Naungana na wewe moja kwa moja, hata mimi inanishangaza sana kuexport raw materials! Hivi inachukua miaka mingapi kugundua, kufanya research na kufanya maamuzi na kutekeleza uamuzi wa kuacha kuexport raw materials?
Manake tumeyasikia haya sana majukwaani, utekelezaji wake hauonekani.
Mfano madini hadi leo tunexport raw!!! Hivi kuna kiongozi ambaye hajui tunapoteza sh ngapi?
Ni jambo la kusikitisha sana.
Tanzania tunachohitaji ni rais mjasiri na mzalendo, sio vyeti, watu wenye vyeti wapewe kazi za kushauri na kutekeleza.
Kama alivyosema Cheyo miaka mingi huko nyuma, ni muhimu watu wa karibu na migodi wakae kidhahabu dhahabu, watu wenye gesi wakae kama matajiri wa gesi.
Kila resource itawaliwe na walio hapo si serikali kuu, serikali kuu itoe ushauri an ipate commission in %age.
Kama watu wa kilimanjaro wanavyoupenda mlima, wanajua unachowapa, je watu wa mara wanapenda migodi yao?
Hivi kuna mtu anafuatilia viwanda vilivyopo katika makazi ya watu, je inashindikana kuhamisha watu au viwanda? basi tuna tatizo kubwa sana.
Nawatakia wizara ya viwanda mafanikio mema