Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Salaam ndugu zangu, tuvitazame vivumishi kwa mapana yake. Katika andiko hili tutafafanua dhana ya vivumishi, aina zake pamoja na kutoa mifano mbalimbali. Twende pamoja;
VIVUMISHI
Kivumishi ni neno au fungu la maneno linaloeleza zaidi juu ya nomino. Kivumishi ‘huvumisha’, yaani hueleza mtu namna alivyo au kitu nama kilivyo, kinavyofikirika au kufikiriwa. Pia huonyesha idadi fulani ya kile kinachozungumziwa. Kuvumisha ni kutoa habari.
Tunaweza pia tukasema, vivumishi ni maneno yanayosifu au kufasili sura za nomino.
AINA ZA VIVUMISHI
1. Vivumishi vya sifa
Haya ni maneno yanayotaja sifa au tabia ya nomino inayovumishwa. Kwa mfano, Mtoto mzuri amefaulu mtihani.
2. Vivumishi vya idadi
Hivi ni vivumishi vinavyoonyesha idadi ya nomino zinazozungumziwa. Vivumishi hivi huweza kuwa:
3.Vivumishi vioneshi (Vya ishara)
Vivumishi vinavyotumika kuonyesha mahali kitu kilipo kwa njia ya kuashiria. Kwa mfano, Gari lile liliegeshwa karibu na duka kuu.
4. Vivumishi viulizi
Vivumishi vinavyodhihirisha kuwepo kwa swali. Hutumiwa ili kuuliza swali kuhusu nomino. Kwa mfano, Rahma amejifungua mtoto gani?
5. Vivumishi vimilikishi
Vivumishi hivi huelezea ni nani anayemiliki nomino. Kwa mfano, Kikombe changu ni kidogo.
6. Vivumishi vya majina
Hizi ni nomino ambazo hutumika kama vivumishi. Hutumika ili kuelezea zaidi maana ya majina mengine. Vivumishi hivi vikiwa peke yake huwa ni majina tu, lakini vikiunganishwa na majina mengine hufanya kazi ya wasifu (yaani kusifu) au kuelezea jina linalotangulia. Kwa mfano, Mwanamke tajiri amekuja shuleni.
Tajiri ni nomino iwapo itatumika bila neno mwanamke. Kwa mfano, tajiri amekuja shuleni.
7. Vivumishi vya pekee
Hivi hutokana na mizizi ‘-ote, -o-ote, -ingine, -enye na -enyewe’. Kwa mfano, Wanafunzi wengine wamefika shuleni.
8. Vivumishi vya A-Unganifu
Hivi ni vivumishi vinavyoundwa kwa a-unganifu na hutumika kutoa sifa za nomino. Kwa mfano, daftari la mwalimu lipo juu ya meza.
9. Vivumishi virejeshi
Hivi ni vivumishi vinavyotumika kurejelea nomino. Hujengwa kwa kutumia ‘O-rejeshi’. Kwa mfano, mtoto huyo alikunywa uji wa wimbi.
10. Vivumishi vya kusisitiza/ sisitizi
Hivi hutumika kusisitiza nomino iliyotajwa hapo awali. Kwa mfano, Daftari lili hili ndilo alilotumia.
Pia Soma:

- Vya idadi mahsusi/maalum (idadi dhahiri). Kwa mfano, wanafunzi wawili walishiriki mashindano ya uandishi wa insha.
- Vya idadi ya jumla(idadi isiyodhahiri). Kwa mfano, watu wengi walihudhuria harusi hiyo.