio kwa gari ndogo ni 1/100km sijazungumzia matumizi ya mafuta ya gari ambazo mtoa mada alisema pia nikasema swala la ulaji wa mafuta kwa gari inatokana au mwenye maamuzi ya kupanga ni mtengeneza gari mwenyewe kutokana na nguvu ya engine (HP) na kwa kiwango cha mwendo kasi(RPM) sikusema vitz inatumia 1/100km angalia post zangu zote kama nimesema hvyo!

Sasa sijui tatizo ni maana ya ratio(uwiano) au tatizo ni recommandation(mapendekezo)

recommandation ratio ni 1/100km sasa unaposema mapendekezo si lazima mtu afate hvyo na wala si sheria kwa mtu kufanya hvyo ndio maana swala la ulaji wa mafuta linabaki mikononi wa mtengenezaji wa gari

Pia swala la ulaji wa mafuta kwenye magari tayali wameshalipatia ufumbuzi mm mwenyewe kuna mshikaji wangu yuko Malaysia kuna kifaa alinitumia unakiweka kwenye gari kinafanya kazi zaid ya 13 kwenye gari ikiwamo kupunguza ulaji wa mafuta kwenye gari kwa 30% so ninachokiongea nakijua na pia nimekiishi na mm nakitumia sasa mtu anapobisha tu kwa vile nikisemacho hakipo Google mm namwona Upeo wake ni mdogo sana kwa kudhani Google pekee ndio source ya Taarifa zoteee
 
Mkuu naona toka mwanzo unajichanganya tu ila kuna kitu hukuelewa kwenye post zako. Ngoja nikueleweshe kwa lugha rahisi kama ni muungwana utakubali ulipokosea. Consuption ya mafuta inapimwa kwa kiwango cha mafuta kwa lita itachotumia chombo chako kwa umbali wa kilomita 100. Na hii inatofautiana kati ya urban na highway. Tofauti na wabongo tulivyozoea kwamba lita moja inatembea kilomita kadhaa. Hakuna kitu kama 1l/100km popote pale. Tofauti na hapo utatumia nguvu kubwa sana kuelewesha watu na mwishowe wasikubaliane na hoja zako.
 
Safi sana kiongozi hats Mimi sasa sins haja ya kuuliza nadhani nimepata elimu toosha kuhusu magari
 
foolish
 
Mkuu naona hujaelewa kwanini watu wengi mnashindwa kulewana hapo juu,hapa kwetu wengi tumezoea kwamba Lita 1 inakwenda km...so and so,sasa wewe umeweka maelezo yako interms of ratio kuwa ni 1/100 hapo mtabishana mpaka asubihi.Na kama hiyo ratio yako ulioweka ya 1/100 ina maana ya lita 1 inatembea km 100 basi hata mimi sikubaliani na wewe.
 
ingia Google au Wikipedia tafuta hiyo mada yako ya lita 1= 100km[/QUOTE]

.

hajasema hi yo mkuu amesema L/100km
 
Mkuu nakuomba ukipata muda anzisha uzi kwa ajili
ya kutoa elimu.Jambo hili la mafuta linatuumiza sana
na sababu yake ni kudhani tunajua na kumbe
hatujui na ujinga wetu unaendelea kukaa,
tukiwa wakweli tutajifunza mengi juu ya yale tusiyoyajua.

Ukweli ni kwamba watanzania tuliowengi
tunanunua magari used ambayo hayaletwi na manual
of operation,Tunaendesha kwa kukariri
na hivyo hata makosa tunayaona ni sawa tu.
kwa hiyo ni vyema kama una uelewa zaidi
anzisha uzi toa darasa,tupo tunaohitaji kujifunza
asante sana kwa kunielewa.
 
hivi ww izzo akili yako inafanya kazi vizuri ratio ya gari kubwa kwenda 13km kwa lita utazan ist umeonea wap?? au lita moja kwa km 100 umesoma kwenye kitabu gani ??? hivi unawezaje lishauri gari sijui kupendekeza liende km kazaa kwa lita flani et recommended ...em na ww i recommend piki piki yenu iende 200km kwa nusu lita
 
Mm mjadala huu nilishaufunga siwezi kuwa nafanya kazi ya kuwaelewesha utadhani watoto humu kuna post zangu zaid ya 15 kama umesoma zote unaweza kujua nilikuwa namaanisha nini
 
Ebu punguza utani katika hili.... kamwe huwezi fananisha vitz na ist... ist ni gar moja tamu sana yan kuifananisha na vitz ni matusi makubwa... lile jiko la vvti lililofungwa kwenye vitz lina mashetani sana.. huwa linawah kuua cylinder head
 
Mm mjadala huu nilishaufunga siwezi kuwa nafanya kazi ya kuwaelewesha utadhani watoto humu kuna post zangu zaid ya 15 kama umesoma zote unaweza kujua nilikuwa namaanisha nini
Mkuu tofaitisha kati ya I/100km na 1/100km I/100km= L/100km na 1/100km = 1L/ 100km.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…