Viupele hivi vinaota mara kwa mara kwenye uume na vinauma vibaya mno, ni ugonjwa gani?

Ni kweli, hii ni herpes simplex(HSV).
Umepata au ulikuwa nao hapo kabla.

Kuna aina mbili:
1: Herpes simplex(HSV1)
Hii husababisha vidonda mdomoni na nje ya mdomo au kuzunguka pua. Hali hii huandamana na homa za usiku na uchovu. Kwetu sisi wengi husema"malaria inatoka" japo si uhalisia.

2: Herpes simplex(HSV2)
Hii huambukiza mtu kwa njia ya ngono. Kawaida ukipata maambukizi, vipele vyake hupona ila virusi vyake havitaondoka mwilini. Kawaida havina maumivu bali muwasho kwa mbali, maumivu makali hutokea unapovipasua.

Utaendelea kupata vipele vya aina hii maeneo husika kadri unapopata changamoto za mfumo wa kinga kama ikiwa na stresi, lishe mbovu/isiyo kamili kwa muda mrefu au kazi ngumu nk.

Kawaida kuwa havihitaji tiba kwani hupotea baada ya wastani wa wiki moja. Ingawa dawa za kupaka kama dhidi ya virusi na za kuzuia muwasho na kukausha huweza kutumika.

Wengi wamekuwa wakiingizwa gharama ya kutibu visitokee tena kwa kuchomwa sindano mbalimbali bila mafanikio.

Dawa au kitu muhimu ni:
1: Weka mwili wako kwa kuwa na afya njema
A: kula mlo kamili
2: mazoezi mepesi
3: epuka kuishi na stresi
4: usiwe mtu wa kujichosha sana
5: pata muda wa kupumzika
6: Nk

2: Tiba
Hutolewa kwa dozi tofauti unapokuwa na vipele walau vimetokea mara 6(kama nakumbuka vyema) kwa mwaka. Kuna dozi aina tofauti ya dawa husika. Hii hulenga kupunguza kiadi cha idadi ya virusi na utokeaji wa vipele.

Kiafya
Hakuna madhara ya moja kwa moja kwa mhusika kuhusu uzazi, urefu wa maisha nk.

Ukisha kuwa na shida hii upo uwezekano wa kuendelea kuambukiza mwenza wako wakati una vipele au hata vinapokuwa vimekauka. Mjari na kumkinga mwenzako.
 
Utajuaje kama una herpes
 
Una govi
 
Utajuaje kama una herpes
Kwa maeneo yote mawili, unapata vipele vilivyojaa maji/clear fluid. Havisababishi maumivu mara nyingi huwa vimekaa pamoja viwili au zaidi. Vyepesi kupasuka na vikipasuka huleta maumivu. Mfano wake ni vile vinavyotokea maeneo ya mdomo au pua/wengi husema malaria inatoka.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…