Viungo Mzamiru na Kanoute

Kerosine Bal

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2014
Posts
247
Reaction score
231
Hongereni Simba kwa kusonga mbele group stage. Leo mechi niliiangalia kwa hawa viungo wa kati wa simba Mzamiru Yasin na Kanoute a.k.a Putin.

Kwanza majina yao ya utani yanaakisi wanachokifanya uwanjani (Kiungo Punda, punda kweli kweli na Vladimir Putin roho ya paka ukizubaa anakutoa roho) hahahaaaaa wanafurahisha sana. Mzamamiru kazaliwa upyaaaa.

Wanakaba, wanaunganisha timu, wanasogea kushambulia pande zote, wanachukua mipira kwa mabeki na kusogea nayo mbele hakika wameiva.
Bonge la combination. Nungunungu atulie kwa kweli anacheza kifaza sana ye atasubiri mechi lainilaini.

Group stage tunategemea burudani zaidi kutoka kwao.
 
Hawa waliopigwa 6 na Namungo,wapimeni wakikutana na kina Fei
 
Putin roho mbaya sana. Yule dogo asipopewa kadi nahisi anakosa amani.

Tatizo la kiungo punda ni kwenye kutulia wakati akiwa na mpira ila kwenye kukata umeme ni superb kabisa.
 
Kanoute sasa hivi ni free role anapandisha team haraka chama na mzamiru wanacheza pembeni yake maana hana speed ndo maana anaitwa Vladimir Putin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…