Viungo bora wakabaji wa muda wote top ten

Viungo bora wakabaji wa muda wote top ten

d6a08c9bb7cb2f6c410c66e961f8a05f.jpg


Rijkaard alikuwa anaweza kucheza kama defender au midfielder.
OK Haya mkuu, mi nilizoea kuwaona wakicheza kama defenders
 
Viungo "wakabaji" mwanzoni walikuwa na jukumu la kuunganisha timu kati ya defence na wachezaji wa mbele.
Ukweli ni kwamba Jose Mourinho ndo haswa kaitambulisha hii ya KIUNGO MKABAJI WA SASA na majukumu anayofanya, na shughuli hii aliianzisha kwa Makelele na Essien pale chelsea. Kwa kuwa ilifanikiwa basi kila mtu akaichukua on board na sasa imekuwa ni kama standard. Ni kama full backs, mwanzoni hawakuwa wanapanda sana mpaka alipoanzishaga kwa sana Carlos Roberto na Cafu.
Hivyo kiungo ukabaji haina muda mrefu sana dimbani. Wapo wachache waliitumiaga hii falsafa lakini kwa kiwango kidogo.
Roberto Carlos na Cafu hawakuanzisha hii kitu. Isome Brazil iliyotwaa WC ya 1994 pale USA. Cafu aliingia kama Sub baada ya mtangulizi wake kushindwa kuhimili pressure ya Azurri (chini ya Arigo Sacchi) na mfumo wao wa 3-5-2. Brazil chini ya Carlos Alberto Perreira walienda na 4-4-2.
 
Viungo "wakabaji" mwanzoni walikuwa na jukumu la kuunganisha timu kati ya defence na wachezaji wa mbele.
Ukweli ni kwamba Jose Mourinho ndo haswa kaitambulisha hii ya KIUNGO MKABAJI WA SASA na majukumu anayofanya, na shughuli hii aliianzisha kwa Makelele na Essien pale chelsea. Kwa kuwa ilifanikiwa basi kila mtu akaichukua on board na sasa imekuwa ni kama standard. Ni kama full backs, mwanzoni hawakuwa wanapanda sana mpaka alipoanzishaga kwa sana Carlos Roberto.
Hivyo kiungo ukabaji haina muda mrefu sana dimbani. Wapo wachache waliitumiaga hii falsafa lakini kwa kiwango kidogo.

Roberto Carlos na Cafu hawakuanzisha hii kitu. Isome Brazil iliyotwaa WC ya 1994 pale USA. Cafu aliingia kama Sub baada ya mtangulizi wake kushindwa kuhimili pressure ya Azurri (chini ya Arigo Sacchi) na mfumo wao wa 3-5-2. Brazil chini ya Carlos Alberto Perreira walienda na 4-4-2.
Sisemi kwamba alianzisha, ila ndio full backs walioanza kutumiwa ktk stailo hii na makocha wao.
 
Yeah! Wanasoka wenzangu nipo hapa kutoa List fupi wa viungo wa kukaba bora wa mda wote kwa upande wangu katika tasnia ya soccer .
1.Sergio Busquets - kwa upande wangu huyu jamaa ni bora kabisa katika viungo wote kutokana na uwezo wake wa kuziba matobo na kupiga killer pass na unyumbulifu wake
2.Gatusso- huyu nampa nafasi ya pili kutokana na ubora wake katika kukaba na roho mbaya ya unyama unyama
3.Claudia Makelele- kijana kutoka ufaransa nae alikuwa ni bora kabisa katika nafasi yake hiyo
4.Ngolo Kante- kijana pia kutoka ufaransa ambaye anakipaji cha hali ya juu katika kusakata kabbu katika hiyo nafasi
5.Cassemiro - a.k.a the Tank ni kipaji kinachochipukia lakini kutokana na ubora wake nampa nafasi ya tank
6.Xavi Alonso mhisipaniola fundi nae ni xavi Alonso anasifika kwa kupiga long passes na kukaba .


Japo heading inasema ni top ten naomba niishie 6 ilikuwapa nafasi na wachangiaji kumalizia hao wa 4 waliobaki
Una umri gani,tatizo la utoto lakwako linakusumbua
 
Uliposema Viungo bora wa kukaba wa muda wote nilitegemea nione majina haya kwa haraka sana;

Claude Makelele
Roy Keane
Patrick Vieira
Marcon Sena
Lothar Matthiaus
Didier Deschamps
Frank Rijkaard
Gilberto Silva

Na wengineo wa kariba hiyo. Sasa ninapoona akina Sergio Busquet ndio namba moja nabaki kushangaa!
Hivi lidondo alikuwa ngapi
 
Uliposema Viungo bora wa kukaba wa muda wote nilitegemea nione majina haya kwa haraka sana;

Claude Makelele
Roy Keane
Patrick Vieira
Marcon Sena
Lothar Matthiaus
Didier Deschamps
Frank Rijkaard
Gilberto Silva

Na wengineo wa kariba hiyo. Sasa ninapoona akina Sergio Busquet ndio namba moja nabaki kushangaa!
Soma ID yake ndio utaelewa kwanini kwamuandika huyo sergio
 
mie nilifikiria utaanza na wa kwetu hapa Tanzania kama akina Mohammed Richard(Adolf),Nico Njohole,Aluu Ally etc etc ...
 
Hivi lidondo alikuwa ngapi
Lidondo ndio nini mkuu? Tusiharibu majina ya watu. Anaitwa Fernando Redondo " El Prince " alikuwa anacheza namba 6 ( Deeplying Midfielder ).

Alikataa kwenda Kombe la Dunia mwaka 1998 na kikosi cha Argentina mara baada ya kuambiwa anyoe nywele zake na kocha wake Dani Passarella.
Gwiji wa soka wa Argentina Maradona alijitahidi kumshawishi lakini Redondo aliendelea kugoma.

Licha ya kujaliwa kipaji maridhawa cha kusakata kabumbu alishindwa kuwika kwa muda mrefu kutokana na muda mwingi aliutumia nje ya Uwanja kuuguza majeraha yake.

Ni mmoja kati ya viungo bora kutoka Amerika ya Kusini, ambao walijitengenezea ufalme barani Ulaya, na hii ilidhihirika pale Real Madrid walipomuuza kwenda Ac Milan hali iliyofanya Madridista ( Wanazi wa kutupwa wa Real Madrid ) kuandamana kupinga kuuzwa kwa staa huyo.

Ahsante!
 
Hapa tunapoteza muda kwa Kubishana na Mtu asiyejua Mpira....

Kwanza Unaposema Kiungo mkabaji bila Ya Kufafanua basi bado tunaojua Mpira Hatujakuelewa!!!
Labda nianze Kukwambia tu manake Najua Hunielewi...

AINA YA VIUNGO WAKABAJI NA UBORA WA STYLE YAO
Note: Hapa nitawazungumzia Kuanzia Mwaka 1998 mwaka nilioanza Kufatilia Mpira wa Europa....

1) Deep-lying defensive midfielder:
Hapa Hapana Ubishi CLAUDIO MAKELELE atakuwa ni Bora na sijaona Mwengine Kwa Wakati wote Niliotazama Mpira (From 1998 mpaka sasa...)

2) Holding Midfielder:
Hapa Ninathubutu Kusema EDGAR DAVIDS ni best kiasi ya kwamba sijapata ona mpinzani..

3) Deep-lying Playmaker:
Hapa ninampa Credit ANDREA PIRLO bila ya Wasiwasi wowote...

4) Box-to-Box defensive Midfielder (Regista)
:
Hapa Nampa Credit Yaya Toure bila ya Wasi wasi wowote...

5) Destroyer-Defensive-Midfielder:
Hii Ndiyo Style Pekee anayoweza Kuingia SERGIO BUSQUET! Lakini Hawezi Kuwa Bora Kuliko Wengine Kama MICHEL ESSIEN au ROY KEAN coz Hawa Wamebeba Sifa Za Ziada Kama vile Holding and Box-to-box yao ilikuwa bora Zaidi.

Note: Hapa nazungumzia Modern Football Na wala sizungumzii Kina Ronald Koeman! Sikuwafahamu...

Usione Mchezaji Anacheza tu Midfield area ukaanza kuwagia sifa! Kwanza jifunze je ni aina gani Ya Mido style anayocheza?
Ndiyo wewe unapoekewa Matic, Kante na Herrera Ukaanza Kuchanganyikiwa hujui Umchezeshe Yupi!!
Kumbe Hapo Kila Mmoja ana sifa yake Aliyomzidi Mwenziwe..
Kwa Mfano iwe Kante, Matic na Herrera Wote hawa wanacheza Man U..

√ Siku ya Mechi Ya Liverpool Chezesha Kante (Ana sifa ya Box-to-box & Holding and Destroyer Midfielder) lakini Kakosa Sifa ya Playmarker... Kwahiyo Yeye peke yake Anaweza Kusimama na Viongo 3 akawaharibia tu.

2) Siku Ya Mechi na
Chelsea Chezesha Nemanja Matic (Jamaa Ni Best modern box-to-box na Playmarker) lakini Si Mzuri sana Kwenye Destroyer na Holding Midfielder...

3) Kwenye Mechi na Man City Chezesha Kante na Herrera at the Sametime.. (Herrera ana sifa ya Holding and deep Destroyer) lakini Hana sifa ya Playmarker, Creater, Box-to-box...

So Kabla ya Kupost Pumba Kwanza Jifunze Soccer.
 
Swadakta kabisa hujakosea maana makombe ndyo yanatuonyesha status ya mtu


Nani Kakwambia Makombe ndiyo yanaonesha Status ya Mtu?

Kwahiyo Kwakuwa Willian wa Chelsea ana Makombe mengi Kuliko Pogba, Coutinho Kwahiyo ni Bora Kuliko hao au?
Makombe ni Mshikamano Wa Wachezaji Zaidi ya 20+ na Wala Si Kudetermine Uwezo Wa Mtu Mmoja!
Hata Danny Walbek na yeye Alibeba Makombe akiwa Man U! Je ni Mchezaji?

Uwezo wa Mtu Binafsi Tuambie labda Kafanya nini cha ajabu?
 
Hoja zote ninazo anakila kombe na hajawahi kupigwa benchi na yeyote

Kwahiyo Kutokaa Benchi ndiyo Kigenzo Cha Uchezaji bora wa Wakati Wote duniani au Mchezaji Bora wa Timu Hiyo asiyokaa Bench?
Coz hata Casemiro hakai Bench!!!
 
Yaani kweli wewe umeanza kuujua mpira Mwaka 2010, Carlos Dunga aka The Captain yupo wapi hapo? bila kumsahau Didier Deschamps.
 
Back
Top Bottom